Jichanganye katika maeneo yenye mahandsome na watanashati kama wewe au unaohisi wamekuzidi. Tatizo ulilo nalo linatokana na wewe kudhani una haiba nzuri sana kiasi kwamba kila mtu anakuangalia wewe au anakufuatilia katika kila kitu. Itakuwa ulikulia katika maeneo ambayo ulijikuta kuwa unasifiwa na karibu kila mtu kuwa wewe ni mzuri na blah blah kibao. Au umelelewa katika familia fulani yenye uwezo mkubwa ukilinganisha na jamii iliyoizunguka na wewe kujikuta ukiwa center ya attention ya kila mtu.
Kwa upande mwingine, kuna uwezekano unajiona mbaya kupita kiasi na kila mtu anakushangaa kutokana na kukuzwa katika mazingira ya kusakamwa sana na kukosolewa juu ya mwonekano wako.
Jichanganye na watu wenye vipaji vingi wataokupa changamoto ya wewe kuvigundua vya kwako ili uweze kuzifidia hizo hisia. Jifunze kuogelea kama ulikuwa hujui, somea matumizi ya chombo fulani cha muziki kama gitaa au kinanda n.k Kama una tatizo la kujiona handsome sana au kujihandsamisha sana, jichanganye na mahandsome wa kweli ili ujione ulipopwaya,hilo litakupa changamoto ya kujua kuwa unatakiwa kuwa na vitu vya ziada na sio mwonekano murua peke yake. Itakufanya uone kuwa unatakiwa kujichukulia kuwa ni wa kawaida na si mtu alie special sana. Kama utaendelea kung'ata kucha ukikutana na mademu, basi mtafute Psychiatrist akusaidie maana kuna matatizo mengi ya kisaikolojia na yana fumbuzi za aina tofauti.
Samahani kama nitakuwa Nimekukwaza na kama haumo kwenye makundi haya pia, nisamehe ila naamini kuna mahali patakuwa panakuhusu.