Msaada: Dume zima nina aibu mbele ya wanawake

Kadi Poa

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,015
1,005
Jamani mimi nina aibu ile ya kuzaliwa (introverts) mbele ya mkusanyiko mkubwa wa watu kama vile harusini, kwenye sherehe na hata misibani.

Imeniwia vigumu sana linapokuja suala la kuwa na mahusiano na marafiki wapya hata suala zima la mapenzi na wanawake.

Hapa nilipo sijawahi kuwa na wanawake wapenzi wanaofika hata 20, sasa nimekaribia kufika umri wa kutaka kuoa ila ninajiuliza sijui nioe mwanamke wa tabia ya namna gani anayeweza kufanana na mimi.

Sijui nioe muongeji sana ili niweke balance ama awe full aibu kama mumewe hapa wakija wageni wakose wakuwachangamkia.

Naombeni msaada wa mawazo yani nimekwama njia panda.
MWENJEJI WA KIGOMA ILA SIO MRUNDI AMA MCONGO MAN
 
"hapa nilipo sijawahi kuwa na wanawake wapenzi wanaofika hata 20". Haha kwani uliambiwa unatakiwa kufikisha idadi gani, ili uwe normal?
mkuu naomba unisaidie kwa hili
nimekaribia kufika umri wa kutaka kuoa ila ninajiuliza sijui nioe mwanamke wa tabia ya namna gani anajeweza kufanana na mimi
 
Duh pole sana ila usikate tamaa nakushauri utafute mwanamke wa kati sio mkimya na sio muongeaji sana ila ukichukua muongeaji sana na akajua udhaifu wako basi atakuonea sana
 
Back
Top Bottom