Mramba anasafishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mramba anasafishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 9, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,782
  Likes Received: 83,139
  Trophy Points: 280
  Mramba aandaliwa mapokezi mazito
  • Mahakama yamruhusu kutembelea jimbo

  na Happiness Katabazi
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu


  HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Rombo, anayekabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha, Basil Mramba, kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku 29 kwenda kuwasalimia wananchi jimboni mwake.

  Kutokana na ruhusa hiyo, Mramba sasa anatarajia kwenda jimboni kwake kesho ambako inaelezwa kwamba ameandaliwa mapokezi makubwa kutoka kwa wapiga kura wake kwa lengo la kumpa pole kwa matatizo yaliyomfika.

  Diwani wa Kata ya Kelamfua Makola, Kata ya Mkuu Rombo, Festo Kilewe, aliiambia Tanzania Daima kuwa Mramba aliyekuwa rumande kwa kesi hiyo na baadaye kuachiwa kwa dhamana, ameandaliwa mapokezi makubwa na atafanya ziara katika kata za jimbo lake kuhamasisha shughuli za maendeleo.

  Mipango hiyo imethibitishwa pia na msaidizi wa mbunge huyo, Roman Kilega, ambaye alisema Mramba atakuwa na ziara ya siku nne, ambapo ataanzia Kata ya Tarakea na Useri kuhamasisha ujenzi wa madarasa ya shule pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tarakea hadi Mkuu Rombo na kutoka Mkuu Rombo hadi Marangu.

  “Kwa vile mahakama imetoa ruhusu hiyo leo (jana), tunatarajia atawasili hapa kati ya Ijumaa na Jumamosi na wapiga kura wake wamejiandaa kumpokea kwa kishindo ili kumpa pole,” alisema Kilega.

  Uamuzi wa kumruhusu Mramba kwenda jimboni mwake, ulitolewa jana na mahakama hiyo kutokana na ombi la Mramba lenye kumbukumbu namba 10RCA/A1/64/2009, lililowasilishwa Ijumaa iliyopita na wakili wake, Hubert Nyange na Peter Swai, kutaka aruhusiwe kwenda jimboni kuwasalimia wapiga kura wake.

  Akitoa uamuzi huo jana, Mwankenja alisema, amezingatia ibara ya 13(6)(B), inayotamka kwamba mtu asichukuliwe kuwa ana hatia hadi mahakama itakapomkuta na hatia na ibara ya 17 ya katiba ya nchi, inayosema kila mtu ana haki ya kutembea.

  “Kwa kuzingatia ibara hizo za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mahakama inakubaliana na ombi la Mramba kwa sababu bado hajakutwa na hatia, pia ana haki ya kutembea ili mradi asivunje sheria za nchi, na kwa sababu hiyo kuanzia sasa mshitakiwa anaruhusiwa kutoka nje ya mkoa huu.

  “Pia niliipitia kwa kina sheria ya Bunge la Tanzania kabla ya kutoa uamuzi huu, kuona mbunge anayeshitakiwa mahakamani kwa kesi za jinai, anatakiwa atendeweje, nimebaini sheria hiyo haisemi chochote katika hilo, hivyo nimetoa uamuzi wangu kwa kutumia ibara hizo nilizozitaja ambazo zipo kwenye katiba ya nchi,” alisema Mwankenja.

  Ijumaa iliyopita Mramba kupitia mawakili wake aliwasilisha ombi mahakamani hapo akitaka aruhusiwe kutoka nje ya Dar es Salaam kuanzia Januari 3 hadi Februari mosi mwaka huu.

  Ruhusa hiyo itamwezesha pia mbunge huyo kuhudhuria mkutano wa Bunge unaotarajia kuanza Januari 27, lakini pia huenda akalazimika kuomba muda mwingine kwani kwa ruhusa ya sasa, ana uwezo wa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku sita kabla ya muda aliopewa wa Februari mosi kumalizika.

  Mramba ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya jinai namba 1200 ya mwaka jana, ambapo anashitakiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

  Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Awamu ya Nne pamoja na Yona na Mgonja, wanakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

  Ilidaiwa kuwa kwa makusudi au kwa kushindwa kuchukua tahadhari kwa mujibu wa taratibu za kazi, akiwa Katibu Mkuu Hazina na wakiwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu waliruhusu kutolewa kibali cha serikali kilichoisaidia Kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) Government Bussiness Corporation kutolipa kodi, tofauti na mapendekezo ya Mamlaka ya Mapato (TRA), uamuzi ambao uliisababishia serikali hasara ya sh 11,752,350,148.00.

  Wakati huo huo, Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya, amesema Januari 16 mwaka huu, atatoa uamuzi wa kukubali au kutokubali mtuhumiwa wa 21 wa wizi wa Fedha katika Akauti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jonathan Munisi, aunganishwe kwenye kesi inayomkabili ya mfanyabiashara Japhet Lema.

  Lyamuya aliyasema hayo jana baada ya kusikiliza hoja za upande wa wakili wa serikali Fredrick Manyanda na wakili wa utetezi Evarist Mbuya ambapo upande wa utetezi uliomba mteja wao, aunganishwe kwenye kesi inayomkabili Lema kwa sababu mashitaka yake, yanafanana na yanayomkabili mteja wao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 9, 2009
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Utaendeshaje vita dhidi ya ufisadi kama wananchi sisi wenyewe tunasema pole kwa kushikwa kwa ufisadi lakini hongera sana, siku nyingine uhakikishe hushikwi!!!!!!!!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,782
  Likes Received: 83,139
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Kichuguu. Hili linasikitisha sana. Kwanza Lowassa alipewa mapokezi ya nguvu baada ya kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, akafuata Mzee wa Vijisenti naye akapewa mapokezi ya nguvu kwenye jimbo lake na sasa Mzee wa "Hata Majani tutakula lakini Rada ni lazima inunuliwe" halafu CCM imeyafumbia macho na kukaa kimya kabisa kuhusu mapokezi haya ya Watuhumiwa. Halafu wakati huo huo inajitangaza inapambana na mafisadi!!!!
  Huyu angepewa masharti na korti unaenda kwenu basi hustahili kupokewa kwa mapokezi makubwa lakini kaachiwa tu sasa anapeta!!! Bongo inastaajabisha kweli kweli!!!
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Njaa, shida, na kukosa matumaini ni kitu kibaya sana...
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na maneno yako; utashangaa kugundua kuwa sehemu kubwa ya hao "wapokeaji" ni watu waliokatiwa kitu kidogo.
   
 6. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna, because sehemu nyingine za watu wenye njaa na shida, mafisadi wananyongwa (revolutions are created etc)...hii ni simple case ya "miafrika ndivyo tulivyo..", Lowassa was greeted as a hero, so did Chenge..beyond any rational explanation

  must be in the genes...
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Duh!! Inawezekana lakini nadhani huenda siyo kweli.

  Nafahamu kuwa kule Ukerewe mafisadi walikuwa wakipigiliwa mambo vichwani na kufungwa jiwe zito baadaye wakatoswa majini; Mkandara anaweza kuniunga mkono kwa hili.
   
 8. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa nashangaa sijui sikuhizi values zetu zimeenda wapi, maana ni mbunge huyo huyo aliwaambia wanyonge hao hao kama ikibidi, "wale nyasi" ...sasa wanawapokea hawa watu kwa shangwe....na leo naona yule waziri aliyesema labda Chenge aliuza Ng'ombe ku-justify his money - ameshinda UWT - na bado...
  ...ndidyo tulivyo...
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Semo semo mafisadi's style, ilianzishwa na Lowassa, Mkapa, Chenge, now Mramba kwenda kuwadaganya wananchi wa jimboni, maana huku mjini hakuna wa kumpandisha mkenge, akirudi mjini kesi Kisutu iko pale pale, mpaka kieleweke!

  - Hivi jamani si nimewahi kusikia kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa kuwa na shule nyingi za secondari na elimu Tanzania au? Kuwa na shule yningi sio guarantee kua wananchi watakuwa na na elimu? I mean this mapokezi ya fisadi is beyond imagination!
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kwani kuna tofauti gani kati ya Sofia Simba na Janet Kahama?
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mapokezi atakayopewa Mramba hayawezi kufikia yale waliyopewa Lowassa na Chenge huko majimboni kwao. Sababu hasa ni hiyo uliyoieleza hapo juu. Ila pia tuangalie hili suala kwa upana kidogo, hasa tunapojadili jimbo la Rombo.

  Baada ya uchaguzi wa mwaka wa 1995 CCM ilishindwa vibaya Kilimanjaro; isipokuwa Rombo; tena Mramba aliibuka "miongoni" mwa wabunge waliopata kura nyingi kuliko wote Tanzania nzima.

  Serikali ya Che Nkapa kwa sababu hiyo pamoja na sababu zingine (zinazojulikana) wakaamua kumpiga tafu Mramba. Leo hii sehemu kubwa ya Rombo ina maji "safi" ya bomba ("masafi kuliko ya Dar, sababu unakunywa bila kuchemsha bila madhara), sehemu kubwa ina umeme, simu za ttcl, vijizahanati vya kumwanga (vya serikali au vya misheni), na barabara ndio hiyooo mlisikia Mramba akishikiwa bango bungeni kuwa anajipendelea. Ohh mtakumbuka pia kulikuwa na ule mpango wa kujenga Airport ndogo kule Tarakea..!!

  Yote hiyo ilikuwa ni kuhakikisha jimbo la Rombo linabaki imara chini ya CCM na pia ikiwezekana linabaki chini ya Mramba. Sasa, mtanisamehe iwapo nikisema "sikubaliani" warombo kumpokea kwa kishindo, lakini naelewa kwa nini wanafanya hivyo.

  FMES...Kilimanjaro inashika namba za juu kuwa na shule nyingi lakini siku hizi shule hizo zimejaa Wanyamwezi, Wagogo na wengine kutoka kila kona ya Tanzania...Wachaga wenyewe watoto wao wanasoma Jitegemee, St Mary's, Lake Sec na kwingineko..!!
   
 12. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  both were rotten..that was an example... then again i am not surprised, mambo ya Takrima hayo, Miafrika inashangilia chochote tu wanachokiona kinamelemeta (VX, big smiles, funny gold watches leaders wear...etc)

  ..ndivyo tulivyo
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kweli safari ya vita dhidi ya ufisadi bado ni ndegu jamani,sasa wanamuandalia mapokezi kwa ajili ya nini???,kwamba ameshinda kesi yake ama!!!(kama ningekuwa ni mimi hata ningekuwa nimeshida kesi nisingekubali kupokelewa),,,huu ni ujinga mtupu jamani,,,Lazima hao wanaompokea wameandaliwa na kukatiwa mshiko kama ilivyokuwa kwa EL na AJC (WIZI MTUPU)...Pia usishangae kuona anapokelewa na DC na viongozi wengine wa wilaya wakiwepo wale wa CCM...Siasa za Bongo jamani,sometimes zinasikitisha na kufurahisha kwa wakati mmoja...Hata wafanye nini Mramba ni Fisadi na DAIM ataendelea kuitwa FISADI
   
 14. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Suala la kupokelewa kama shujaa kwa mafisadi ni tete sana, wananchi wana treat hao mafisadi kama watoto wao. Mtoto wako hata akiwa muuaji au haramia still utamkumbatia na kumpa busu ili hali ukimuonya to change. Wananchi waliowengi hasa wanakotoka hao mafisadi angalieni je wamecontribute kiasi gani kuleta maendeleo katika sehemu zao. wheather waliiba ama kukiuka taratibu. Mie siwalaumu wananchi 100% Kwani hata kama ni fisadi basi alikula na watu jamani. Hapa ndiyo sheria kiimla zingetumika!! Shoot em. Period. Lakini ukiwaacha still ni syndicate babu kubwa na hamuezi kijua who is who!! wamo wa kila aina. wali bado kukamatwa wanasazisha mambo kimyakimya.
  TUNZENI HAYA MAANDISHI. HAWA WALIOKAMATWA WATAACHIWA TU ONE DAY. HAKUNA ATAKAYEFUNGWA HAPO.
   
 15. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Ndio demokrasia.
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Jamani, mmeshamhukumu Mramba? Kwani ukishukiwa kosa basi umeshakuwa mkosaji? Kuweni na subira.

  Mjue vile vile hizi kamata kamata ni cheap politics. Kwenye ushahidi kama kwa Lowasa hakamatwi mtu, lakini hapa kwa Mramba penye shuku ya kutofuatia maoni na TRA ndio wanakamata!

  Ushauri ni ushauri tu. Kama Mramba alipuuza ushauri wa TRA, basi bosi wake anaweza kumfukuza kazi, lakini hawezi kumfunga. Kumkamata na kumweka ndani Waziri kwa kutofuata ushauri ni kosa kubwa!

  Warombo watampokea "kijana wao" anayeonewa na watu wanaotafuta kuchaguliwa tena 2010. Hawampokei "fisadi" kwani hajatiwa hatiani.
   
  Last edited: Jan 9, 2009
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Samahani Yebo*2, Nadhani kama sikosei mwaka 1995 Mramba aliangushwa Rombo na Jamaa mmoja kutoka CHADEMA aitwaye Salakana ( sijui sasa hivi yuko wapi), baada ya hapo Che Nkapa akamteua Mramba kuwa RC Mbeya.

  Naruhusu kurekebishwa kama kumbukumbu zangu hazijakaa vizuri

  Asante
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ni jambo la kufurahisha sana kusikia kuwa mtu aliyezaliwa na kukulia kwenye nchi inayoitwa Tanzania leo hii akisema kuwa afadhali kutumia sheria za kiimla. Watu tumechoka kusubiri tena

  Inanikumbusha kule kwetu kulikuwa na aina fulani ya mihogo ambayo ilikuwa haiivi hata ukiichemsha miaka mingapi. Halafu ilikuwa ni vigumu sana kuitofautisha mihogo ile na mingine kwa macho tu hata ukiionja kabla ya kuipika. Kwa hiyo sheria ilikuwa ni moja tu, isipoiva baada ya muda fulani unaipakua na kuitupilia mbali kwa vile tunajua kuwa haitaiva.
   
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani ni wapambe wachache, alafu... ni kawaida ya binadamu kumwangalia mtu akiwa amepata matatizo kumuangalia anakuwa vipi angawa anakuwa Mramba yule yule!

  SIo lazima watakaokuwa kwenye mapokezi wakawa watu wanaomshabikia... wengine wanaweza kuwa watu wanaomkejeli.
   
 20. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
   
Loading...