Mrejesho wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika 3 - 4 January 2024

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,693
59,841
Mkutano huu ulihudhuriwa na watu wengi maarufu nchini.

Leo nitaweka mrejesho wa kile kilichozungumzwa, watu waliohudhuria na impact ya mkutano huo katika demokrasia ya hapa nchini.
558c1b5f-de90-4f3c-91f2-24c4d26d7c9a.jpg



Tutaanza kwa kuongelea 4R jinsi zilivyoongelewa na wachangiaji mbalimbali katika mkutano huo.
Bila kupotenza muda nataka niweke viambatishi vinavyoongelea 4R. Maana kuna baadhi yetu hawajui 4R ni nini.
KWA UFUPI
4R ni falsafa ya kuongoza nchi ya kisasa. Ni falsafa inayolenga kujenga taifa tulivu na linalopiga hatua kubwa ya maendeleo ya watu na nchi. Taifa la kisasa linaamini katika kujenga Demokrasia ya kweli.

R1.jpg

R2.jpg

R3.jpg


R4.jpg
 
Video fupi ya kuhusu ufunguzi wa Mkutano huo. Naomba upitie na uweze kusikiliza kwa makini na kisha utaelewa mwelekeo wa mkutano.
 
Hii ni Demokrasia ya kweli watu kukaa pamoja na kuzungumza masuala yanayohusu nchi yao. Falsafa ya 4R itaweza kutufikisha mbali sana.
Hata kwenye familia zetu. Tukiweza kutumia 4R uvunjifu wa ndoa na mapenzi vitapungua.
9a4f37e9-4f7a-4521-99ea-6f4aeff8ce47.jpg
 
Mkutano huu ulihudhuriwa na watu wengi maarufu nchini.
Leo nitaweka mrejesho wa kile kilichozungumzwa, watu waliohudhuria na impact ya mkutano huo katika demokrasia ya hapa nchini.
View attachment 2863303


Tutaanza kwa kuongelea 4R jinsi zilivyoongelewa na wachangiaji mbalimbali katika mkutano huo.
Bila kupotenza muda nataka niweke viambatishi vinavyoongelea 4R. Maana kuna baadhi yetu hawajui 4R ni nini.
KWA UFUPI
4R ni falsafa ya kuongoza nchi ya kisasa. Ni falsafa inayolenga kujenga taifa tulivu na linalopiga hatua kubwa ya maendeleo ya watu na nchi. Taifa la kisasa linaamini katika kujenga Demokrasia ya kweli.

View attachment 2863309
View attachment 2863310
View attachment 2863311

View attachment 2863312
Asante sana Mkuu Venus Star kwa hii kazi mzuri unayoifanya kuhusu mkutano huu. Ubarikiwe sana.
P
 
Siku ya kwanza:
Wachakoza mada walikuwa ni:-

1. Ndugu Doyo Hassani Doyo
2. Mama Gertrude Mongella
3. Salim Mwalimu
4. Steven Wasira
5. Ado Shaibu
 
Salum Mwalimu alisema nini kuhusu 4R?
Kabla sijajibu swala hilo. Nilipojibu hizo asilimia nilijua kuwa ni utendaji kumbe ni kuzijua. Kama kuzijua nazijua kwa 100%.
Kwa maoni yake, Mh raisi aliichukua nchi katika hali ngumu sana. Tulitoka katika uchaguzi ambao ilikuwa katika taharuki kubwa sana.

Anaendelea kuongelea mambo mbalimbali yaliyotokea. Anaendelea kusema raisi aliona lazima mambo yarudi kama kawaida. Ndio maana kukawa na Uhuru wa mikutano ya vyama vya siasa. Vikao vya vyama vya siasa. Kama vitu hivyo vimefanyika nini sasa kifanyike. Ni lazima kuwaunganisha wananchi.

Lazima sasa kuirudisha nchi katika mstari. Anaendelea kuongelea mambo yakipindi kilichopita.
Kaitka hayo yote anaongelea hayo yote yalifanya rais aje na 4R. Kutokana na changamoto tuliyokuwa tunaipitia katika mambo ya kijamii.

Nadhani kwa kiwango gani 4R zinaisaidia au zitaweza kuisaidia tanzania kuenda sambamba na maendeleo ya dira ya dunia na Africa.

Maeneo yote haya mawili Dunia na Afrika inaleka katika maendeleo ya watu. pia maendelo ya nchi.
Kama taifa tunataka kwenda sambamba na dunia na tunataka kwenda sambamba na Africa.
Tunatakiwa kujua Pillars zipi wenzetu wanazitumia. Kama unataka kufika huko na kuna kuwa joto kubwa nchini huwezi kuendelea. Na huna namna uje na 4R ili muweze kuelekewa kwenye reforms.

Jambo la pili, kama mnazungumzia kupata yale dunia inayoyapaya. Ni lazima kuwe na reforms siyo kwenye siasa pekee. Bali kwenye mambo ja kijamii, mifumo na kisiasa.
Ili tuweze kwenye nda huko wezentu na dunia iweze kutupima, lazima kuwe na reforms na kuvumilia kwa hoja.
Ili tuweze kutengeneza nchi yetu tuondokane na joto la ndani lazima tuje na 4R.
 
Ado Shaibu alisema nini kuhusu 4R?
Mimi nyenzo inayoniongoza ni uchambuzi wa mkutadha. Contexture Analysis. Kwenye Hotuba ya Rais ailsema anafungua ukurasa mpya wa Tanzania. Yaani tulipotoka kulikuwa na ukurasa lazima tuufunge. Maeneno mawili yalitakiwa ili tufungue ukurasa upya

1. Kuyumba kwa ustawi wa kitaifa
2. Kuyumba kwa Demokrasia

Lazima tuje kwenye mambo na kujenga msingi wa Taifa. Na katika hizo 4r ndio msingi
Je hizi 4R zinaweza kuwanyenzo kwa kiasi gani Tanzania inaweza kujiweka katika nafasi nzuri kwenye Nyanja za kimataifa?
Mimi ninaungana na wenzangu kwamba falsafa ya 4R lazima itazamwe kwa muktadha mpana zaidi. Kama inaweza ikaijenga nchi yetu kama itatekelezwa kwa ukamilifu katika vipengele hivyo vinne. Na tutaendenda sambamba na dira zadunia.

Mambo ya kuzingatia, ninamuono tofauti ya Wasira ni kweli lazima tuanze kwaajili ya kuridhiana lakini nguzo mama ni reforms.

Lazima hii nguzo mama ya reforms lazima iende sambamba na mabadiliko ya katiba na sehria.
Mchakato wa katiba lazima uanze sasa.
Nguzo ya reforms ni katiba mpya na kuweka msing wa sheria nzuri.
Hatuna kalenda maalum ya kutekeleza mapendekezo yaliyoweka. Ripoti ya kikosi kazi ilitoa maelezo mazuri. Tunahitaji roadmap.

Tunataka reconciliation ya kitaifa. Yako mambo ukiyatazama yalishapata mwafaka wa kitaifa. Mambo hayo yaiswe na majadiliano marefu. Utelekezaji. Mfano ruzuku nk.
 
Doyo Hassani Doyo alisema nini kuhusu 4R
Kaitka uelewa wake wa 100% ameangazia katika uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya siasa. Katika hizo R kutakusamehena, kujenga.
Aliposema 100% ni uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza. Ametoa hotuba 19 march 2023 na ameendelea kuisimamia.

Mimi katika mada iliyowasilishwa naanza kwa ushauri. Nia ya rais isisitizwe katika viongozi wa chini. Ili tunufaike kama nchi. Nchi isiyo na maridhiano hamuwezi kuendelea.

Itakiwa itengenezwe program maalum ili watumishi wa serikali waijue wote. Anaeleza tukio la Police.
Hizi 4R zifundishwe ili watu wazijue ili tuweze kupata wawekezaji.

La pili Rais anania njema sana. Hata alipokuja kuhutubia mkutano uliopita. Amesisitiza kuwa serkali yake inaweza kusikiliza na kuvumilia
 
Mama Gertrude Mongella alisema nini kuhusu 4R?
Rais ameleta misingi ambayo itatusaidia katika wakati huu wa kutengenza dira. Dira ni chombo kitakazo saidia taifa katika miaka 25.
Anaomba ziwekwe katika kiswahili ili tuelewe kwa pamoja. Anaomba lazima tuweke msingi muhimu. Yaani elimu itumike.

Naomba nianzie alipoishia Wasira "Mardhiano" hizi 4R alizozileta Rais. Mwisho wake lazima tubadilishe mtazamo wa mambo. Lazima tubadilike kwa mfano. Siasa zetu zinaendelea kuwa siasa za uana harakati. Ni lazima tutoke kwenye mtazamo huo.

Dunia inabadilika kwa haraka sana. Bila kuwa na falsafa inayotuongoza hatuwezi kwenda pamoja. Zamani tuliachwa nyuma kwa sababu tulikuwa hatujui kusoma na kuandika. Kwa sasa mambo ya teknolojia na kwa sasa Artifial Intelligent. Hizi 4R zinatupeleka katika 5Th industiral revolution.

Kwa mfano msipofanya reconciliation hamna muda wa kutafakari. Na maendeleo ya sasa yanahitaji akili sana. Msipofanya reconciliation hamuwezi kuendelea.
Msipo heshimu mawazo ya mwingine hatuwezi kuendelea. Muda wa kuanza kuhangaika na migonngano.

Hizi 4R kuna mahali tunataka kujenga upya.
 
Steven Wasira alisema nini kuhusu 4R?

anaeleza namna anavyo elewa kuhusu falsafa ya 4R,
Anaeleza namna alivyoelewa kuwa katika historia yetu tumekuwa na siasa za kujenga uhasama. Lakini 4R ni utatuzi wa tatizo hili.

Huu mtazamo wa kuanzisha 4R hauwezi kutazama katika Historia fupi. Haya mambo ya kisiasa yalikuwepo tangu miaka mingi. Siyo katik awamu fulani. Yalikuwa yakibadilika katika kila kipindi kwa sura tofauti.
Rais anaitazama Historia yetu yote. Siyo Awamu fulani,
Katika vyama vya Siasa kumekuwa na msingi ya uhasama. Tumejengewa na waasisi wetu kutokutofautiana kwa ukabila udini nk.

Naamini Maridhiano ndio msingi wa kwanza. Maridhiano ndio msingi wa kwanza. Kama huwezi kuridhiana huwezi kufanya mambo mengine. Alipoapishwa alionesha kuwa yupo serious katika jambo hili. Hata katika mazingira ya uchumi, historia ya nchi yetu ilikuwa na uchumi shirikishi. Hata katika Maono ya Afrika, Na maono ya Taifa unaona kabisa 4R ndizo zinazofanyika.

Kitu cha kwanza ni maridhiano. Nasiyo cham cha chama. Ni maridhiano na jamii. Ili kujenga uchumi.
 
Mkutano huo ulisheheni kila aina ya watu. Kusema kweli, mkutano huo umeleta hamasa kubwa sana katika kujenga Demokrasia ya kweli nchini.
f6f5f9c3-a745-4ede-a51e-b4f4cbd04264.jpg
02615108-ada4-420e-8b7c-f442d7c63b15.jpg
e2097710-448e-4b23-9edf-38c793b4712e.jpg
d636a6e6-4a5f-4b94-95f6-0248352231a5.jpg
 
UFUPISHO KUHUSU 4R
Falsafa ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reform, na Rebuild) inaweza kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni nchini Tanzania.

Reconciliation (Maridhiano):
  • Kisiasa: Kuimarisha maridhiano kunaweza kuleta umoja na kusaidia kupunguza mivutano ya kisiasa. Mchakato wa maridhiano unaweza kujumuisha majadiliano na upatanishi kati ya vyama vya kisiasa na makundi mbalimbali, na hivyo kusukuma mbele ajenda ya kitaifa.

  • Kiuchumi: Maridhiano yanaweza kuleta utulivu wa kisiasa, ambao ni muhimu kwa ukuaji wa kiuchumi. Hali ya utulivu inaweza kuvutia wawekezaji na kusaidia kujenga mazingira bora ya biashara.

  • Kiutamaduni: Maridhiano yanaweza kusaidia kuleta umoja wa kitamaduni na kuheshimu tofauti za tamaduni mbalimbali nchini.
 
Resilience (Ustahimilivu):

  • Kisiasa: Ustahimilivu wa kisiasa unaweza kusaidia kushughulikia changamoto za kisiasa kwa njia inayosaidia kudumisha utulivu. Mfumo imara wa kisiasa unao ustahimilivu unaweza kusimamia mizozo na kuhakikisha utawala wa sheria.

  • Kiuchumi: Ustahimilivu wa kiuchumi unaweza kuwa kinga dhidi ya athari mbaya za mabadiliko ya kiuchumi duniani. Kujenga uchumi imara na wa kustahimili kunaweza kusaidia kuweka mwelekeo thabiti wa maendeleo.

  • Kiutamaduni: Ustahimilivu wa kitamaduni unaweza kuimarisha utambulisho wa kitamaduni na kusaidia jamii kudumisha thamani zao wakati wa mabadiliko.
 
Reform (Marekebisho):

  • Kisiasa: Marekebisho ya kisiasa yanaweza kuboresha utawala wa sheria, kuongeza uwazi, na kukuza uwajibikaji wa kisiasa. Hii inaweza kuleta mabadiliko chanya na kuongeza imani ya wananchi kwa vyombo vya utawala.

  • Kiuchumi: Marekebisho ya kiuchumi yanaweza kujumuisha sera za kifedha zinazounga mkono ukuaji, kuondoa vikwazo vya biashara, na kuongeza ufanisi wa miundo ya kiuchumi.

  • Kiutamaduni: Marekebisho katika sekta ya utamaduni yanaweza kusaidia kulinda na kudumisha urithi wa kitamaduni na kuhakikisha kuwa utamaduni unachangia katika maendeleo ya nchi.
 
Back
Top Bottom