Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Majuzi nilileta uzi humu kwamba kuna pesa nimezipata kwenye ATM nilipokwenda kufanya muamala usiku. Pesa hizo ziliachwa na mtu ambaye naamini alikua amezidiwa na kilevi

Nilipata ushauri mwingi wa aina tofauti kuhusiana na ama kuzitumia au kumrejeshea pesa hizo muhusika ambaye kwakweli simjui hadi muda huu. Nimeuthamini sana sana ushauri wote niliopewa na wadau humu jukwaani na hata PM, na naomba Mola Awabariki wote waliotoa maoni kwani naamini walikua na nia njema hata wale walioniponda kwamba eti hii ni chai

Jana Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha
Nilipongezwa na kushukuriwa kwa hatua niliyochukua na kwamba imenijengea imani. RM wangu akanambia yapo matukio machache ya namna hiyo yanatokea na mara zote watu huwa wanasepa na pesa lakini huishia kujulikana na kuaibika maana camera na technolojia zingine zikitumika itajulikana tu. Akasema kuna Mbunge tena alishawahi kua Waziri miaka ya nyuma aliumbuka baada ya kuondoka kwenye ATM na pesa zisizokua zake!!!

Bado sijapigiwa simu wala kwenye simu yangu hakujaingia ujumbe wowote wa kuonyesha kufanyika kwa muamala wowote lakini nahisi nimeutua mzigo flani uliokua unanipa wasiwasi na shauku ambayo siwezi kuilezea

Mkuu uliyesahau pesa zako ATM tuwasiliane uweze kuzichukua - JamiiForums
Mkuu, pongezi kubwa kwako, na mola akuongoze wewe na kizazi chako.
 
Ushamba saa zingine unaokoa ndugu yangu, hata kama ningetumia hizo pesa ingejulikana wangekata kwenye akaunti yangu kiulaiiini kabisa mkuu
Wengine huna sababu ya kuwajibu, waache tu waongee. Binafsi bado napendekeza tena, kama kuna watu hua wanakua black listed kwa makosa yao, tuanzishe pia kitengo cha ku white list watu kwa mema yao" You need to be white listed
 
Hongera kwa uaminifu mpo wachache, niwe mkweli ningezitumia tu
😀😀😀😀

Asante Simara lakini pengine Mungu Angekuongoza na weye ukazirudisha huwezi jua, ngoja ikutokee siku moja mtu asahau halafu uziokote wewe
 
Mkuu wazo langu ni kuwa km una lengo la kumsaidia kwa nn usien branch ulotoa hela uwape muda ulionda bank,bila shaka transaction yake ilitangulia yako si watamjua mwenye a/c hiyo?
 
Mkuu wazo langu ni kuwa km una lengo la kumsaidia kwa nn usien branch ulotoa hela uwape muda ulionda bank,bila shaka transaction yake ilitangulia yako si watamjua mwenye a/c hiyo?
Mkuu nimeelimishwa kuhusu hili

Ni kwamba ipo kama mtu aliyekosea kutuma hela kwenye simu akatuma kimakosa kwenda kwenye namba ambayo hakuikusudia

Aliyepokea ni vizuri akaicha kwenye simu yake hata kama atapigiwa simu na aliye mtumia ili kazi ya kuurejesha muamala huo uwe ni wa mtandao husika baada ya kua kumekuja malalamiko/maombi rasmi ya kurudishiwa pesa hizo kwa aliyetuma

Ndio maana kama utakua umesoma post yangu hii ya mrejesho nimeambiwa pesa niiweke kwenye a/c yangu na uchunguzi ukikamilika kama watamjua mwenye pesa zake basi wata debit a/c yangu wazipeleke kwa muhusika
 
Back
Top Bottom