Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Ngoja nikushauri
Mahal ni wap
Aina ya nyumba
Ya kazi gan
Vifaa umenunua kwa bei gan
Fundi awe namna gan
Aina ya vifaa
Unajenga wakat gan
 
Bei ya vifaa vya ujenzi imepanda maradufu!
Mfano nondo 12MM imefika shs 22,000/- na matumaini ya kupungua hayapo, cement nayo imepanda n.k
Kwa hiyo Wewe anza utakaishia utasubiri ukipata hela nyingine utaendelea!
 
thanks kwa ushaur mzur mkuu
 
Ohoo... tiles? Tiles tena dogo??? Hebu acha masihara basi.

Vipi umejaribu kuwaza kuwa lazima utahitaji choo??
ndo maana nikafata kaushaur humu mkuu nikijua naweza pata mawazo mbadala
 
Wala usiwe na hasira kwasbb hili ni jukwaa la great thinkers kwahiyo sitegemei km great thinker unilishe maneno matupu. Umeelewa ulichokiandika? Nafikiri hata ww ukisoma baadae utashangaa sana kwa ulichokiandika. Nilitegemea utanipinga kwa fact huku ukitoa mchanganuo wa A-Z kumbe maneno matupu. Nasubiria huo mchanganuo wako
Nimekujibu kutoka na qoote yako ya dharau...ungeuliza bila dharau ningekujibu vizuri na ufafanuzi ningekupa .
 
unajenga vizuri kuta msingi na kuta zake kwa kuimarisha msingi ila fundi awe mstaarabu na aelewe lengo lako na kila kitu ununue mwenyewe
 
mimi nina vi boy kota vyangu vyumba viwili kimoja master, sebule na jiko HUWA najenga kuta mpaka mwisho kwa 5m
 
Tofari 1400@1000 ni1,400,000.inabaki laki sita .fundi bado,mchanga bado,kokoto bado,mbao bado,nondo bado,maji bado bati bado,misumari bado,kuchimba msingi bado,madirisha na milango bado ,fundi hajaiba kidogo.Labda ujenge mbavu za umbwa.

Duh! [emoji23][emoji23]
 
nataka nyumba ya kawaida tu chumba na subure kama iz tunazopanga mjin
Unaweza kaka, sema jaribu pia kutafuta vifaa vya bei rahisi vya ujenzi, pia fanya tathmini kwanza kabla ya kuanza ujenzi mkuu
 
Mkuu unajenga na chenji inabaki.

-Chumba na sebule ni tofali 800 tu. = 800,000/=
-Bati 15 = 150,000/=
-Cement Mifuko 10 = 140,000/=
-Ufundi 270,000/= Msingi hadi Juu
-Linta Nondo 6 na Mifuko miwili ya cement Kokoto Viroba 12,Mchanga Yebo moja = 182,000/=(120K+12k+50k)
-Mbao 20(4x2 and 2x2) + Misumali =150,000/=
-Mlango m1 na madirisha matatu = (150k +50k x3 ) =300,000/=

Total ni 1,992,000/=

Hayo ni Mahesabu Maximum sana,Kuna vitu unaweza kupunguza kwenye bei ya mlango,dirisha au kwenye bati unaweza ukanunua zile za reject ambazo nzuri kwa 6000 na sio kwa elfu 10.

Kwenye ufundi mnaweza mkabargain kwa tofali mie nimeweka 250 kuna mafundi wa kitaani hadi 200 kwa tofali.
 
Unajenga inatemegemea unataka iwe na ubora gani...achana na wanaokukatisha tamaa.
Habari zenu wakuu,

Kwenye shughuli zangu za hapa na pale nimepiga bingo nna milion mbili cash ndani nataka kuondokana na maisha ya kupanga nna kiwanja Goba-Mbezi, je nitaweza kujenga vyumba viwili nikaamia kwa gharama ya milioni2.

Msaada wenye uzoefu please
Unaweza mkuu...usiwasikilize wanaosubiri maimilioni, adha ya kupanga ni mbaya sana, unajega vizuri na zaweza kubaki, fundi mmoja tu, wewe msaidizi..na unahamia safi kwako...
 
Mkuu unajenga na chenji inabaki.

-Chumba na sebule ni tofali 800 tu. = 800,000/=
-Bati 15 = 150,000/=
-Cement Mifuko 10 = 140,000/=
-Ufundi 270,000/= Msingi hadi Juu
-Linta Nondo 6 na Mifuko miwili ya cement Kokoto Viroba 12,Mchanga Yebo moja = 182,000/=(120K+12k+50k)
-Mbao 20(4x2 and 2x2) + Misumali =150,000/=
-Mlango m1 na madirisha matatu = (150k +50k x3 ) =300,000/=

Total ni 1,992,000/=

Hayo ni Mahesabu Maximum sana,Kuna vitu unaweza kupunguza kwenye bei ya mlango,dirisha au kwenye bati unaweza ukanunua zile za reject ambazo nzuri kwa 6000 na sio kwa elfu 10.

Kwenye ufundi mnaweza mkabargain kwa tofali mie nimeweka 250 kuna mafundi wa kitaani hadi 200 kwa tofali.
Maji ya ujenzi?
Gharama za usafiri wa hivyo vitu?
 
Maji ya ujenzi?
Gharama za usafiri wa hivyo vitu?
Ungekuwa unajua gharama zake wala usingeuliza Mkuu,amesema anajenga goba,goba kuna Hardware kibao wengine ukinunua mzigo kwako anakuletea vifaa hadi site bure kabisa ila anakuwa ameweka 500 ya usafiri ambayo nimeiweke kwenye vifaa,Kwenye kupandisha tofali vyumba viwili maji hayatumiki mengi na hayazidi hata dumu 20 kwa project yote ambayo sawa na Tsh 4000 au unaweza kununua lile la Boza la Tsh 10 lita 1000.
 
Jenga room moja master, ila lazima uwe na ramani ya nyumba nzima, ili ukipata pesa umalizie nyumba nzima
 
Back
Top Bottom