Msaranga
JF-Expert Member
- Feb 10, 2009
- 956
- 227
kwa kweli nchi hii si jui mtanzania atafaidika kwa lipi na rasilimali za nchi yake jamani kama waziri ananisikia naomba achukua tahadhari mapema kabla hatujaenda mjengoni.na unajiuliza kama kweli walengwa wa mpango huu ni watanzania, maana kipato cha watanzania kinafahamika. Huu ni mpango wa kuwafungia milango wenye shida ya viwanja kweli na kuwaachia wale wenye tabia ya kuhodhi. Kama mtu anatakiwa kulipa milioni 9 katika wiki 1 kabla hata hajajua bei ya tofali au trip ya mchanga basi huyo si mtanzania wa kawaida. Je watanzania elfu 20 wa kipato hicho wanatoka sekta gani? Hivi ni lini watu watafaidika na rasilimali zao ndani ya nchi yao? Wanataka ku-achieve nini na wanalenga watu gani?