Mrejesho wa panya wasumbufu

Mrejesho wa panya wasumbufu

Pamoja na kupulizia dawa pia hakikisha mlango uwe unarudishia anzia mida ya SAA moja,yaan MTU akitoka nje asiuache mlango wazi na madirisha yawe na nyavu za kuzuia mbu
Mm kwangu tatizo ni mbu jamani yani kila siku lazima nipulize dawa ndani la sivyo silali kbs.

Natafuta dawa nzuri ile ya kupuliza nje kuzunguka nyumba
 
kuna ile ya gundi akikanyaga tu wananasa, hatoki hapo. Unamkuta mzima.
 
Ila mkuu acha tu ujimwae mwae, na kujiona upo huru, panya anasumbua aisehhh, panya anatia hasira jamani acha tu, ndiyi ukute ametafuna suti yako kali tena kwenye eneo la tako
 
Mimi nikafikiri ni wale Panya wanaokula mahindi kule Handeni, nakumbuka nao wameomba msaada.
 
panya walikuwa wananisumbua sana enzi hizo yani unalala kidogo tu unamsikia anaanzisha mizunguko ndani ya nyumba, siku moja wakazidisha vurugu na mimi ikaamka na kubeba mabox yote ndani ya nyumba na kuyapaki nje na kuanza kufungua moja moja huku nikiwashughulikia, niliwauwa wote hadi vitoto toka hapo sijaona usumbufu wa panya ila kwa sasa nina tatizo na mende ndani kwangu yaani hadi wanakera
 
Sijui hao mijusi hasa wale wa wanaopenda kukaa ndani makosa yao siyaoni, ni wapole hawana mashara kwa binaadamu, hawachafui nyumba na wanaua buibui na wadudu wasumbufu isipokuwa MFALME WA WADUDU WASUMBUFU NA WENYE ROHO NGUMU NDUGU KUNGUNI (LANA TULAH)
Kweli mkuu mijusi hawanaga noma na mtu kwanza wao kukaa juu hawaingii hata kwenye misosi wala masufuria. Mimi sinaga time nao na nikiwa nataka kufunga mlango akawa yukl kwenye bawaba nikiona namtisha kwa atoke ndipo nifunge. Mijusi sina noma nao kabisa hawa ndugu zetu
 
Wakuu hamjambo?
Nachukua fursa hii kuwashukuru wakuu wote waliyonisaidia mawazo ya kuwamaliza panya ndani mwangu.
Luna mkuu moja humu alinishauri niwape sumu ambaye ni dawa ya maumivu inayoitwa Indosin. Kwa kweli nimefanikiwa kupata hiyo dawa na wamekufa wote.
Kwa heshima kubwa nawashukuru wote waliyonipa mawazo yaliyosababisha kufanikiwa.
Asanteni sana
Uliitumiaje hiyo dawa ya maumivu
 
Back
Top Bottom