sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,989
- 4,168
Mimi hawa washenzi panya kwanza waliniingizia ndani bonge la nyoka, maana nyoka nao wanawafuata panya wawameze, lakini washanitia hasara kwa speaker zangu za Sony, yaani wamefanya nyumba ndani ya speaker badala ya kukaa na kutulia wakakata nyanya na kutafuna speaker ili kupata karatasi za kutandika malalio ya watoto wao.Mimi sinaga noma na panya niliwahi kuishi sehemu mlango ulikuwa na nafasi kubwa chini sasa kulikuwa na panya wawili ikifika jioni wanatoka nje wanakuja ndani mimi nikaona nisihangaike nao maana wanatafuta ulaji.
Sasa walivyo washenzi nikiwa sebuleni natazama tv mara wakatishe halafu wakifika katikat wanasimama wanaanza niangalia mimi nawaacha tu.
Walicho nifanya walikula vyeti vyangu wakaingia kwenye stabilize wakakata nyaya wakakata nyaza za friji wakaacha kula vyakula wakawa wanakula nguo.
Hapo ndipo niliona ubaya wao nikawatafutia dawa nikiweka kwenye vyakula hawali iwe dagaa au samaki hawali nikaja kuwanasa kwa mtego wa gundi kwa hasira niliwapa mateso balaa walikufa kifo kibaya sana