Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,443
Bwana Mrope pia amewaponda wote wanaotumia mifano ya nchi nyingine duniani kujenga hoja yao. "Hao wanatumia mfano wa Marekani, hao Marekani wenzetu wameendelea, wana makompyuta kibao". Bwana Mrope alisisiza hoja yake huku akipigiwa makofi na wabunge walio wengi. Mheshimiwa Mrope aliyasema hayo wakati akichangia muswada wa uendeshaji wa Bunge unaojadiliwa hii leo.
----------------
Hivi ni kitu gani kilichowafanya watu wazima hawa kushangilia na kumpigia makofi Bwana Mrope.
Swali zuri sana na jibu lake pia ni rahusi sana.
(a) Wabunge wengi hugonbea wakiwa na matumaini ya siku moja kuukwaa uwaziri; kwa hiyo wazo la kuondoa utaratibu wa wabunge kuwa mawaziri liko kinyume na utashi wao wa ubunge.
(b) Maneno ya Mrope yanaonyesha kuwa Wabunge wana thamani kubwa, yaani siyo wa kuokota mitaani. Kama wewe ungekuwa mbunge ungejisikiaje katika mazingira hayo kama siyo kuunga mkono tamko hilo?