Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Dah! Mkuu umekosea sana kucoment mada hii.

Hata kama wewe ni mwizi kamili, hauwezi paza sauti kulaani muungwana mwenye utu wake aliyerejesha pesa za kuokota ambazo hakuzipata kwa jasho lake.

Ogopa sana kufungwa na dhamira, hasa kama wewe umekua katika malezi na maadili mema.

Tabia ya mtu haihukumiwi na binadamu, kwa kuwa sote tu wadhaifu.

Kusema huyo mlevi ama mzinzi nk nk, hiyo tayari ni hukumu na mwenye kuhukumu ni Mwenyezi Mungu pekee.

Je wewe binadamu waweza kumhukumu binadamu mwenziyo kwa madhaifu yaleyale utendayo wewe?

Ama labda nikuulize, mlevi hana haki?

Unawezaje kutoa sadaka kwa pesa ya wizi?

Inapendeza sana jambo la kheri lijadiliwe kwa kheri, siyo jambo la kheri lijadiliwe kijambazi ama kihalifu.

Nimesikitishwa sana na comment yako hiyo.
We sio msamalia mwema bali ni mshamba tu, unarudishaje hela ya mlevi? mimi ningeenda kutoa kwa watu wenye mahitaji maalumu kama yatima, wenye ulemavu n.k, Huyo mlevi hata hajui kama siku hiyo alienda ATM. Ye anachojua pesa aliyokua nayo alihonga yote.
 
Mimi niliwahi kuokota pesa ndani ya bank. Sio nyingi zilikuwa shs 13000. Nikaweka mfuko wa shati. Na niliweka uzi hapa jf. Ilikuwa hivi.

Mchana wa siku hiyo niliingia kwenye moja ya matawi ya bank ya CRDB kwa ajili ya kuwithdraw pesa kwa ajili ya malipo ya biashara nayofanya. Nilipooingia tu ndani nikaona note tatu zipo chini moja ya 10000 maja ya 2000 na 1 ya 1000. Kulikuwa na wateja kama 20-30 hivi. Kuna waliokuwa wamekaa na wengine wamesimama.Na zile pesa zilikuwa wazi kabisa kila mtu anaziona.

Nikainama nikaziokota na kuziweka kwenye mfuko wa shati kila mtu akiniona. nikaenda kuandika slip. Nikapanga foleni nikatoa mzigo na kuondoka zangu. Ila kule ndani kukaibuka mjadala. Wengine wakiamini kuwa nilikuwa sahihi na wengine wakiona nilipaswa kuzikabidhi kwa mtoa huduma pale mapokezi. Nilikuja kugundua kuwa wengi waliziona ila waliogopa kuchukua. Nikasepa zangu.
 
na Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha

Hayo maneno ya kitaalamu waliyotumia yanaweza kuwa namna ya kukuchanganya mwisho wa siku wanazichomoa kijanja
 
Pesa zikitoka kwenye a/c yangu nitapata notification ya simu na e mail so nitajua na nitafatilia kupata uhakika kama zimekwenda kweli kwa mwenyewe
 
Mimi niliwahi kuokota pesa ndani ya bank. Sio nyingi zilikuwa shs 13000. Nikaweka mfuko wa shati. Na niliweka uzi hapa jf. Ilikuwa hivi.

Mchana wa siku hiyo niliingia kwenye moja ya matawi ya bank ya CRDB kwa ajili ya kuwithdraw pesa kwa ajili ya malipo ya biashara nayofanya. Nilipooingia tu ndani nikaona note tatu zipo chini moja ya 10000 maja ya 2000 na 1 ya 1000. Kulikuwa na wateja kama 20-30 hivi. Kuna waliokuwa wamekaa na wengine wamesimama.Na zile pesa zilikuwa wazi kabisa kila mtu anaziona.

Nikainama nikaziokota na kuziweka kwenye mfuko wa shati kila mtu akiniona. nikaenda kuandika slip. Nikapanga foleni nikatoa mzigo na kuondoka zangu. Ila kule ndani kukaibuka mjadala. Wengine wakiamini kuwa nilikuwa sahihi na wengine wakiona nilipaswa kuzikabidhi kwa mtoa huduma pale mapokezi. Nilikuja kugundua kuwa wengi waliziona ila waliogopa kuchukua. Nikasepa zangu.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119]Wee noma sanaa
 
Pesa zikitoka kwenye a/c yangu nitapata notification ya simu na e mail so nitajua na nitafatilia kupata uhakika kama zimekwenda kweli kwa mwenyewe
Utakuwa na Uhakika gani kwamba ndo mwenyewee???? Yanii wewe zile helaa ungezichukuaa tuu mbele kwa mbele..maana hiyo bank ulopelekaa nao watafanya janja janjaa tuuu...Watamzungusha huyo jamaa na wewe piaa kwa kuwa hamfaahamianaa... Wewe watakwambia wamempa...Yeye watamwambia kiswahili kinginee Kazi imeishaaaa...[emoji16][emoji16][emoji16]Mjini shulee mzeee
 
Mimi niliwahi kuokota pesa ndani ya bank. Sio nyingi zilikuwa shs 13000. Nikaweka mfuko wa shati. Na niliweka uzi hapa jf. Ilikuwa hivi.

Mchana wa siku hiyo niliingia kwenye moja ya matawi ya bank ya CRDB kwa ajili ya kuwithdraw pesa kwa ajili ya malipo ya biashara nayofanya. Nilipooingia tu ndani nikaona note tatu zipo chini moja ya 10000 maja ya 2000 na 1 ya 1000. Kulikuwa na wateja kama 20-30 hivi. Kuna waliokuwa wamekaa na wengine wamesimama.Na zile pesa zilikuwa wazi kabisa kila mtu anaziona.

Nikainama nikaziokota na kuziweka kwenye mfuko wa shati kila mtu akiniona. nikaenda kuandika slip. Nikapanga foleni nikatoa mzigo na kuondoka zangu. Ila kule ndani kukaibuka mjadala. Wengine wakiamini kuwa nilikuwa sahihi na wengine wakiona nilipaswa kuzikabidhi kwa mtoa huduma pale mapokezi. Nilikuja kugundua kuwa wengi waliziona ila waliogopa kuchukua. Nikasepa zangu.
Hahahaaaaaa,dah wee kiboko aisee
 
Utakuwa na Uhakika gani kwamba ndo mwenyewee???? Yanii wewe zile helaa ungezichukuaa tuu mbele kwa mbele..maana hiyo bank ulopelekaa nao watafanya janja janjaa tuuu...Watamzungusha huyo jamaa na wewe piaa kwa kuwa hamfaahamianaa... Wewe watakwambia wamempa...Yeye watamwambia kiswahili kinginee Kazi imeishaaaa...[emoji16][emoji16][emoji16]Mjini shulee mzeee
Hahahaaa itakua ni sambi sao wenyewe sasa hapo mkuu😀😀😀
 
Hajar mie niseme tu uendelee na moyo wako huo huo Sesten maana vyuma hivi pasi kuwa na roho hiyo haraka haraka yangekuja maamuzi ya kuenda kuitumia tu japo baadae kama angekuja kulalamika ndio madhara ungeyaona.

Allah akubariki mnoo.
 
We sio msamalia mwema bali ni mshamba tu, unarudishaje hela ya mlevi? mimi ningeenda kutoa kwa watu wenye mahitaji maalumu kama yatima, wenye ulemavu n.k, Huyo mlevi hata hajui kama siku hiyo alienda ATM. Ye anachojua pesa aliyokua nayo alihonga yote.
ukila kisicho chako wewe ni mwizi tu sawa na wezi wengine.
 
Majuzi nilileta uzi humu kwamba kuna pesa nimezipata kwenye ATM nilipokwenda kufanya muamala usiku. Pesa hizo ziliachwa na mtu ambaye naamini alikua amezidiwa na kilevi

Nilipata ushauri mwingi wa aina tofauti kuhusiana na ama kuzitumia au kumrejeshea pesa hizo muhusika ambaye kwakweli simjui hadi muda huu. Nimeuthamini sana sana ushauri wote niliopewa na wadau humu jukwaani na hata PM, na naomba Mola Awabariki wote waliotoa maoni kwani naamini walikua na nia njema hata wale walioniponda kwamba eti hii ni chai

Jana Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha
Nilipongezwa na kushukuriwa kwa hatua niliyochukua na kwamba imenijengea imani. RM wangu akanambia yapo matukio machache ya namna hiyo yanatokea na mara zote watu huwa wanasepa na pesa lakini huishia kujulikana na kuaibika maana camera na technolojia zingine zikitumika itajulikana tu. Akasema kuna Mbunge tena alishawahi kua Waziri miaka ya nyuma aliumbuka baada ya kuondoka kwenye ATM na pesa zisizokua zake!!!

Bado sijapigiwa simu wala kwenye simu yangu hakujaingia ujumbe wowote wa kuonyesha kufanyika kwa muamala wowote lakini nahisi nimeutua mzigo flani uliokua unanipa wasiwasi na shauku ambayo siwezi kuilezea

Mkuu uliyesahau pesa zako ATM tuwasiliane uweze kuzichukua - JamiiForums
Hongera mkuu
 
Hajar mie niseme tu uendelee na moyo wako huo huo Sesten maana vyuma hivi pasi kuwa na roho hiyo haraka haraka yangekuja maamuzi ya kuenda kuitumia tu japo baadae kama angekuja kulalamika ndio madhara ungeyaona.

Allah akubariki mnoo.
Aamin Hajar , unajua shida zetu haziishi kwa kutumia haki na jasho la mtu mwingine zaidi ya kujitia mikosi tu

Unaweza kudhani kwamba hiyo ni rizki imekuja yenyewe(Wengine wanasema imeletwa na Mungu) lakini mimi nafikiria vinginevyo, niliona huo ni mtihani Mola wangu kanipa

Japo jamaa alikua kalewa lakini hiyo ni haki yake na haihalalishi mtu mwingine kuichukua bila ridhaa yake

Na pia hata watu wa bank mwishoe watakuja kujua tu na watakukata hela zako mwenyewe kwenye a/c yako ubaki unashangaa tu
 
Back
Top Bottom