Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Majuzi nilileta uzi humu kwamba kuna pesa nimezipata kwenye ATM nilipokwenda kufanya muamala usiku. Pesa hizo ziliachwa na mtu ambaye naamini alikua amezidiwa na kilevi

Nilipata ushauri mwingi wa aina tofauti kuhusiana na ama kuzitumia au kumrejeshea pesa hizo muhusika ambaye kwakweli simjui hadi muda huu. Nimeuthamini sana sana ushauri wote niliopewa na wadau humu jukwaani na hata PM, na naomba Mola Awabariki wote waliotoa maoni kwani naamini walikua na nia njema hata wale walioniponda kwamba eti hii ni chai

Jana Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha
Nilipongezwa na kushukuriwa kwa hatua niliyochukua na kwamba imenijengea imani. RM wangu akanambia yapo matukio machache ya namna hiyo yanatokea na mara zote watu huwa wanasepa na pesa lakini huishia kujulikana na kuaibika maana camera na technolojia zingine zikitumika itajulikana tu. Akasema kuna Mbunge tena alishawahi kua Waziri miaka ya nyuma aliumbuka baada ya kuondoka kwenye ATM na pesa zisizokua zake!!!

Bado sijapigiwa simu wala kwenye simu yangu hakujaingia ujumbe wowote wa kuonyesha kufanyika kwa muamala wowote lakini nahisi nimeutua mzigo flani uliokua unanipa wasiwasi na shauku ambayo siwezi kuilezea

Mkuu uliyesahau pesa zako ATM tuwasiliane uweze kuzichukua - JamiiForums
Sesten umefanya jambo jema.Mungu akubariki.
 
Ndugu MTU asikudanganye hela ya MTU MPE mhusika. Hii itakuletea amani ya kutosha kuliko kutumia hio pesa.

Wakati Fulani bank ya NBC walinizidishia 500,000. Niliwapigia simu bila kutaja kiasi, kesho yake wakanitafuta na nikawapa hio hela. Ingawa niliona afisa mhusika hakusema hata neno la ahsante.

Mungu akubariki. Umaskini wetu usiwe sababu ya kula usichopanda.
 
Mungu Azidi kukupa moyo huohuo mkuu
 
We sio msamalia mwema bali ni mshamba tu, unarudishaje hela ya mlevi? mimi ningeenda kutoa kwa watu wenye mahitaji maalumu kama yatima, wenye ulemavu n.k, Huyo mlevi hata hajui kama siku hiyo alienda ATM. Ye anachojua pesa aliyokua nayo alihonga yote.
Kama ungezipata wew hzo Pesa nadhani hata hao watu wenye mahitaji maalumu wasingepata.
 
We sio msamalia mwema bali ni mshamba tu, unarudishaje hela ya mlevi? mimi ningeenda kutoa kwa watu wenye mahitaji maalumu kama yatima, wenye ulemavu n.k, Huyo mlevi hata hajui kama siku hiyo alienda ATM. Ye anachojua pesa aliyokua nayo alihonga yote.
Mkuu wewe ndo mshamba kwanini unahukumu mapema?? Una uhakika gani jamaa ni mlevi?? Je kama amekunywa sababu ya stress za maisha mkuu usipende kutoa hukumu moja kwa moja
 
Muda mwingine ushamba unasaidia, mimi ni mfanyakazi wa benki, kwa security iliyopo sehemu za bank na kwenye ATM huwezi fanya kitu usijulikane nn labda wahusika waamue kupuuzia tuu. Kuna jamaa alishawai kukuta simu kwenye kaunta ya bank teller baada ya mteja wa awali kuisahau, yule jamaa akaichikichia. Baada ya muda yule jamaa akarudi na madai ya kuwa kasahau simu yake, watu wa security wakarudi kwenye cctv camera, wakamuona jamaa wakarudi muda wa transaction wakapata detail zake, jamaa kupigiwa simu akakataa kuwa hajachukua simu, meneja wa bank akaamua kumpigia mwajiri wa jamaa maana wakati anafungua akaunti alitumia barua ya mwajiri. Mwajiri akaomba ushahidi wa video akaamua kumfukuza kazi jamaa kwa kutokuwa mwaminifu na kwa kuchafua jina la kampuni.
 
Back
Top Bottom