Lissu awalipua mawaziri, wabunge kwa unafiki wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii

Status
Not open for further replies.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,820
1,195
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana amewalipua baadhi ya mawaziri na wabunge kwa kugeuka ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Akizungumza bungeni jana katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa mwaka 2014/15, Lissu alisema kuwa atawasilisha hoja binafsi katika Ofisi ya Spika ili iundwe tume kwa ajili ya kuwachunguza wabunge na mawaziri hao.

Huku akionyesha baadhi ya nyaraka ambazo wabunge hao wameiandikia mifuko hiyo ya jamii kuomba fedha, Lissu alisema kitendo hicho kimewafanya viongozi hao kusifia kila jambo linalofanywa na mifuko hiyo, hata kama ni baya.

Lissu alitoa kauli hiyo huku wabunge watano kati ya wanane waliomtangulia kuchangia mjadala huo, kuisifia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, huku wakimtaja kwa jina Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau kwamba ni mfano wa kuigwa.

“Sifa hizi zina sababu yake. Kuna nyaraka na barua zinazoonyesha wabunge mbalimbali waliochukua fedha za mifuko hii kwa sababu mbalimbali,” alisema Lissu na kuongeza;

“Naomba baadaye Bunge liunde kamati teule ili kuichunguza mifuko hii na viongozi hawa.”

Hata hivyo, Lissu hakumalizia hoja yake hiyo baada ya muda wake wa kuchangia kumalizika na kutakiwa kukaa chini na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu.

Wahusika

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha Bunge, Lissu alilionyesha gazeti hili nyaraka za vigogo hao zikionyesha wote wameomba kati ya Sh500,000 hadi Sh10 milioni.

Kati yao wapo mawaziri, naibu mawaziri ambao wameomba fedha hizo kwa ajili ya matumizi mbalimbali, huku baadhi yao wakieleza kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao, ikiwa pamoja na kununua jezi na mipira.

Sakata hilo pia linaihusisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo kigogo mmoja wa wizara hiyo (jina tunalo) ameomba mfuko mmoja wa jamii kumnunulia vifaa vya ofisi ikiwamo kompyuta kwa ajili ya matumizi ya wizara.

“Unaweza ukajiuliza maswali mengi. Wizara inaomba fedha katika mfuko wa jamii ili kununua kompyuta na vifaa vingine vya ofisi wakati ina bajeti ya ununuaji wa vifaa hivyo.

Ni wazi kuwa mhusika alikuwa akipeleka vifaa hivyo nyumbani kwake,” alisema Lissu.

Alisema atawasilisha hoja yake ili kuomba Spika aunde tume kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Awali, Lissu wakati akichangia mjadala huo alisema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa miaka mitatu mfululizo ripoti yake inailalamikia mifuko ya hifadhi ya jamii kutumia fedha kuwekeza katika miradi isiyo na tija kwa mifuko yenyewe na pia wafanyakazi.

“CAG anaeleza katika ripoti zake kwamba Sh661 bilioni, ambazo mifuko ya jamii imewekeza katika miradi mbalimbali mpaka sasa hazijalipika. Fedha hizi zilitakiwa kuwekezwa katika miradi harafu zirudishwe kwa riba na CAG anasema fedha hizo hazilipiki” alisema Lissu.

Alisema kuwa taarifa ya CAG mwaka 2013/14 inaonyesha kuwa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali (PSPF) una nakisi ya uwezo wa kulipa wanachama wao ya Sh6.4trilioni, kwamba fedha hizo ni za wafanyakazi na zimewekezwa katika mambo mbalimbali.

UPDATE:

TUNDU LISU AWATAJA KWA MAJINA.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewataja kwa majina mawaziri na wabunge aliosema bungeni kuwa wamekuwa ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi; Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana na wabunge Betty Machangu (Viti Maalumu), Livingstone Lusinde (Mtera), John Komba (Mbinga Magharibi), Eugen Mwaiposa (Ukonga) na Gudluck Ole Medeye (Arumeru Magharibi).

Hata hivyo, gazeti hili halijawataja majina mawaziri na wabunge wengine waliomo kwenye orodha hiyo ya Lissu kwa kuwa hawakupatikana jana kujibu tuhuma hizo.

Mbali na kuwataja kwa majina, Lissu pia ametoa vielelezo vinavyoonyesha jinsi walivyokuwa wakiidhinishiwa malipo kwa nyakati tofauti na Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), kwa sababu mbalimbali.

Lissu alimwambia mwandishi wetu jana kuwa licha ya kiwango cha fedha kutokuwa kikubwa, lakini kinaweza kusababisha mgongano wa kimasilahi kati ya wajibu wa wabunge kwa umma na masilahi yao binafsi.

“Hali hii inaweza kusababisha Bunge likashindwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuisimamia Serikali na taasisi zake,” alisema Lissu huku akisisitiza azimio lake la kuwasilisha hoja binafsi kwa Spika wa Bunge ili iundwe tume kuchunguza suala hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga jana alikiri kuwa shirika hilo liliidhinisha malipo kwa mawaziri na wabunge hao kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, alisema shirika hilo halitoi fedha taslimu, bali hununua vitu ambavyo viliombwa na viongozi hao kwa ajili ya kusaidia wananchi na si kufanya biashara.

Sakata lenyewe

Akizungumzia jinsi mawaziri na wabunge hao walivyosaidiwa, Lissu alisema LAPF ilitoa Sh2.5 milioni kwa ajili ya mradi wa madarasa Jimbo la Kongwa linaloongozwa na Ndugai.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Ndugai alisema hakuna tatizo lolote kwa mbunge kupewa msaada na mfuko wa kijamii.

“Huyo Lissu ana upungufu mkubwa. Hivi LAPF ikisaidia Sh2 milioni kwa ujenzi wa darasa unaogharimu Sh10 milioni ni tatizo hilo? Nchi hii inakwenda wapi jamani, siyo kila kitu wanachozungumza wapinzani ni hoja, kama LAPF wangekuwa wanatoa

Ndugai alisema hiyo ni mara ya kwanza Jimbo la Kongwa kupatiwa msaada na shirika hilo huku akihoji juu ya Lissu katika jambo hilo ambalo alisema ni la kawaida mno.

Pia Lissu alisema LAPF ilitoa Sh1.6 milioni kwa ajili ya kuisaidia Shule ya Isimani iliyopo katika jimbo la Waziri Lukuvi.

Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo, Waziri Lukuvi alisema asingeweza kuzungumza lolote kwa sababu alikuwa akiuguza huko Iringa. Shirika hilo liliidhinisha Sh1.5milioni kwa ajili ya mradi wa maabara wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Lissu alisema Waziri Kairuki aliidhinishiwa fedha kwa ajili ya ununuzi wa kompyuta mpakato (Laptop) mbili kwa ajili ya vyama vya wafanyakazi. Akizungumzia tuhuma hizo Kairuki alisema: “Sina la kusema katika hilo pengine ungewauliza LAPF watakuwa na ufafanuzi zaidi kuhusu fedha wanazozitoa kwa ajili ya kusaidia masuala mbalimbali.”

Lissu pia alisema LAPF iliidhinisha Sh2.5milioni kwa Waziri Chana ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kwa ajili ya taasisi ya Iringa Constituency Development Account.

Kuhusu madai hayo Chana alisema: “Mifuko ya kijamii ina idara za kusaidia jamii. Mtu yeyote anaweza kuomba msaada katika mifuko hii na akasaidiwa.”

Alisema hakuna sheria zinazombana mbunge kuomba msaada kwa ajili ya kusaidia wananchi wa jimbo lake na kusisitiza kuwa hata Rais huwa anaomba msaada.

“Sijui huyo Lissu anasaidiaje wananchi wake jimboni. Kuna mifuko ya kusaidia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi. Sijaelewa dhambi iko wapi katika hili. Benki ya NMB hivi karibuni ilitoa msaada wa mashuka Wilaya ya Ludewa, sioni tatizo,” alisema.

Kuhusu Mbunge wa Ukonga, Lissu alisema Aprili 5 mwaka jana, LAPF iliidhinisha malipo ya Sh500,000 kwa ajili ya taasisi ya Ukonga Constituency Development Trust Fund inayoongozwa na Mwaiposa.

“Hiyo Saccos ipo mpaka leo na kuomba siyo kosa. Sisi kama wabunge tuna dhamana ya kushirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo. Si dhambi kuomba fedha za ujenzi wa madarasa,” alisema Mwaiposa.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema alisema Februari 2013, uongozi wa LAPF uliidhinisha Sh2.8 milioni kwa Machangu kwa ajili ya taasisi inayoitwa Iyana Education Trust.

Hata hivyo, Machangu alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema: “Ni muongo kabisa (Lissu) yeye inamhusu nini hiyo?”
hawakupatikana jana kujibu tuhuma hizo.

Lissu alisema nyaraka alizonazo zinaonyesha kuwa Agosti, 2013 LAPF iliidhinisha fedha za kununulia pikipiki mbili kwa ajili ya vituo vya afya vya Jimbo la Mtera linaloongozwa na Lusinde.

Kama ilivyokuwa kwa Mwaiposa, Lusinde naye alisema kuomba si kosa na kwamba amekuwa akiomba misaada sehemu mbalimbali kwa ajili ya kulisaidia jimbo lake.

“Fedha hizo tumeshapata na pia tuliomba nyingine katika Kiwanda cha Saruji cha Wazo bado hatujapata,” alisema Lusinde na kusisitiza kuwa mbunge hawezi kuona mambo hayaendi katika jimbo lake kisha akakaa kimya.

Lissu pia alisema LAPF ililipa Sh1.5 milioni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa ajili ya Mfuko wa Nyasa Foundation uliopo katika eneo la jimbo linaloongozwa na Komba ambaye pia ni mlezi wa mfuko huo.

Komba alifafanua kuhusu fedha hizo na kusema: “Zilikuwa za Harambee na tuliomba sehemu nyingi lakini mimi siyo niliyeomba. Wao ndiyo waliomba na hata hundi walichukua wao.”

Lissu pia alisema LAPF iliidhinisha Sh1.5 milioni kwa ajili ya mradi wa maabara wa Jimbo la Arumeru Magharibi la Medeye madai ambayo mbunge huyo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema ili ayajibu anataka mwandishi awe pamoja na Lissu na wakae wote watatu kwa pamoja.
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,660
2,000
Unawezaje waziri au mbunge kuomba shillingi 500,000/- kwenye mfuko wa hifadhi? Idadi hii anaweza kukupa mtu binafisfi kutoka mfukoni mwake. Huu unaonyesha umasikini mkubwa wa mawazo.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.
 

kuku87

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
1,221
1,500
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.

Majina tu mkuu mwnyw yuko na majina mwaka wa 4 sasa hajayafanyia chochote sasa Mh. Lisu akitoa majina yatafanyiwa nn?
 

bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.

wewe ni kipofu wa akili,vijana wapuuzi kama wewe ni janga la taifa!
 

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,820
1,195
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.

Wewe ni kidudumtu kweli! Aliyegoma kutoa majina ni lisu au ni gazeti.
 

bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Hujui kuwa joyce banda katokea chama cha upinzani halafu kagongwa kama nini kura zake hata mamia hazikufika ndiyo yatakayowakuta ukawa.

kwa hiyo aliyeshinda ametokea chama tawala au? Tukisema nyie ni misukule hamtuelewi,chama tawala ni kile kilichopo madarakani kwa wakati huo! Kwa upumbafu wako unadhani ccm ikiondoka madarakani itaendelea kuitwa chama tawala? Shirikisha ubongo wako!
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.
Kwani majina ndio nini,mangapi yametajwa wamefanywa nini so far!!!!!
Hela zinatoka BoT na.majina yapo nini kimefanyika???!!!
Ya majangili? ??!! Cartels ngapi zipo na zinapeta tu!!!!

Ni akili ya kizamani sana kufanya siasa kwa majina kama hao wanaotumia jina la Nyerere na mama Nyerere!!!!!
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Unawezaje waziri au mbunge kuomba shillingi 500,000/- kwenye mfumo wa hifadhi? Idadi hii anaweza kukua mtu ninafikiri kutoka mfukoni mwake. Huu unaonyesha masikioni mkubwa wa mawazo.

Hawa viongozi waliokulia mfumo fisadi wa MaCCM lolote linaweza kutokea. Mtu anayetuma V8 ya ofisi iende kumpeleka mkewe sokoni na watoto shuleni wakati ana magari binafsi zaidi ya mawili hapo nyumbani kwake, anaweza kuomba hata laki moja akipata fursa. Hii mi viongozi ya CCM ni hatarishi
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Naiona siku CCM ikidondoka kifo cha jambazi sugu, naiona nchi ikisimama tena kwa miguu yake na kuyumba kwa maria kunaisha, naiona hiyo siku ambapo uchumi wa TZ utawakuwa kwa waTZ wote na sio genge la wezi
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom