Ukiambiwa uchague kimoja kati ya hizi project za Kilimo utachagua ipi? na why?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
1. Project ya Ng'ombe wa maziwa
2. Project ya Ng'ombe wa Nyama
3.Project ya Mbuzi wa nyama
4. Project ya Mbuzi wa Maziwa.
5.Project ya Kondoo wa nyama
5. Project ya Kuku wa Mayai
6.Project ya Kuku wa nyama/Kienyeji/Chotara
7.Project ya Ufugaji wa nyuki
8.Project ya kilimo cha uyoga
9.Project ya protein mbadala ya Binadamu au mifugo.
10.Project ya ufugaji Samaki.
11.Project ya uzalishaji wa vyakula vya mifugo
13.Project ya Kilimo cha nafaka
14.Project ya Kilimo cha matunda ya muda mfupi au muda mrefu
15.Project ya Spice na herbals
16.Project ya miti ya Mbao na kuni
17.Project ya Sungura
18.Project ya Kware/ Kanga
19.Projects ya Ducks
20.Project ya Miche ya matunda, mboga na miti mingine.
21.Project ya Petties animals
22.Project ya Nguruwe

Unachagua moja tu na sababu zako tusaidie.
 
Unachagua moja tu na sababu zako tusaidie.
Swali zuli, ila ni vyema ukapanua wigo kwa kuongeza malezo.

- Mfano: Uchaguzi Mradi wa Mtanzania wa kiwang cha kati, waweza kuwa tofauti na uchaguzi wa mtu mwenye fedha zake/ tajiri.

- Hivyo ungeongezea na vigezo (criteria) katika uchaguzi wa uchaguzi ili kuboresha mjadala.

My take:

Kwa mtanzania wa kipato cha kati, ningependekeza ufugaji wa kuku wa mayai kama mradi bora. Huu ni mradi rahisi kuanzisha, hauna gharama kubwa, na una faida nzuri.

Sababu zangu ni:
  • Gharama ndogo ya kuanzisha - inahitaji tu boma, vyakula, na kuku wa kutosha.
  • Faida nzuri - mayai yana soko kubwa, na bei nzuri. Kuku mmoja anaweza kuzalisha mayai 300 kwa mwaka.
  • Usimamizi rahisi - hauhitaji elimu ya juu au utaalam mkubwa.
  • Soko kubwa - mahitaji yanaongezeka kila siku.
Kwa hiyo ningependekeza ufugaji wa kuku wa mayai, kwani ni rahisi na wenye tija kwa mtu wa kipato cha kati.
 
Nazani projeft nyingi unaweza zifanya eitjer kwa kiwango cha kati au juu, mfano Ng'ombe, mtu wa chini anaweza kuwa na Ng'ombe 2 ila mtu wa juu akawa na project ya Ng'ombe 50+ wa maziwa
 
Na.2 Kg 1 ya nyama ya ngombe Mchanganyiko ni 9,000-10,000 na ngombe 1 mkubwa ni zaidi ya 700,000.Demand ya nyama kwa Tanzania ni kubwa sana zaidi ya sana, ufugaji ngombe ni zaidi ya utajiri.

sema capital ndio shughuli,risk nyingine ni wizi
Na Kadri population inavyo kuwa kubwa plus majanga ya asili, ndivyo kadri Nyama inavyo adimika,kwa baadae nyama itakuwa dili mno na ghari mno, ni matajiri pekee watamudu kula nyama, mark my words.
 
Inategema na eneo ila kwa huku kusini katika utafiti wangu ,ningechagua namba 1&2 .

Huku hamna maziwa wala nyama yaani ni dili sana hivyo vitu. Kusini haswa Mtwara
Kwa maziwa na nyama now ni karibia nchi nzima, Majanga ya asili hasa Ukame yanateketeza sana mifugo hasa Ng'ombe, hajuna kwenye unafuu sana, hata huku Kaskazini, na kwa baadae nyama itakuja kuliwa na wenye uwezo tu, wengine tutangoja siku za sikukuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom