Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Kwahio bajeti haitakuwa 2m tena itakuwa 2.3m
inaweza kuzidi ikafika hata milioni sita ila kwa milioni mbili anaweza kuhamia.
nasema hivi ninao mfano hai mwaka 1976 babu yangu alisumbuliwa na mwenye nyumba mjini dar ikabidi aamue kuhama na kuhamia nje ya mji kwa siku ya kwanza tulilala nyumba imefungwa vito tuu lakini bati imepigwa na nakumbuka vilikuwa vyumba viwili na sebure.
siku ya pili upande mmoja ukakandikwa kwa udogo na ndani ya wiki mbili nyumba yote ilikwisha.
ninachokumbuka babu alimlipa fundi wa kufunga fito na kupiga bati na pia kununua fito,kamba na mijengo lakini zoezi la kukandika tulifanya wenyewe babu akikanda udongo mimi, mkewe na shemeji yake tukikandika nyumba.
lakini baadaye palibadilika tukajenga nyumba nzuri na yamaana.
ninachotaka kusema kikubwa hapa sio fedha kiasi gani inatosha kujenga lakini kubwa je unao msukumo wa kutosha toka katika nafsi yako na roho yako na utashi wako kwamba umepania kuhama na kujenga?
kwa hiyo kwa chochote tufanyacho tunatakiwa tuamini kuwa kinawezakana, tufanye sehemu yetu na mwisho kitakuwa.
ziko success story nyingi ambazo nikikueleza hauwezi amini nimeshuhudia nikiwa mwanzo siamini lakini leo nayaona mafanikio yao na najifunza kutoka kwao.
 
Bajeti tosha hiyo lakini usitake kuweka mpaka milango na madirisha ya aluminium, cha kufanya jenga kwa awamu pamoja na tempo toilet kisha hamia.
....
Kujenga kwa awamu ni kama hivi, jenga kota room hata moja pembeni mwa kiwanja chako ukiwa na Imani in future days utavunja na kupandisha 'hekalu' ili ujisitiri kwa muda huku ukiwa na uchungu wa kung'atwa na mbu and soon utaona utakachofanya mkuu.
 
Kwa kuwa una plan kujenga chumba kimoja weka bajeti ya tofali 400 hadi 500 inategemea Na Kiwanja kilivyo. Mabati matano, mbao 4*2 wastani 4 Na mbao 2*2 = 4. Nondo 2.

Anza Na hapo.
 
hilo mbwebwe watu wanaamia kwanza kwenye vumbi kisha kila mwezi ile kodi ya nyumba inasaidia kuboresha sehemu ya nyumba.
nyumba nyingi za kitunda,kiwalani na mbagala zimejengwa kwa mtindo huu kwakuwa hawakuwa na jinsi ya kuiba au kukopa fedha nyingi kwa pamoja.
Mzee unaweza kuamka kwenye tope siku ya mvua
 
Habari zenu wakuu,

Kwenye shughuli zangu za hapa na pale nimepiga bingo nna milion mbili cash ndani nataka kuondokana na maisha ya kupanga nna kiwanja Goba-Mbezi, je nitaweza kujenga vyumba viwili nikaamia kwa gharama ya milioni2.

Msaada wenye uzoefu please
Labda ujenge kibanda cha bati
 
Ukija pm nitakupa ushuhuda wangu,na naamin hitajuta na utaanza ujenzi Mara moja.kwa kuwa una kiu ya kuhamia kwako inawezekana kabisa,usirudi nyuma tafadhari

Mkuu kama hutajali tuwekee tu hapa huo ushuhuda wengi tunawakilishwa na mtoa mada hapa. Tukikufuata wote huko pm utachoka kutufafanulia. tafadhali mkuu
 
Tofari 1400@1000 ni1,400,000.inabaki laki sita .fundi bado,mchanga bado,kokoto bado,mbao bado,nondo bado,maji bado bati bado,misumari bado,kuchimba msingi bado,madirisha na milango bado ,fundi hajaiba kidogo.Labda ujenge mbavu za umbwa.
Hahahababa c mchezo
 
Choo vipi?
Ceiling board/gypsum?
Vifaa vya umeme?
Plumbing?
Plaster/rangi?
Rough floor ndani?

au anapanga matofali tu anaishi bila umeme,maji na choo?
Ana mil2 anataka ahamie,hiyo ndio solution,Choo ni very simple Mkuu kuna cha matairi ya gari au pipa,lengo ni kuhamia kwanza,hayo ya gypsum,wiring,plumbing etc baadae sana .
 
Jenga ya udongo piga plasta nje na ndani hata milioni haiishi.
 
Back
Top Bottom