Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,666
- 19,394
Majuzi nilileta uzi humu kwamba kuna pesa nimezipata kwenye ATM nilipokwenda kufanya muamala usiku. Pesa hizo ziliachwa na mtu ambaye naamini alikua amezidiwa na kilevi
Nilipata ushauri mwingi wa aina tofauti kuhusiana na ama kuzitumia au kumrejeshea pesa hizo muhusika ambaye kwakweli simjui hadi muda huu. Nimeuthamini sana sana ushauri wote niliopewa na wadau humu jukwaani na hata PM, na naomba Mola Awabariki wote waliotoa maoni kwani naamini walikua na nia njema hata wale walioniponda kwamba eti hii ni chai
Jana Jumatatu nilikwenda kuonana na Relationship Manager wangu na akaniambia wakati wanashughulikia hilo jambo niziweke hizo pesa kwenye account yangu wao wata zi block/hold na watu wa reconciliation watajua ni za wapi na kama kuna complain yoyote na mwisho wa siku watanijulisha
Nilipongezwa na kushukuriwa kwa hatua niliyochukua na kwamba imenijengea imani. RM wangu akanambia yapo matukio machache ya namna hiyo yanatokea na mara zote watu huwa wanasepa na pesa lakini huishia kujulikana na kuaibika maana camera na technolojia zingine zikitumika itajulikana tu. Akasema kuna Mbunge tena alishawahi kua Waziri miaka ya nyuma aliumbuka baada ya kuondoka kwenye ATM na pesa zisizokua zake!!!
Bado sijapigiwa simu wala kwenye simu yangu hakujaingia ujumbe wowote wa kuonyesha kufanyika kwa muamala wowote lakini nahisi nimeutua mzigo flani uliokua unanipa wasiwasi na shauku ambayo siwezi kuilezea
Mkuu uliyesahau pesa zako ATM tuwasiliane uweze kuzichukua - JamiiForums