Mradi wa Viwanja vipya - Kinyerezi

jamani wadau kuna mtu ameliona hilo tangazo kwenye gazeti lingine zaidi ya mtanzania? kama mwananchi ambalo lina mtandao mkubwa nchini au limetangazwa kwenye mtanzani ambalo haliuzi copy zaidi ya 1000 kwa lengo maalum
 
  • Thanks
Reactions: Aza
nenda pale mbezi unanunua viwanja vinne kwa iyo bei na unapata na hela ya kuanza ujenzi kila kiwanja cha 30x 30 ni millioni mbili umeme upo kasoro maji

mkuu mbezi ipi hiyo? naomba uniPM aisee am serious
 
hili nalo neno. ngoja kesho niamkie huko nijue kinachoendelea nitawajuza baadae nikitoka huko. twende tu tukapambane na ho mafisadi. tuchukue form hata kama hatuna hela.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Watanzania tuna safari ndefu ya kwenda.
Hivi huyu prof. Anataka watu wa aina gani wakakae kule kinyerezi?
Hebu atueleze tunapata wapi 9mil kwa muda wa wiki 1.
Labda mafisadi ndio watakao nunua,
hii lazima ifike wakati tukatae tu.
Hiwezekani jamani haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa?
 
kwa standard ya upimaji huwezi nunua sq meter moja au mbili unaanzia sqm480 na kuendelea kwahiyo ni tsh 4,800,000/= .zipo standard low density na high density wataalamu watusaidie dimension zake tafadhali

Katika standard za viwanja vya makazi, kiwanja kidogo kinaweza kuwa na ukubwa wa 400 mita za mraba (sq.m) na kiwanja kikubwa kabisa hadi mita mraba 5000 au zaidi kwa maeneo ya shule na viwanda. Bei ya kiwanja inaweza kupangwa kwa vipimo vya mita au futi (metre or feet). Hivyo, bei ya kiwanja itakuwa kwa mita za mraba au futi za mraba. Haimaanishi kwamba unaweza kununua mita moja ya mraba. Viwanja vyoye vikishapimwa ukubwa wake unaonyeshwa kwenye ramani, hivyo, kulingana na ukubwa wa kiwanja bei itakuwa kama ifuatavyo. Kwa mfano kama, bei ni sh. 10,000 kwa mita moja ya mraba na kama ukubwa wa kiwanja ni mita za mraba 400, ndio kusema gharama ya kiwanja itakuwa 10,000x400 = 4,000,000/=. Hesabu rahisi tu za kuzidisha.
 
ila elewa wavitumia kwa sasa ila wakiondoka tutavitumia tuu wewe huoni sasa kuna daladala zinaenda masaki je mwaka 2007 zilikuwepo.

Masaki wanaopanda Daladala ni wafanyakazi wa Hotel,Maduka,ofisi nk wengineo wengi...
 
mkuu labda unisaidie kitu hiki kabla sijachangia, umesema square metre sh.10,000/=, ina maana mtu akitaka square metre 3 atalipa 30,000/=, ivo ivo akitaka sq.metre 4 ataongeza elfu 10,000/= ivo ivo mpaka metre sq.metre 30 atalipa elfu kumi kumi mpaka mra 30, je itafika 9,000,000/=. Mimi nafikiri itakuwa 10,000/=mara 30 ambayo ni sawa na (10,000/=*30= 300,000/=) plus 10,000/= ya maombi. Au apa na ela inawekwa kwenye meter squared?????????? Kazi ipo.
Kwa nini isifike au hujaelewa Soma...! Ndio maana kumbe huwa mnafail... lol Kakuambia square meter 30 kwa 30 ndani yake humo utapata square meter jumla 90 so ukizidisha kwa kumi elfu utapata hiyo hesabu yake ya Million 9 Kama hujaelewa kajiandikishe tena Shule...

2005 nilishanunua changu kwa laki tano na ushee nishafuatwa na watu last year wanakitaka kwa million hizo 9 this year wanakitaka kwa million 10 nasubiri 2015 nikiuze kwa Million 15 nipate pesa ya kugombea au kwa jina lingine Mtaji wa Uraisi, kwa kuiongoza Tanzania ni kazi rahisi kama tujioneavyo wenyewe naanza kujifunza kucheka cheka... na kukemea kwa upoleeeeeee ai jamani mawaziri fanyeni kazi..... Can't you Behave Yourself! agrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Elewa hivi. Ufisadi ni mfumo wa kunufaisha kikundi fulani chenye uwezo kipesa. Hata ufanye nini, hata uhubiri dini gani; ufisadi hauondolewi kwa maneno. Hivi ni vita vya kitabaka, na kila tabaka hutetea maslahi yake, ndugu zangu. Utaandika sana na mafisadi wanasoma sana yanayoandikwa humu. Lakini kwa sababu ni maandishi tuu hayawanyimi usingizi.

Ili kuushinda ufisadi, unahitaji serikali inayolinda na inayotetea maslahi ya wanyonge . Serikali (dola) ambayo itatumia nguvu za dola kuangamiza ufisadi. Kwa sasa Tanzania haina serikali ya namna hiyo.

Nchi hii sasa inahitaji ukombozi wa dhati. Amini usiamini, we have the wrong class in power. Mwanachi wa kawaida sio lengo lao wala hayuko katika mawazo yao. Ukiuelewa ukweli huu, utafungua akili yako ili itafakari njia mbadala ya kuwaletea wananchi (wenyenchi) maendeleo ya kweli na haki yao ya kufaidi keki ya taifa. Lakini kama utategemea CCM na serikali yake kuwanufaisha wanachi then there is something seriously wrong with your ability to see, analyze, synthesize and interpret facts and figures. WAKE UP and JOIN STRUGGLE.
 
mkuu labda unisaidie kitu hiki kabla sijachangia, umesema square metre sh.10,000/=, ina maana mtu akitaka square metre 3 atalipa 30,000/=, ivo ivo akitaka sq.metre 4 ataongeza elfu 10,000/= ivo ivo mpaka metre sq.metre 30 atalipa elfu kumi kumi mpaka mra 30, je itafika 9,000,000/=. Mimi nafikiri itakuwa 10,000/=mara 30 ambayo ni sawa na (10,000/=*30= 300,000/=) plus 10,000/= ya maombi. Au apa na ela inawekwa kwenye meter squared?????????? Kazi ipo.

kwa hesabu yako inabidid uanze upya chekechea
 
hata wangeviuza 500,000. bado wangeuziana wao kwa wao tu. This govt is rotten when it comes to corruption.
 
Jamani mbona hii thread niliipost juzi jumanne lakini haikupata wachangiaji? Nimemaindi Kimtindo.....hii ni kama mwandishi wa habari kuchukua habari ya mwenzie na kuiuza ati!
 
hata wangeviuza 500,000. Bado wangeuziana wao kwa wao tu. This govt is rotten when it comes to corruption.

ni kweli kabisa halafu najiuliza waposema pesa ya kurudisha form aitarudishwa(non refundable). Je wataangalia vigezo gani ili upate hicho kiwanja? Maana naona kama viwanja ni 20,000. Wakijaza watu 40,000, watakosa watu 20,000(tayari inabidi mazingira ya rushwa yawepo ili upate) then sidisha hiyo 20,000 mara tsh 20,000 ya form (20,000x20,000 = 400,000,000)!! Hizo zitaliwa na wachache...
My take: Wangesema watu 20,0000 waishakamilika hawatapokea tena maombi otherwise ni wzi mtupu
 
mkuu labda unisaidie kitu hiki kabla sijachangia, umesema square metre sh.10,000/=, ina maana mtu akitaka square metre 3 atalipa 30,000/=, ivo ivo akitaka sq.metre 4 ataongeza elfu 10,000/= ivo ivo mpaka metre sq.metre 30 atalipa elfu kumi kumi mpaka mra 30, je itafika 9,000,000/=. Mimi nafikiri itakuwa 10,000/=mara 30 ambayo ni sawa na (10,000/=*30= 300,000/=) plus 10,000/= ya maombi. Au apa na ela inawekwa kwenye meter squared?????????? Kazi ipo.

Gsana

Square metre moja ni 10,000/=
Kwa hiyo kwa kiwanja cha square metre 30, maana yake ni 30m times 30m = 900 square metres , kwa maana ya kipimo cha eneo ra mraba.

sasa zidisha hiyo 900 kwa 10,000/= unapata 9m.
 
Solution ya kununua viwanja bongo bado sana maana gharama zenyewe za viwanja zipo inflated na hata hizo za ujenzi zipo juu kinoma. Yaani hapa nilipo hata kufikiria kukarabati kibanda cha Bi. mkubwa napata kizunguzungu. Huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, maana binadamu wote tunahitaji malazi bora.

Suala la makazi Tz linahitaji uelekeo mpya. Uwezo wa kununua kiwanja achilia mbali kujenga ni muhali kwa wengi wetu, sana tu, unless uwe ni fisadi au una mabiashara yako yanayolipa. Option bora ya kudhibiti ujenzi holela ambao ni tishio kwa hata miji ya huko bara, ni kuwa na mfuko wa kujenga makazi nafuu ambapo nyumba zinajengwa systematically sanjari na huduma zengine nyeti. Kwa mwendo huu wa sasa makazi holela yataendelea kwa kasi ileile na kila siku watu watakuwa wanalalamikia bomoaboma na kukosekana kwa huduma muhimu za maji, umeme, barabara nk.
 
Tarehe 16/05/2011 nilisoma Tangazo kwamba serikali imepima viwanja Kinyerezi inaviuza kwa bei ya mita moja ya mraba shiringi 10,000, 15,000, 20,000, 5,000 na 8,000 kwa Viwanja vya makazi, makazi na biashara, huduma za jamii na ibada respectively, bei ambazo Watanzania wachache (hasa humu JF)wenye uelewa walilalamikia, mimi nikiwa mmoja wao, Pamoja na hayo jana nikaamua kwenda kujipinda kulipia form, leo nimeenda mahala husika(viwanja vya anautogro) na pay in slip ili kuchukua form za maombi, sijaamini nilichokiona kwasababu nimekuta kuna foleni ya watu wasiopungua miatano(500) na baadhi yao wana form zaidi ya moja mkononi na mbaya zaidi watu wanazidi kumiminika kulipia forms. Binafsi nilijua tutakuwa wachache sana tulioamua kujilipua kwa hizo bei, ndipo nikajua kumbe Watanzania wana pesa nyingi sana haiwezekani bei kubwa namna ile kukawa kuna ushindani mkubwa kiasi hicho. baada ya kudodosa dodosa nikaambiwa viwanja tunavyogombea vipo jumla 150 tu ambavyo kimsingi watapata watu 150 tu. Kwasababu mimi naamini haki itatendeka hivyo mtu wa kwanza kuviomba mpaka wa miamoja hamsini(150) ndiyo watakaopata, sisi wengine imekula kwetu sikutaka niendelee kupoteza mda wangu nikaamua kujiondokea na kuiachia serikali 20,000 ya form.

Nikiwa naondoka nilijaribu kuingizia habari za bei za viwanja kwa watu niliokuwa karibu nao wengi walionyesha hawajui bei yake na mbaya zaidi hawajui hata unaposema Mita moja ya mraba unamaanisha nini, na chakustaajabisha zaidi wengi wa watu wa namna hiyo wamelipia form za maombi ya viwanja zaidi ya kimoja.

Mtu mwingine nilipo muuliza alinijibu kwamba yeye anataka kiwanja kimoja tu cha mita 40 kwa 30 ili jumla iwe mita 70 maana ana 700,000 kwenye akaunti yake ambayo alikuwa anatafuta sana eneo la kujenga kibanda cha kujihifadhi.

Kutokana na niliyoyaona leo serikali inatakiwa inapotoa tangazo itoe kwa makusudi elimu ya ziada kwa umma maana siyo wote wanaelewa nini maana ya mita moja ya mraba, wangetoa mfano kwa kiswahili kwamba kiwanja cha 40 kwa 30 ni Milioni12 kusingekuwa na msongamano wa watu wengi kiasi kile, vinginevyo itaishia kuzikusanya elfu ishiriniishirini za Watanzania wengi ambao wana elimu duni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom