Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Mrejesho wa Pesa nilizozipata kwenye ATM

Naomba nitofautiane na wewe hapo mkuu. Bank washindwe kukakata pesa ambazo zimekua wrong posted kwenye account yako? Tena na wao wenye ndio wame miss post!!!? Hakuna bank ya namna hiyo
Mkuu hapo pesa haijawa wrong posted kwako. Ni kwamba umeokota pesa wala hujaiba.

Lakini kwa watu wa maadili na utu ni vema kumrudishia alie
poteza kama unaweza kumpata.

Hapo sasa mwambie RM wako au bank manager kwamba utampa pesa mtu aliepoteza kama utaoneshwa ushahidi wa CCTV camera na ushahidi mwingine kama statement na uzuri sura na gari yake umeiona na nguo alizovaa uliziona.

Vinginevyo wagomee kutoa pesa na waambie usikatwe kwenye account. Akipatikana mwenyewe wakukutanishe umpe mkononi maana pesa haikuhamishwa kwake na kuingia kwako toka kwenye accound direct.
 
Ukichukua cha MTU nawe chako kitachukuliwa,Mimi hata Konda akinisahau kuomba nauli nikishuka nampa nauli yake,nimezidishiwa sana chenji na makonda nawarudishia,kwann nichukue kisicho halali yangu.Hata ingekuwa Milioni 10 kwenye ATM ningerudisha,maisha ni zaidi ya pesa, Pesa haina thamani kihivo kama watu waitukuzavyo.
Unaijua thamani ya utu na heshima yako mkuu
 
Hapo safi mkuu,kwa kuwa huyo jamaa atarudi kwenye bank yake na kufungua madai ,then makamera ya ATM aliyotoa yatacheki muda na picha ya mtu aliyechukua pesa na wewe utaonekana ukizichukua.
 
Hahahaaa labda!

Mimi pesa nimeambiwa niziweke kwenye account yangu mwenyewe kwa hiyo kama kuzikata watazichukua wenyewe kutokea hapo

Nadhani wakishafanya uchunguzi na wakigundua kwa uhakika kua mwenyewe ni nani
Watakula tu hao watu wa bank.
Wewe rudi waambie naomba nikambidhi mwenyewe mkononi nijiridhishe imerudi kwake.

Wewe si unamkumbuka huyo jamaa?
 
Hapo safi mkuu,kwa kuwa huyo jamaa atarudi kwenye bank yake na kufungua madai ,then makamera ya ATM aliyotoa yatacheki muda na picha ya mtu aliyechukua pesa na wewe utaonekana ukizichukua.
Kuna uwezekano mkubwa hatakumbuka amepoteza pesa wapi.

Kama akihisi imekatwa na bank kimakosa ataenda kulalamika atampata.
 
Watakula tu hao watu wa bank.
Wewe rudi waambie naomba nikambidhi mwenyewe mkononi nijiridhishe imerudi kwake.

Wewe si unamkumbuka huyo jamaa?
Kumkumbuka kwa sura yes sasa nampataje? Labada siku watakapozikata kwenye acc yangu niwaambie wamlete nimuone au wanipenamba yake
 
Hapo safi mkuu,kwa kuwa huyo jamaa atarudi kwenye bank yake na kufungua madai ,then makamera ya ATM aliyotoa yatacheki muda na picha ya mtu aliyechukua pesa na wewe utaonekana ukizichukua.
Ni kweli kabisa mkuu
 
Mkuu hapo pesa haijawa wrong posted kwako. Ni kwamba umeokota pesa wala hujaiba.

Lakini kwa watu wa maadili na utu ni vema kumrudishia alie
poteza kama unaweza kumpata.

Hapo sasa mwambie RM wako au bank manager kwamba utampa pesa mtu aliepoteza kama utaoneshwa ushahidi wa CCTV camera na ushahidi mwingine kama statement na uzuri sura na gari yake umeiona na nguo alizovaa uliziona.

Vinginevyo wagomee kutoa pesa na waambie usikatwe kwenye account. Akipatikana mwenyewe wakukutanishe umpe mkononi maana pesa haikuhamishwa kwake na kuingia kwako toka kwenye accound direct.
Ni ushauri mzuri sana mkuu, nitaongea tena na RM
 
Uaminifu ni mtaji. Umejiweka huru mbele za Mungu na hata mbele ya wanadamu walio wema. Mungu akubariki sana
 
Majuzi nilileta uzi humu kwamba kuna pesa nimezipata kwenye ATM nilipokwenda kufanya muamala usiku. Pesa hizo ziliachwa na mtu ambaye naamini alikua amezidiwa na kilevi

Nilipata ushauri mwingi wa aina tofauti kuhusiana na ama kuzitumia au kumrejeshea pesa hizo muhusika ambaye kwakweli simjui hadi muda huu. Nimeuthamini sana sana ushauri wote niliopewa na wadau humu jukwaani na hata PM, na naomba Mola Awabariki wote waliotoa maoni kwani naamini walikua na nia njema hata wale walioniponda kwamba eti hii ni chai

Jana Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha
Nilipongezwa na kushukuriwa kwa hatua niliyochukua na kwamba imenijengea imani. RM wangu akanambia yapo matukio machache ya namna hiyo yanatokea na mara zote watu huwa wanasepa na pesa lakini huishia kujulikana na kuaibika maana camera na technolojia zingine zikitumika itajulikana tu. Akasema kuna Mbunge tena alishawahi kua Waziri miaka ya nyuma aliumbuka baada ya kuondoka kwenye ATM na pesa zisizokua zake!!!

Bado sijapigiwa simu wala kwenye simu yangu hakujaingia ujumbe wowote wa kuonyesha kufanyika kwa muamala wowote lakini nahisi nimeutua mzigo flani uliokua unanipa wasiwasi na shauku ambayo siwezi kuilezea

Mkuu uliyesahau pesa zako ATM tuwasiliane uweze kuzichukua - JamiiForums
Hao bank mbona wanatumia njia ndefu sana....wakishajua tarehe na muda transaction ilifanyika ya hiyo laki nne ni rahisi kwao kumjua mwenye account...wampigie simu maana wana namba za wateja wao wamrudishie pesa zake....sio wanaleta politics....mpaka mtu aje kulalamika waache blah blah
 
Nadhani wameendelea kuchunguza na kufatilia mpaka wawe na hakika kuhusu muhusika halisi wa hizo pesa

Mimi nilipomaliza kuzitumbukiza kwenye a/c yangu nikajiondokea zangu
 
Back
Top Bottom