Mrope(Mb): "Hatuwezi kuokota Mawaziri mitaani, wawe Wabunge"

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Mbunge wa Bunge la JMT(CCM) ameponda hoja ya Kambi ya Upinzani ya kutaka mawaziri wasiteuliwe kati ya Wabunge. Bwana Mrope amesema kwamba taifa haliwezi kuokota mawaziri toka mitaani badala yake mawaziri lazima watokane na Wabunge. "Haiwezekani kuokota tu mtu mtaani. Lazima awe amepigiwa kura na kuchaguliwa na watu, hivyo napinga kabisa hao wanaosema mabunge wasiwe mawaziri". Bwana Mrope pia amewaponda wote wanaotumia mifano ya nchi nyingine duniani kujenga hoja yao. "Hao wanatumia mfano wa Marekani, hao Marekani wenzetu wameendelea, wana makompyuta kibao". Bwana Mrope alisisiza hoja yake huku akipigiwa makofi na wabunge walio wengi. Mheshimiwa Mrope aliyasema hayo wakati akichangia muswada wa uendeshaji wa Bunge unaojadiliwa hii leo.

PM
 
Ndio wabunge ambao watanzania wanawategemea wahoji suala la EPA,RICHMOND , hata kama wakihutubiwa utumbo wa namna gani.
 
Kama ni Mrope, hoja zake (kama hoja kweli) ni vijembe vijembe. Anaelekea kuwa mtumwa wa CCM. Haoni wala hasikii kingine chochote. Nimemfuatilia katika maelezo yake mengi; ni mtu wa kupenda ushabiki, bila hoja.
 
Kwa hiyo huyu Bwana Mrope anataka kutuambia teuzi nyingine zote za rais ambazo hazihitaji mtu kuwa mbunge huwa ni za watu wanaookotwa mitaani?

Mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu, wakurugenzi wa idara za serikali pamoja na mashirika ya umma, wote wameokotwa mitaani?

Kuna wabunge wengine wako choka mbaya zaidi hata ya watu wa mitaani.

Pointless.
 
Mbunge wa Bunge la JMT(CCM) ameponda hoja ya Kambi ya Upinzani ya kutaka mawaziri wasiteuliwe kati ya Wabunge. Bwana Mrope amesema kwamba taifa haliwezi kuokota mawaziri toka mitaani badala yake mawaziri lazima watokane na Wabunge. "Haiwezekani kuokota tu mtu mtaani. Lazima awe amepigiwa kura na kuchaguliwa na watu, hivyo napinga kabisa hao wanaosema mabunge wasiwe mawaziri". Bwana Mrope pia amewaponda wote wanaotumia mifano ya nchi nyingine duniani kujenga hoja yao. "Hao wanatumia mfano wa Marekani, hao Marekani wenzetu wameendelea, wana makompyuta kibao". Bwana Mrope alisisiza hoja yake huku akipigiwa makofi na wabunge walio wengi. Mheshimiwa Mrope aliyasema hayo wakati akichangia muswada wa uendeshaji wa Bunge unaojadiliwa hii leo.

PM

Pure NONSENSE!!...........hawa akina Mrope ndio nawaita WAVIVU WA KUFIKIRI....ni aibu na HATARI sana kuwa na wabunge wenye kufikiri/mawazo ya namna hiyo
 
Wabunge wengi ndio wanaokotwa mtaani,hawana lolote hao .

huyo mrope kama anaona nini basi nafasi za uwaziri ziwe ajira zitangazwe na ziwe na mwenye qualifications anapata.

Huo ufisadi umezidi kwa sababu hao wabunge wengi wanaogopa kuhoji wanafikiri siku moja nao watateuliwa.

kwa hiyo huyo jamaa kwa namna nyingine anatwambia wakuu wa wilaya ,mikoa na yusufu makamba wote wametoka mitaani?

Mimi nafikiri waliokua wanampigia makofi wote wametoka mtaani
 
Wabunge wa Tanzania Kaaazi kweli kweli; wako pale kumwaga pumba tu ili wasikike. Kabla ya kusimama bungeni na kuzungumza maneno ambayo yataingia kwenye hansard, mbunge anatakiwa afanye utafiti na kutathmini kile anachokisema. Wabunge wetu wanakurupuka bila kufanya tathmini yoyote kuhusu maneno yao, na hapo ndipo pumba zinapoanza kupeperuka kwa wingi kutokea huko bungeni mpaka zinatuziba macho hadi tunashindwa kuona tunakwenda wapi.
 
Jamaa anawakilisha jimbo gani? Inabidi tuanze kumwandaa mwana JF kwenda kuchukua hilo jimbo.

Hivi mbunge kama huyu anachaguliwa kwa hoja au kwa rushwa?
 
Mbunge wa Bunge la JMT(CCM) ameponda hoja ya Kambi ya Upinzani ya kutaka mawaziri wasiteuliwe kati ya Wabunge. Bwana Mrope amesema kwamba taifa haliwezi kuokota mawaziri toka mitaani badala yake mawaziri lazima watokane na Wabunge. "Haiwezekani kuokota tu mtu mtaani. Lazima awe amepigiwa kura na kuchaguliwa na watu, hivyo napinga kabisa hao wanaosema mabunge wasiwe mawaziri". Bwana Mrope pia amewaponda wote wanaotumia mifano ya nchi nyingine duniani kujenga hoja yao. "Hao wanatumia mfano wa Marekani, hao Marekani wenzetu wameendelea, wana makompyuta kibao". Bwana Mrope alisisiza hoja yake huku akipigiwa makofi na wabunge walio wengi. Mheshimiwa Mrope aliyasema hayo wakati akichangia muswada wa uendeshaji wa Bunge unaojadiliwa hii leo.

PM

Viongozi waliookotwa tu mitaani (according to Mrope's Theorem):

a) Mabalozi wote wa TZ nje.
b) Wakuu wa mikoa yote
c) Wakuu wa wilaya zote
d) Makamba na wabunge wenzake 9 wa kuteuliwa
e) Makatibu wakuu (na manaibu wao) wa wizara zote,
f) Wakurugenzi wote wa mashirika ya umma (PPF, NSSF, Tanesco, ATCL, etc)
g) Wakuu wote wa usalama (UWT, Polisi, Jeshi, Magereza, n.k.)
h) Watendaji wote wa serikali wanaoteuliwa na Rais au Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais.
i) Pretty much viongozi wote 'wasiopigiwa kura na watu'

No wonder nchi haiendelei. Watu wote hao wanaokotwa tu mitaani wakati akina Mrope waliochaguliwa na wananchi wapo?
 
kwa watunga sheria wa namna hii, sishangai kuona tanzania haina maendeleo
 
CCM people are boring....bunch of Vihiyo wa mawazo! They may be schooled, but educated fools!
 
walitaka malipo ya mbunge yawe kama nchi nyingine lakini hawataki kulinganisha mifumo yao iwe sawa na nchi nyingine. Mawaziri wanapoteza mda bungeni ndio sababu nchi imechoka. hakuna mtu wa kushughulikia wananchi katika wizara wote wanamsubiri waziri anepiga usingizi bungeni kwa miezi mitatu. What a waste of our tax money.
 
Na ile dhana ya kujaribu kutenganisha BUNGE na SERIKALI haitafanikiwa kama mawazo kama haya ya Mrope hayatapingwa kwa nguvu zote. Ukiangalia BARAZA lote la Mawaziri isipokuwa Makamu wa Rais wote ni WABUNGE na RAIS kwa mujibu wa KATIBA yetu ni sehemu muhimu ya Bunge. Bunge linaonekana kama IDARA mojawapo ya SERIKALI!
Ni lini tutakuwa na BUNGE huru litakaloweza kuisimamia SERIKALI kikamilifu?
 
Hapa naona yeye ni mbunge aliyeokotwa mtaani akaambiwa agombee ubunge huko jimboni kwake nahisi kulikuwa hakuna mgombea wakamuokota yeye agombee.Ndo maana anaongea pumba za mbao tu.....sasa huyu wananchi anawatetea kweli??anaonekana ana mawazo ya miaka 47 enzi za kila Kingunge.
 
Wabunge wengi ndio wanaokotwa mtaani,hawana lolote hao .

huyo mrope kama anaona nini basi nafasi za uwaziri ziwe ajira zitangazwe na ziwe na mwenye qualifications anapata.

Huo ufisadi umezidi kwa sababu hao wabunge wengi wanaogopa kuhoji wanafikiri siku moja nao watateuliwa.

kwa hiyo huyo jamaa kwa namna nyingine anatwambia wakuu wa wilaya ,mikoa na yusufu makamba wote wametoka mitaani?

Mimi nafikiri waliokua wanampigia makofi wote wametoka mtaani

Hapa mwanangu nakupa 5 zote.
Akina chitaliho ni wengi humo ndani ya mjengo.
Mbunge anatetea upuuzi na watu wa sampuli yake wanapiga makofi.
 
Jamaa anawakilisha jimbo gani? Inabidi tuanze kumwandaa mwana JF kwenda kuchukua hilo jimbo.

Hivi mbunge kama huyu anachaguliwa kwa hoja au kwa rushwa?
Mmh nafikiri ni kibaraka wa mafisadi ndio maana anaweza kuongea pumba.Mtu mzima hovyooooooooooooooooooooooo
 
Ninasikitika sana kwamba kwa mujibu wa Mrope, muungwana alituwekea waziri wa fedha (meghji) wa kuokotwa mitaani
 
Ninasikitika sana kwamba kwa mujibu wa Mrope, muungwana alituwekea waziri wa fedha (meghji) wa kuokotwa mitaani

Mbona hiki ni kioja,

Kimsingi Tumepoteza Mweleko hapa Jf,kwa kipindi cha miezi miwili tumekuwa wazungumaji wa hoja dhaifu sana na kama tukiendelea hivi...watu watatupuuza,Meghji kabla ya kuwa waziri ilipewa Ubunge na hii ipo kisheria..sasa tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom