Madhara ya kuzaa nje: Familia inajuta mpaka leo kwa uamuzi walioufanya kwenye urithi wa kaka yao. So sad

Record Man

Member
May 25, 2023
77
343
Habari za weekend,

Jana kuna dogo wangu mmoja alikuwa wanaongea na mzee na mimi nilikuwepo home alikuwa anawaambia madhara ya kuzaa nje ya ndoa yanayoweza kujitokeza baadae.

Alitoa kisa kimoja hivi cha kweli kabisa.

Ilikuwa hivi.

Kulikuwa na Baba mmoja alizaa na mkewe watoto 3, wakike 2 na wakiume 1, watoto asilimia kubwa walifanana na mama yao.

Mzee alisema kuwa walikuwa wanapenda na kwenye ile familia tena sana.

Mtoto wake wa kwanza kwenye ile familia aliolewa na mzungu wa USA. Na wa pili ambaye ni binti pia alikuwa anasoma USA. Ila wa mwisho ni wakiume alikuwa hapa bongo.

Yule Baba alikuja kuugua kisukari ambapo ilimpeleka mpaka kufariki. Siku ya msiba alikuja mdada mmoja ana watoto 2 wakiume wamefanana sana na Baba. Mmoja kama miaka mitano hivi na mdogo wake.

Watu ndiyo wakajua kumbe Baba alikuwa na nyumba mbili. Japo watoto wa nje walipishana umri mkuwa tuu na watoto wa ndani ya ndoa.

Mama wa ndoa alishituka sana lile tukio na watoto wake. Kumbe Mume wake alishawatambulisha watoto kwa baadhi ya ndugu.

Baada ya msimba. Kwenye mgawanyo wa mali walisema hizi mali ni za kaka yetu na hawa watapata , waliogombana mapaka mahakamani ila ilishindikana walimwambia tuu mama kwa sababu watoto walitambulishwa. Walikuwa na nyumba kadhaa na mali zingine.

Waligawa sawa na tuu na wengine. Kitendo kile kilimpelekea mama kupata msongo wa mawazo mpaka kufariki. Ile ishu iliwaumiza sana watoto wake wakaamua kumzika tuu mama yao.

Mwishowe wale watoto waliuza mali zote za Baba yao wakamchukua mdogo wao wa kiume na kwenda nae USA.

Mpaka leo wapo USA na hawana mawasiliano na familia yao upande wa baba tangu waondoke.

Na yule binti baada ya kuchukua mali alikata mawasiliano na ndugu wa Yule Baba aliyezaa nae.

Alichukua nyumba moja, mwishowe aliolewa na mume wake alimwambia kuwa anataka watoto wadogo wawe wake kwa hio wabadili jina la mwisho la watoto wawili.

Aliishi kwenye nyumba ya yule Baba aliyopewa na mume mpya.

Ni ishu ya kweli yani ndugu wale mzee alisema walijilaumu sana baadae.

JAMANI WANAUME TUACHE KUZAA NJE YA NDOA , KAMA IMETOKEA BASI KUWA MAKINI MADHARA BAADAE YASIJITOKEZE.
MI NI HAYO TUU FRIENDS.
 
Daaa mkuu unanikumbusha ishu mmoja nilishuhudiaga kipiendi namaliza chuo ni kama 13 years ago.

Baba na ndoa yake alichepuka nafikili kipindi mkewe anamimba ya pili. Mchepuko alipata mimba na kujifungua mtoto wa kiume.
Maana mtoto wa mchepuko anaumri sawa tuu na mtoto wa pili wa ndoa.

Yule baba alipata watoto 2 wa kike so wakiume ni wa nje.
Alinyamaza kama 29 years baadae akaja kufariki. Yeye alikuwa wa kwanza kwao.

Kumbe alishamtambulisha mtoto kwa dada zake. Siku ya msiba alikuja watu walishangaa sana.

Kwenye mgao nae alichukua.

Ila baada ya kuchukua alitokomea kabisa , yani mpaka leo hana hata mawasiliano na shangazi na hata dada zake , yeye anaendela na maisha tuu.

Nafikili kwa sababu hawakuishi pamoja.
 
Hayo madhara yapo wapi? Kwahiyo ulitaka uyo mjane mchepuko asiolewe?
Na kuhusu kubadili majina ya watoto hiyo ni hadithi ya kufikirika ili kunogesha story
Hivi umesoma vizuri alivyoeleza ujaona kifo hapo cha mama huyo.

Fikilia watoto wa kaka yako kabisa wa baba mmoja na mama mmoja, wanawasusa na kuwasahamu kwa kitendo kilichotokea kwa mama yao.
Utajisikiaje?

Kwa hio unaona ni sawa tuu.
Hayo ndo madhara yenyewe ujayaona mkuu
 
Kitendo kile kilimpelekea mama kupata msongo wa mawazo mpaka kufariki.
Msongo wa mawazo wa Nini na vitu vya kupita hivi uchoyo, ubinafsi ndivyo vyatutesa wanawake.

Tena mnagawana siyo Kwamba wanachukua vyote. Jamani maisha haya siyo magumu kiasi hicho.

Kila kitu ni ubatili mtupu na hakuna tutakachozikwa nacho....aisee🙌
 
Kwangu watoto wa nje watarithi jasho la Baba yao, jasho langu haliwahusu kamwe....ndo maana naipenda Sheria ya mirathi ya kiislamu.....jasho la mke linatolewa linawekwa Kando kinachobaki kinapigwa pasu, na mke anarithi kwenye Hicho kinachobaki.
Lkn hata sheria ya mirathi iko hivyo mali zilizopo mnagawana nusu kwa nusu bada mwenza akifariki kwenye ile nusu yake ndo mnarithi tena kwa maana ya mke na watoto.

Sema ndo hivo mahakimu wanaoendesha hizo kesi nao ni binadamu, ukichangana na vikao vya ukoo mtu anaona nini cha kufia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom