Mrejesho baada ya kuomba ushauri wa mambo ya mapenzi hapa JF

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,233
22,316
WanaJF natumaini mnakumbuka siku chache zilizopita niliomba ushauri kuhusu jambo langu la mapenzi hapa JF kuhusu mchumba wangu aliyekuwa akisita mimi kuendelea na mchakato wa kutuma mshenga kwao kwa nia ya kumuoa. Kwenye huo uzi nilipata ushauri mwingi ingawa baadhi ya wanaJF wenye roho mbaya walikuwa wakinidhihaki kutokana na mimi kuwa mwanaCCM lialia. Mimi sina tatizo nao kwasababu 2025 tutawaadhibu kwenye sanduku la kura.

Baada ya kutafakari sana kila ushauri nikaamua pia nisome nyuzi za Robert Heriel Mtibeli kama nitaambulia mawili matatu kabla ya kufanya maamuzi magumu. Wengi mlisema niachane nae kwasababu sipendwi na huenda manzi ana mtu mwingine. Hilo labda ni kweli kwasababu hata mimi huwa naona mademu za watu wakitafunwa na watu wengine. Ndo ukweli mchungu. Baada ya kusoma nyuzi za Taikoni na kujiongeza pia nikagundua mambo yafuatayo;

1. Lilikuwa ni kosa kubwa sana mimi kushauriana sana na mchumba. Kuna baadhi ya mambo kwa wanawake haitakiwi demokrasia. Ni YES au NO. Ukitoa nafasi ya kujadili lazima jambo lifeli.

2. Kumwonea mwanamke huruma kila wakati ni vibaya. Wanawake hupenda watu walio rafu na sio kuwa soft sana na kumsikiliza kila kitu. Mfano ni wazee wetu wengi huwa ni amri tu kicheko adimu. Mwanamke ni kumwambia TUNAENDA au HATUENDI. Na kama HAENDI ni kupiga chini kwenda na mwingine.

3. Haki za wanawake ni mtego utakaovuruga ndoa nyingi sana. Kuna mambo yanahusu maamuzi ya wanaume tu.

UAMUZI; Niliongea na mchumba wangu na kumuuliza tuko pamoja au hatuko pamoja. Akajibu tuko PAMOJA. Nikamwambia kama ni hivyo kuanzia leo sitataka kusikia maoni yake kwenye mambo ya mshenga na taratibu zingine zinazotuhusu wanaume. Kukiwa na ulazima atajulishwa. Vinginevyo tusitishe zoezi zima ikiwemo uchumba kuvunjika.

Ameomba radhi na kuahidi kutoleta usumbufu wowote tena. Tayari mshenga kashaenda kwao. Nadhani muda wa harusi ukifika nitawaalika wote hapa JF. Natumaini Lucas mwashambwa Magonjwa Mtambuka FaizaFoxy Erythrocyte Mshana Jr na wanaCCM wengine mtanisapoti kwa karibu.
 
baadhi ya wanaJF wenye roho mbaya walikuwa wakinidhihaki kutokana na mimi kuwa mwanaCCM lialia. Mimi sina tatizo nao kwasababu 2025 tutawaadhibu kwenye sanduku la kura.
Madhara ya ndoto nyevu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom