Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Mwaka 2016 mfumo wa maisha ulibadilika baada ya Serikali mpya kuingia madarakani! Vijana wengi tulijikita katika kilimo na ufugaji baada ya motivational speaker kutuhakikishia tutapata utajiri bila kutoa jasho!

Nami nikaanza na nguruwe wenye mimba 3. Mwanzoni hakukuwa na changamoto sana ila shida ilianza walipozaa! Asikwambie mtu kulisha nguruwe ni kipawa toka mbinguni!

Walikuwa wanakula nikanunua gunia 150 za pumba! Walikula mpaka zikaisha kukua hawakui ipasavyo, huku nimeaminishwa nguruwe wa miezi 6 anafikisha kilo 100! Motivational speaker Mungu anawaona!!!!!

Nilikuja kugundua ndani ya miezi 6 nguruwe wana kilo 30-40! Bei ya walanguzi uchwara ni laki hadi laki na nusu! Ukitaka faida uchinje uuze nyama! Ilifikia gunia la pumba 2017 linauzwa elfu 10 na linaliwa siku 1!

Yaani kwa mwezi nguruwe wanakula laki 3! God forbid!!! Nikagundua nimekuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea badala ya nguruwe! Nikaamua kupunguza cost za vyakula kwa kuanza kilimo cha matikiti ili nikiuza yanayobaki madogo madogo nilishie nguruwe!

Hiyo nayo ikawa biashara kichaa, unalima unaivisha vizuri walanguzi wanakuja na bei ya 700- 1000 shambani, unakuwa unarudisha tu mtaji na wakati mwingine mtaji haurudi!!!!

Nikaona nitembelee masoko ya stereo Dar, Buguruni, Mwanza, Kahama na Dodoma! Huko nako nikaamua kupeleka mzigo mwenyewe, madalali Mungu anawaona!!!!

Kila tikiti ukiuza dalali anakula 200! Matikiti mazuri yakiisha inabidi umwachie dalali auze taratibu na ili kupunguza gharama na kuokoa muda umamwachia mzigo!!!

Utaambiwa yalioza, yalishuka bei!! Bla bla nyingi. Nikaona ujinga biashara ya tikiti na ufugaji wa nguruwe haina uwiano kama tunavyoaminishwa kwenye makaratasi na forum kibao!

Nikahamia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa! Mwanzoni kabla ya kuzaa changamoto za kulipa mshahara mfanyakazi, chakula nk. Lakini baada ya kuzaa! Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa!

Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa!
Uko wap mkuu Mimi binafsi nahitaji sana ng'ombe wa maziwa
 
Hongera kwa kufanikiwa kweny ufugaji wa ng'ombe...Kilimo na ufugaji ndivyo ilivyo wewe umepatia ng'ombe..mwingine kapitia tikiti..mwingine kapatia kuku...mwingine kapatia nguruwe...mwingine kapatia nyanya...lakini huwezi kutoa general conclusion kuwa kilimo hiki ni pasua kichwa...
kuna mwingine kakosea ng'ombe pia...tuendelee kupambana
 
Kiufupi Tu kwenye kilimo ni about best luck, unaweza kuoutshine weather problem but you hit market disaster instead
 
Mwaka 2016 mfumo wa maisha ulibadilika baada ya Serikali mpya kuingia madarakani! Vijana wengi tulijikita katika kilimo na ufugaji baada ya motivational speaker kutuhakikishia tutapata utajiri bila kutoa jasho!

Nami nikaanza na nguruwe wenye mimba 3. Mwanzoni hakukuwa na changamoto sana ila shida ilianza walipozaa! Asikwambie mtu kulisha nguruwe ni kipawa toka mbinguni!

Walikuwa wanakula nikanunua gunia 150 za pumba! Walikula mpaka zikaisha kukua hawakui ipasavyo, huku nimeaminishwa nguruwe wa miezi 6 anafikisha kilo 100! Motivational speaker Mungu anawaona!!!!!

Nilikuja kugundua ndani ya miezi 6 nguruwe wana kilo 30-40! Bei ya walanguzi uchwara ni laki hadi laki na nusu! Ukitaka faida uchinje uuze nyama! Ilifikia gunia la pumba 2017 linauzwa elfu 10 na linaliwa siku 1!

Yaani kwa mwezi nguruwe wanakula laki 3! God forbid!!! Nikagundua nimekuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea badala ya nguruwe! Nikaamua kupunguza cost za vyakula kwa kuanza kilimo cha matikiti ili nikiuza yanayobaki madogo madogo nilishie nguruwe!

Hiyo nayo ikawa biashara kichaa, unalima unaivisha vizuri walanguzi wanakuja na bei ya 700- 1000 shambani, unakuwa unarudisha tu mtaji na wakati mwingine mtaji haurudi!!!!

Nikaona nitembelee masoko ya stereo Dar, Buguruni, Mwanza, Kahama na Dodoma! Huko nako nikaamua kupeleka mzigo mwenyewe, madalali Mungu anawaona!!!!

Kila tikiti ukiuza dalali anakula 200! Matikiti mazuri yakiisha inabidi umwachie dalali auze taratibu na ili kupunguza gharama na kuokoa muda umamwachia mzigo!!!

Utaambiwa yalioza, yalishuka bei!! Bla bla nyingi. Nikaona ujinga biashara ya tikiti na ufugaji wa nguruwe haina uwiano kama tunavyoaminishwa kwenye makaratasi na forum kibao!

Nikahamia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa! Mwanzoni kabla ya kuzaa changamoto za kulipa mshahara mfanyakazi, chakula nk. Lakini baada ya kuzaa! Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa!

Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa!

"Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa!

Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa!"

Uko maeneo gani mkuu!! Umenivutia sana. Kama hutojali tatafute namna ya kuonana.
Ahsante
 
Pole sana mkuu,yaliyokukuta kwenye nguruwe
yaliwahi kunikuta.Ila kuna mfugaji ameniambia
kuwa nilikosea,nguruwe mmoja anatakiwa kula kilo moja
ya pumba kwa siku.muda wote uliobakia anatakiwa apewe maji ya kutosha.

Na ikitokea akawa mzembe wa kula,jitahidi uondoe hayo masalia
ili asizoee kula kila wakati.Hayo mabaki kama unafuga bata au kuku wawekee hayo mabaki
na nguruwe mpe maji tu mpaka kesho yake utakapompa haki yaki ya kilo moja ya pumba.
Hii inasaidia kwamba kesho yake ukimuwekea hiyo kilo moja atakula na kumaliza
maana atakuwa na njaa ya jana.
pia epuka mtindo wa kuwawekea nguruwe vitu mbalimbali kama vile mabaki ya vyakula
au makabichi n.k.ukifanya hivyo unamzoesha kula kila mara bila mpangilio
ambao utakughalimu,maana wakihisi njaa watakupigia kelele na kukukosesha amani.

Natarajia kufuga tena kwa kufuata maelekezo hayo,nione kama nitaweza
kupata faida.Hayo maelezo hapo juu nilipewa na mdau anayefuga
ambaye nilimtembelea nikaona mabanda yake ndo akanipa siri hiyo.

Asante sana!
Ni nguruwe wa umri gani anakula kilo moja tu ya pumba kwa siku? au ni yeyote tu awe mkubwa au mdogo?
Nguruwe haitaji vyakula vingine zaidi ya pumba?

Nitashukuru kama nitapata mwanga kidogo kwenye hili
 
Ni wa umri wowote,unaweza kumpa na vyakula vingine ila cha msingi ni kuzingatia muda wa kula.
ule muda ukishapita hicho chakula kitoe ili kesho yake ukiweka anakifakamia chote muda ule ule na baada ya hapo ni mwendo wa maji
hadi kesho yake.
 
Asante sana Kaka kwa ufafanuzi huu
Hivi huu muda wa kula ni kama nikiamua nampa asubuhi saa moja. Ina maana nitampa tena kesho yake saa moja hiyo hiyo.

Sasa ninatakiwa kutoa mabaki hayo saa ngapi kama hakumaliza?
Naomba mwanga kidogo hapo mkuu. Au ni muda ule wa kula mfano nikiweka saa moja inatakiwa akae nacho kwa saa ngapi ndipo nikitoe kama hajamaliza?
 
Asante sana!
Ni nguruwe wa umri gani anakula kilo moja tu ya pumba kwa siku? au ni yeyote tu awe mkubwa au mdogo?
Nguruwe haitaji vyakula vingine zaidi ya pumba?

Nitashukuru kama nitapata mwanga kidogo kwenye hili
Nguruwe wanahitaji usafi,hivyo kabla ya kuweka chakula unahitaji kusafisha banda maana yake huwezi kuweka chakula kabla ya saa mbili.

Hivyo ukiweka chakula masaa mawili mpaka manne yanamtosha kuwa amekula na kushiba.baada ya hapo toa hayo masalia na hakikisha
maji ya kunywa yapo muda wote.

Naomba nikukumbushe kuwa mimi sijaanza kufuga,ila ujuzi huu nimeupata kwa jamaa yangu ambaye nimemkuta anafuga nguruwe.

Kwa ufanisi,nikawa namshangaa na kumsimulia nilivyopata hasara ndo akanipa abc za kufuga wanyama hawa kwa faida.

Nguruwe wake ni wasafi na wana afya bora. Usafi huo wa kila siku unasaidia kuondoa ile harufu mbaya ya nguruwe unafugia nyumbani na si rahisi wageni kugundua kama una nguruwe kwa sababu ya kuidhibiti harufu kwa njia ya usafi.
 
Nguruwe wanahitaji usafi,hivyo kabla ya kuweka chakula unahitaji kusafisha banda maana yake huwezi kuweka chakula kabla ya saa mbili.
hivyo ukiweka chakula masaa mawili mpaka manne yanamtosha kuwa amekula na kushiba.baada ya hapo toa hayo masalia na hakikisha
maji ya kunywa yapo muda wote.
Naomba nikukumbushe kuwa mimi sijaanza kufuga,ila ujuzi huu nimeupata kwa jamaa yangu ambaye nimemkuta anafuga nguruwe
kwa ufanisi,nikawa namshangaa na kumsimulia nilivyopata hasara ndo akanipa abc za kufuga wanyama hawa kwa faida.
Nguruwe wake ni wasafi na wana afya bora. Usafi huo wa kila siku unasaidia kuondoa ile harufu mbaya ya nguruwe
unafugia nyumbani na si rahisi wageni kugundua kama una nguruwe kwa sababu ya kuidhibiti harufu kwa njia ya usafi.
Ushauri mulua
 
Mie mfugaji wa nguruwe nawapatia mashudu ya mise mara moja tu
Kila mwezi nachoma sindani za vitamin
Kila baada ya miezi miwili nachoma sindano za minyoo
Matokeo
Wanakula chakula kidogo sana
Wanakuwa vuzuri sana picha nitaweka kesho.
Nilivyoona mise...nikakumbuka SIDO kigoma, hongera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom