Kilimo cha umwagiliaji kwa maji ya maziwa

Jan 10, 2018
43
55
Tanzania imezungukwa na maziwa makubwa yenye maji mengi kama vile ziwa Victoria , ziwa Tanganyika, Ziwa nyasa nk. Mara kwa mara viongozi wetu wamesikika wakisema tutumie maziwa haya kwa kilimo cha umwagiliaji, na wakati mwingine watu hujishangaa kwa nini maji haya hayatumiki kwa umwagiliaji.
Sina haja ya kuingilia mijadala hiyo, na kama mnavyonifahamu mimi ni mtu wa vitendo (kumbuka ile thread ya Chia Kilimo na masoko)

Kwanza kabisa tujue kuwa eneo linalofaa kwa kilimo linakuwa usawa wa juu wakati maji yako usawa wa chini (ukilinganisha na eneo la kilimo). Hivyo basi ili uweze kutumia maji hayo kwa umwagiliaji, lazima uyapandishe juu shambani. (Hii ni tofati na umwagiliaji kwa kutumia maji ya mito ambayo huwa yanatiririka kutoka juu kuelekea ziwani au baharini na hivyo unachofanya ni kuyazuia na kuyaelekeza shambani)

Hivyo basi ili uweze kuyapandisha unahitaji mashine yenye nguvu kutegemea na mwinuko toka ziwani. Hapa kuna mashine mbili zinatakiwa. Ya kwanza ni pump ya maji, na ya pili ni mashine ya kuendesha hiyo pump.
Changamoto ya kwanza unaipata hapo - ni pump ya ukubwa gani (uwezo wa kuvuta na kusukuma maji) na horse power zake ukioanisha na mashine (engine) ya kuendesha hiyo pump! Pia hapa kuna suala la mzunguko (rotation) ya engine na mzunguko wa pump Utakutana na kitu kinaitwa RPM.

Kwa sisi tunaoishi vijijini kupatata wataalamu wa mahesabu hayo ni vigumu Kwa hiyo tunategemea zaidi trial and error (kujaribu jaribu). hii husababisha gharama kubwa kwa kujikuta unanunua vifaa ambavyo ni vya bei ndogo na kumbe uwezo wake ni mdogo.

Kwa kuwa maji ni ya ziwa, lazima kukumbuka kuwa huruhusiwi kulima ndani ya mita 60 toka ziwani. Kwa hiyo lazima pump yako iweze kusukuma maji zaidi ya mita 60, na pia kama utataka kuyapandisha maji kwenye tenki la juu huko shambani, lazima ufikirie pia mwinuko wa hilo tank.

Baada ya hapo fikiria kupata mabomba sahihi, ya kuvuta maji na kuyasukuma, vinginevyo ytaishia kupasuka maana kunakuwepo mashindano ya maji (pump inasukuma maji yaende juu na yaliyoko juu yanataka kurudi (gravity); kama bomba si imara basi litapasuka au engine kama haina uwezo wa kutosha itazidiwa na kuzimika (kama gari lililoshindwa kupanda mlima) Madhara ya maji kurudi ghafla ni makubwa maana hupelekea kuharibika kwa pump ya maji.

Sehemu inakayofuata nitaonyesha nilikofikia ili mpate nafasi ya kuuliza maswali na kunipatia ushauri. Msichoke
 
KUJENGA MAHALI PA KUSIMIKA MASHINE
Pump nyingi zilizo madukani zina uwezo wa kuvuta maji kati ya mita 4 hadi 8. Kwa hali hiyo inabidi engine na pump isimikwe karibu kabisa na chanzo cha maji (ziwa). Katika maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo, kando kando ya ziwa ardhi huwa ni tifutifu. Kujengea engine na pump kunahitaji utaalamu na gharama ili kuhimili mtikisiko na wakati mwingine kudidimia.
 

Attachments

  • IMG-20220207-WA0007.jpg
    IMG-20220207-WA0007.jpg
    95 KB · Views: 50
  • IMG-20220207-WA0006.jpg
    IMG-20220207-WA0006.jpg
    140.7 KB · Views: 46
  • IMG-20220207-WA0003.jpg
    IMG-20220207-WA0003.jpg
    112.8 KB · Views: 54
  • IMG_20220206_122853_HDR.jpg
    IMG_20220206_122853_HDR.jpg
    505.2 KB · Views: 54
Mitambo yote hiyo ikishasimikwa lazima kuzuia isinyeshewe na mvua na kupigwa na jua pia. Hivyo kuna kukamilisha jengo dogo ambalo pamoja na kuhifadhi engine na pump, laweza kutumika kutunzia vifaa vidogo vidogo kama spanners, vipuri nk.
Unaweza kuona ziwa nyuma yake
 

Attachments

  • IMG_20220613_100607.jpg
    IMG_20220613_100607.jpg
    496.1 KB · Views: 59
  • IMG_20220508_115527_HDR.jpg
    IMG_20220508_115527_HDR.jpg
    612.1 KB · Views: 44
  • IMG_20220424_174635_HDR.jpg
    IMG_20220424_174635_HDR.jpg
    677.9 KB · Views: 42
  • IMG_20220414_101133.jpg
    IMG_20220414_101133.jpg
    297.4 KB · Views: 61
Hongera sana, hapo umepanga kulima mazao gani?
Mitambo yote hiyo ikishasimikwa lazima kuzuia isinyeshewe na mvua na kupigwa na jua pia. Hivyo kuna kukamilisha jengo dogo ambalo pamoja na kuhifadhi engine na pump, laweza kutumika kutunzia vifaa vidogo vidogo kama spanners, vipuri nk.
Unaweza kuona ziwa nyuma yake
 
Pamoja na kwamba sikuwa na mahesab ya kitaalamu, ni kweli ilinigharimu sana, Lakini sasa maji yameshafika shambani umbali wa mita 300 na mwinuko wa kama mita 20 hivi.

 

Attachments

  • [freemake.com LOGO] VID_20220625_184420.avi
    41.5 MB · Views: 14
Video ya mashine ikisukuma maji imekuwa ndefu hadi iwee edited.
Baada ya maji kufika shambani nilifanya jaribio la kulima mahindi ya kiangazi. Nilipanda mwezi wa nane. Unaweza kuona video hiyo yakiwa mwezi wa kumi October 2022. Hiyo video ya pili, maji yamefikishwa umbali wa mita 600 na urefu wa kwenda juu mita 42, Ndiyo maana unaona kasi imepungua kidogo

 
Video ya mashine ikisukuma maji imekuwa ndefu hadi iwee edited.
Baada ya maji kufika shambani nilifanya jaribio la kulima mahindi ya kiangazi. Nilipanda mwezi wa nane. Unaweza kuona video hiyo yakiwa mwezi wa kumi October 2022. Hiyo video ya pili, maji yamefikishwa umbali wa mita 600 na urefu wa kwenda juu mita 42, Ndiyo maana unaona kasi imepungua kidogo
View attachment 2527528
View attachment 2527531
Pampu unayotumia hp ngapi uwezi kuvuta direct majitoka kwenye chanzo Cha maji mpka shamban bila kutumia tank?
 
Hongera kwa hatua hio. Ila laiti ungejua mwanzoni ingetakiwa hio foundation ungeiweka chini kusingekuwa na 7bu ya kuiweka juu. Kwa uzoef wangu hio water pump inlet inatakiwa isiwe mbali na maji pia isiwe juu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom