Jamani, Msikimbie majukumu ya watoto wenu wa nje. Ukizaa jua kuna kulea mtoto

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Habari wa jf.

Kuna rafiki yangu mmoja alioa mwanamke mwenye mtoto tena mapacha ni wakike tupu. Ila wao wanakaa kwa Baba yao na Baba yao ashaoa na amezaa watoto 3 na mke wake huyo mwingine 1 alizaa na mchepuko ni mdogo, Kwa hio mwamba anawatito 6 home kwake.

Huyu rafiki yangu yeye anawatoto 2 tu na mkewe. Alikubaliana na mkewe watoto wake watakaa kwa Baba yake.

Sasa rafiki yangu kipato chake kiko Bomba kabisa.
Kuna kipindi mke wake alianza kung'angania watoto wake wake kukaa kwake, mume wake akamwambia kuja kusalimia sio shida wake tuu, si wanakuja na wanakaa hata 1 to 2 weeks then wanarudi home sio shida.

Sasa kuja kipindi mwishoni mwa mwaka jana watoto wake walikuja home kwake kuja kusalimia baada ya likizo kuishi bibie akagoma kurudisha watoto kwa mwenzie mkoa mwingine. Mume wake akamuuliza vipi tena aa wakae hapa hapa, jamaa akamuuliza hao likizo si ishaisha waenda wakasome. Mke king'ang'anizi.

Mkewe mbona nyumba ni kubwa tunakaa tuu, jamaa anaishi kwenye gorofa moja.

Waligombana yeye na mke, baadae jamaa kuuliza vizuri mke wake akaanza kusema anataka watoto wake wasome shule mzuri , akamuuliza kwani huko wanasoma kubaya. Mkewe anasema shule wanayosoma sio mzuri.

Kipindi hicho mkewe yeye ni mwalimu wa shule moja hivi ya private. Ila mume wake anafanya kazi kwenye shirika moja hivi office zake zipo posta kule , mshaara wake ni mnono kwa mwezi ni mnono kweli. Jamaa akaanza kufuatilia mda mpaka wa shule unaanza still madogo wapo home. Yeye watoto wake wanasoma shule mzuri wanakuja kuchukuliwa na school bus.

Jamaa kumbana vizuri mkewe, mkewe akasema kwamba mwenzie kule anafamilia kubwa kwa sasa anawatoto 6 na mambo mengi sasa anashidwa kwa sababu majukumu ni mengi. Mume wake akamwambia sasa mimi jifanyaje. Mke akamwambia nataka wakae hapapa.

Jamaa anaona aa kukbe nianze kuudumia, akalazimisha mpka watoto madogo wakarudi kwa Baba yao. Jamaa anasema mkewe alimnunuia kama 3 months, ila baadae akajirudi mwenyewe.

Hao mapacha ilitakiwa waanze form 1 mwaka huu. Kumbe mkewe alitaka mume wake ndie awe responsible wa kulea watoto wake wakati Baba yake yupo. Na anataka wasome shule mzuri.

Mimi eee ndo hayo.
Jamani ukizaa ujue Kuna kulea.
 
Mkuu wanaume wanaoacha mtoto au watoto kwa mke wake aliyeolewa na mtu mwingine huwa wanakimbia majukumu ya watoto wao hao wa nje. Afu mtoto akiwa mkubwa anakuja anamchukua na kuondoka naje ili kukata connection kati ya mtoto na step father. Ndo zao hao.
 
Just imagine unaoa single mother.
Na unachukua mtoto unakaa nae ndani, yani ndoa yako inaanza na mtoto , hata kukaa kidogo wewe na mke hata mwaka unaenjoy pamoja ndani , mnaanza na kerere za mtoto.

Huko jamaa yeye akioa ndoa yake ananza huku hakuna mtoto kwenye ndoa .
 
Mkuu natafuta watoto kadhaa wakusomesha,nadhani itakuwa swadaka yangu kwa Mwaka ujao!.

Nahitaji watoto unaowafahamu wenye matatizo ya kukosa Skool fizi ili nijipapatue nami nisomeshe ili moyo wangu uwe na amani!

Kama wapo niunganishe nao mkuu
 
Ukipenda Boga penda na maua yake, hakuna mwanamke atafurahia maisha na wewe huku watoto wake wa kuzaa wanateseka mahali fulani.. hakuna anayependa shida ni maisha tu.. kama hutaki kuwahudumia watoto wa mwanamke ulimpenda na ukakuta ana watoto. Tafuta mwanamke ambaye hajazaa muanze wote match inasoma 0-0.
 
Mkuu Baba yao yupo kabisa , hio vipi
 
Mkuu natafuta watoto kadhaa wakusomesha,nadhani itakuwa swadaka yangu kwa Mwaka ujao!.

Nahitaji watoto unaowafahamu wenye matatizo ya kukosa Skool fizi ili nijipapatue nami nisomeshe ili moyo wangu uwe na amani!

Kama wapo niunganishe nao mkuu
Nimejaribu kukutumia pm yako umefunga, kama hutojali kindly pm me nikupe details za watoto wenye uhitaji.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nina mtoto wa kike ,sio kwamba ni wa nje hapana ,mama yake tulishindwana alikuwa mke wangu wa ndoa kabisa ,natamani nimlee mwanangu ila mama yake hataki ukaribu na mimi hata nikiulizia hali ya mtoto naambulia matusi ,hataki kunipa mtoto nilemlee
Huo maza alikuwa anafanya shughuli za kuuza pombe
Sasa mwanangu akikulia kwenye mazingira ya pombe sijui itakuwaje tu
 
Option one
Jaribu kuongea vizuri na wazazi wa huyo mama wakusaudie kuongea na mtoto wao ili akupe mwanao umlee

Nenda nao pole pole

Wamarinate pole pole

Option 2
Mpeleke dogo boarding

Hata kama ni same town anayo ishi na mama ake

Pole pole unaanza kujipenyeza
 
Back
Top Bottom