Mrejesho: Nyumba yangu kuuzwa

Mrejesho: Nyumba yangu kuuzwa

Dah! Pole dada Mungu akupe Wepesi na kukubariki zaidi
 
Kiufupi wew dada ulivurugwaa hasa kusikia nyumba yako inataka kuuzwa...!! Na mumeo kwa kuwa alikukuta na hiyo nyumba hawezi kuwa na Uchungu nayo hata nuktaa... Hizo helaa zilizobaki nazo atataka mgawanee...!! Kiukweli mwanamke akishapendaa huwa anakuwa FALAAAAA KABISAAAA... yanii upate mwanaume anaejielewa na mwenye huruma na mali ulizonazoo... Lasivyoo atakufilisii zoteee yanii...
 
Sijui ujasiri wa kuwadanganya great thinkers umeutoa wapi wewe mwanamke? Wewe huna nyumba wala mume ila ni kivuruge cha mtaa.
Toa ushahidi, hoja hupingwa kwa hoja! Huenda ni kweli kabisaaaa au ni uongo. Tusaidiane kujua ukweli
 
Kama mambo yenu yanafanana wewe na mume wako.naona umekili ulifukizwa kazi kwa uzembe.

Pia tathimi uhalali wa chanzo cha fedha ulizotumia kujengea.kama zote zilikuwa ni za mkopo na halali basi hiyo ni ajali ya kwaida.ila kama ulichanganya na fedha halamu au za dhuluma basi mara nyingi huwa matokeo yake huwa ni hivyo
 
Ni wengi wanaotamani ndoa ila hujisahau baada ya ndoa kuna maisha ya ndoa
 
Toa ushahidi, hoja hupingwa kwa hoja! Huenda ni kweli kabisaaaa au ni uongo. Tusaidiane kujua ukweli
Hati ya mtu mwingine ukaichukulie mkopo banki tena 20M? Haiingii akilini mkuu labda ingekuwa kwa mtu binafsi tena mwenye uelewa mdogo la sivyo huambulii kitu.
 
Hati ya mtu mwingine ukaichukulie mkopo banki tena 20M? Haiingii akilini mkuu labda ingekuwa kwa mtu binafsi tena mwenye uelewa mdogo la sivyo huambulii kitu.
Hahahahahaa hapo ndio pa kuanzia, la pili, siku hizi bank hawakubali hadi uende na Mrs au asaini. Huenda pengine walifoji...
 
Hahahahahaa hapo ndio pa kuanzia, la pili, siku hizi bank hawakubali hadi uende na Mrs au asaini. Huenda pengine walifoji...
Ni kweli Credit procedure zinataka wife awepo na afisa mikopo ajiridhishe hata kupitia majirani, lakini afisa akipewa rushwa anayoitaka anapindisha tu
 
Ni kweli Credit procedure zinataka wife awepo na afisa mikopo ajiridhishe hata kupitia majirani, lakini afisa akipewa rushwa anayoitaka anapindisha tu
Hebu wanasheria tusaidieni hii kitu.
Ikitokea mtu ametumia vielelezo ambavyo sio vyake na kujipatia mkopo kwa njia ya udanganyifu either afisa mkopo amehusika kwenye udanganyifu au la!
Mwenye mali halisi hawezi kuweka pingamizi la uuzwaji mali yake kisheria kama itabainika hakuusishwa kwenye mchakato mzima?
Achilia mbali mahusiano ya mke na mume sheria itamshughulikiaje mtu kama huyo?
 
Bado ukaendelea kumshirikisha mumeo , wewe ukaenda mahakamani kuweka zuio na yeye harakaharaka katafuta wakili kutoa ushauri , tena wa kumjenga / kumnusuru . Nakuambia utake usitake mtakuja kuachana tu . Tatizo lenu mna udhaifu wa kupenda pale mnapopenda . Hamsubiri kupendwa . Wewe ulijenga nyumba PEKE yako na baadae mkaoana . WANAUME wanahisi sana udhaifu pale anapoona nyumba ina jina la mkewe . Sasa hapo kacheza mahesabu vizuri sana . Nyumba ambayo hakushiriki kujenga ushauza na utakayojenga kwa sasa ni ya wote maana tayari mko kwenye ndoa . UTANISAMEHE PALE NILIPOSEMA MTAKUJA KUACHANA NI KWA SABABU BAADA YA HIYO NYUMBA MTAKAYOJENGA BAADAE , atatafuta mazingira ya kuachana kisha nyumba muuze mgawane . KWA AMRI YA MAHAKAMA .
Mkuu unachosema ni sahihi kabisa hapo hakuna ndoa ni unafiki tu uliobaki atakuelewa baadae sana, alaf hiyo million 10 nayo ataila vizuri tu tena, anatumiwa anasema anapendwa, narudia tena mkuu huyu atakuelew baadae sana
 
Aman iwe kwenu wakuu,

Kutoka Moyoni mwangu, nawashukuru wana jamvi kwa ushauri mzuri. Japo wapo wapo walio nidhihaki nawao pia nawashukuru pia.

Jamani wanaume mnatutesa wake zenu IPO HV wakuu, mume wangu alimchukulia nduguye mkopo wa mill.20 bank akaweka dhamana ya nyumba yetu.

Nyumba ambayo nimejenga kwa jasho langu miaka mitano najenga yeye kaja kunioa juz juz kanikuta nimejiimarisha nyumba yangu imeisha bado kuweka vioo na gypsum tu. Nimetumuia gharama kubwa na mikopo juu ili tu niwe na kwangu.

Akaja kuweka dhamana ya nyumba bila kunishirikisha yaani bado mwezi mmoja ndo napata habar kuwa nyumba yetu inapigwa mnada.

Na usitoshe kwasasa sina kazi ni maza House nimefukuzwa kazi kwa uzembe kazini, na riba imeongezeka plus na dalali jumla nimelipa million10

Amenipa presha nimeuza nyumba yangu, nimelipa deni sasa HV nipo kwenye upangaji napambana na wenye nyumba zao.

Imeniuma SNA wanaume MNA roho gani, yaan hata hamu nae sina natamani niachike ila dini hairuhusu.

HV tukiwasaliti, mtatuona Malaya kweli. Ndoa ngumu ndugu zangu acheni tu.

Umeuza nyumba kwa sababu ya UPUMBAVU!.

Nilikuambia nenda kamwone mwanasheria kwa ushauri. Nikakuambia nyumba ya kuishi haiuzwi. Wewe hukusikia kumbe ukachagua ushauri yeboyeobo.

Nyumba yoyote ya familia hata kama ni ya biashara, haiuzwi kama mwanandoa mmoja haku consent, kumbe iliwekwa dhamana bila wewe kujua. Ungekwenda mahakamani kwa cort injunction ungelikuwa unapiga mruzi tu na nyumba yako ikiendelea kujengwa.

Huyo aliyepewa mkopo angeelewana na bank namna gani amalize deni. Na isitoshe deni kama deni halifungi mtu unless kuna jinai ndani yake.

Wewe ukaona ushauri wa saluni ni bora. Yaone wewe mwenyewe wala usitulaumu wanaume. WANAUME tulikushauri, ukachagua ushauri usio wa kiume!
 
Akaja kuweka dhamana ya nyumba bila kunishirikisha yaani bado mwezi mmoja ndo napata habar kuwa nyumba yetu inapigwa mnada.
Mkuu hebu twende polepole!
Walifoji sahihi yako wakati wa kuchukua mkopo? Kama sio hivyo walifanikiwaje kuchukua mkopo? Maana zama zimebadilika siku hizi.
 
Hebu wanasheria tusaidieni hii kitu.
Ikitokea mtu ametumia vielelezo ambavyo sio vyake na kujipatia mkopo kwa njia ya udanganyifu either afisa mkopo amehusika kwenye udanganyifu au la!
Mwenye mali halisi hawezi kuweka pingamizi la uuzwaji mali yake kisheria kama itabainika hakuusishwa kwenye mchakato mzima?
Achilia mbali mahusiano ya mke na mume sheria itamshughulikiaje mtu kama huyo?

Huyu mlalamikaji ana akili z ayebo yebo. Nilimshauri vizuri lakini akaona kelele za wasuka nywele zinamanufaa kwake, akazifuata. Akauza nyumba kwa upumbavu halafu leo anakuja na makelele ya klaumu wanaume hapa mitandaoni utadhani mme wake ndiye kipimo cha wanaume wote.

Bila shaka kwa akili zake hizi, atajipiza kila siku kwa sababu ya kukosa usikivu na ufahamu wa kuchagua nasaha sahihi.
 
Umeuza nyumba kwa sababu ya UPUMBAVU!.

Nilikuambia nenda kamwone mwanasheria kwa ushauri. Nikakuambia nyumba ya kuishi haiuzwi. Wewe hukusikia kumbe ukachagua ushauri yeboyeobo.

Nyumba yoyote ya familia hata kama ni ya biashara, haiuzwi kama mwanandoa mmoja haku consent, kumbe iliwekwa dhamana bila wewe kujua. Ungekwenda mahakamani kwa cort injunction ungelikuwa unapiga mruzi tu na nyumba yako ikiendelea kujengwa.

Huyo aliyepewa mkopo angeelewana na bank namna gani amalize deni. Na isitoshe deni kama deni halifungi mtu unless kuna jinai ndani yake.

Wewe ukaona ushauri wa saluni ni bora. Yaone wewe mwenyewe wala usitulaumu wanaume. WANAUME tulikushauri, ukachagua ushauri usio wa kiume!
Mkuu hapa either huyu dada anauelewa mdogo kama punje ya haradari au ameleta story ya kubumba.
Alikuja kuomba ushauri wa hili swala na ushauri akapewa tena wenye tija kwake lakini hajaufata.
Alafu kwenye story ya kwanza hakusema kama hajashirikishwa na mumewe wala kuwa nyumba kaijenga mwenyewe.
Alisema mumewe kachukua mkopo wa 20M akagawana na mdogo wake 10 kwa 10 ila shemeji yake kashindwa kurejesha, wamekomaa kulipa hadi imebaki 6M.
Leo kaja na maelezo mengine. Jamani huyu ni muongo hata lolote.
 
nachofaham ukichukua mkopo hati inabaki benki.... umeuzje nyumba bila hati
 
Aliwezaje kuweka bond nyumba ambayo jina si lake? Au hati uliandika jina lake
 
Mkuu hapa either huyu dada anauelewa mdogo kama punje ya haradari au ameleta story ya kubumba.
Alikuja kuomba ushauri wa hili swala na ushauri akapewa tena wenye tija kwake lakini hajaufata.
Alafu kwenye story ya kwanza hakusema kama hajashirikishwa na mumewe wala kuwa nyumba kaijenga mwenyewe.
Alisema mumewe kachukua mkopo wa 20M akagawana na mdogo wake 10 kwa 10 ila shemeji yake kashindwa kurejesha, wamekomaa kulipa hadi imebaki 6M.
Leo kaja na maelezo mengine. Jamani huyu ni muongo hata lolote.

Kweli ni mwongo sana kama siyo basi ni MPUMBAVU, hajielewi. Tuachane naye mkuu.
 
Back
Top Bottom