DOKEZO Mwekezaji analipa fidia ‘kiduchu’ kwa Wananchi katika Mradi wa Madini ya Mchanga Kigamboni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wilaya ya Kigamboni, Kata ya Kisarawe 2, Mitaa ya Mwasonga, Sharrif na Madege wamelipwa fidia isiyo stahiki na Mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Nyati Sand Resources Ltd inayomilikiwa na Strandline Resources ya Australia (84%) na Serikali ya Tanzania (16%).

Awali, Mwaka 2016, wahusika walikuja na mpendekezo hayo ya kutaka kutulipa Sq Meter kwa Shilingi 3,000, lakini baadaye wakareje na kutengeneza mazingira ya vitisho na kuanza kuwalipa Wananchi kati ya Tsh. 1,730 mpaka Tsh. 3,000 kwa Sq Meter.

Walipokuja mara ya pili, pamoja na Wananchi kulalamika na kupeleka malalamiko kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara, Bungeni lakini mamlaka zinazohusika zikafumba macho na zimeendelea kufumba macho na kumuacha mwekezaji alipe Wananchi pesa kiduchu kwa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa kwa ajili ya kupisha mradi wa madini ya mchanga.

Wananchi asilimia 90 wamekubali kulipwa fedha hizo kiduchu kisha wakitakiwa kwenda kujitafutia viwanja wenyewe na kujenga kwa gharama zao wenyewe, waliosalia mpaka sasa ni takribani Asilimia 10 ndio hawajalipwa kwa kuwa wamekataa malipo.

Ukweli ni kuwa sisi wakazi wa Kigamboni tunafahamu thamani ya ardhi yetu, kwani kuna wawekezaji wamekuwa wakilipa Shilingi 30,000 kwa sq metre moja, sasa hii ambayo tunalipwa na mwekezaji haikidhi hata kupata kiwanja na kujenga nyumba sehemu nyingine Dar es Salaam labda uamue kwenda nje ya mjini kabisa.

Tumekuwa tukifuatilia kwa muda mrefu kuwa wanachokifanya si sawa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Baadhi ya wanaosimamia Mradi huo ambao bado haujaanza wanadai Serikali ndio imepanga lakini mwekezaji alikuwa tayari kulipa malipo mazuri.

Viongozi wetu wa Serikali za Mtaa hawana nguvu ya kutengeneza hoja kwa kuwa inavyoonekana ni maagizo kutoka juu.

Miaka ya nyuma Naibu Waziri Mkuu wa sasa, Dotto Biteko akiwa Waziri wa Nishati aliwahi kufika hapa tukamweleza hoja zetu, akawa kimya na hakutupata majibu mpaka leo.

Hiyo inakuonesha kuwa jinsi gani kuna mazingira tata ndio maana hata Serikali za Mtaa hawana ubavu wa kufanya chochote.

Tunaomba Dunia ifahamu kuwa Wananchi waliochuku fedha wamefanya hivyo kwa kuwa wanahofia usalama wao na ambao hawajachukua hatujui nini kitawatokea kwa kuwa mradi haujaanza na kunaonekana kuna mazingira flani ya ‘udalali’.
 
Kule Toangoma kuna machimbo bubu yanaendeshwa na wwnyeviti wa mitaa na maafisa mazingira wasio waaminifu wa Manispaa ya Temeke.

Mashimo yanahatarisha future ya mazingira ya kule. Waende block 9 Kibada watashuhudia hayo......
 
Kulalamika mnajua vizuri linapo kuja susla la kupiga kura kutafuta viongozi wa takao wajibika, mkipewa kanga na sabuni mnaanza kuiba nyimbo za kupamba chama, wengine hata kuhoji biongozi hamwezi kwahiyo msilalamike sasa hivi plz.
 
KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika. Ila ingekua kutengeneza MOVIE hapo chapu angekuja location
 
Wilaya ya Kigamboni, Kata ya Kisarawe 2, Mitaa ya Mwasonga, Sharrif na Madege wamelipwa fidia isiyo stahiki na Mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Nyati Sand Resources Ltd inayomilikiwa na Strandline Resources ya Australia (84%) na Serikali ya Tanzania (16%).

Awali, Mwaka 2016, wahusika walikuja na mpendekezo hayo ya kutaka kutulipa Sq Meter kwa Shilingi 3,000, lakini baadaye wakareje na kutengeneza mazingira ya vitisho na kuanza kuwalipa Wananchi kati ya Tsh. 1,730 mpaka Tsh. 3,000 kwa Sq Meter.

Walipokuja mara ya pili, pamoja na Wananchi kulalamika na kupeleka malalamiko kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara, Bungeni lakini mamlaka zinazohusika zikafumba macho na zimeendelea kufumba macho na kumuacha mwekezaji alipe Wananchi pesa kiduchu kwa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa kwa ajili ya kupisha mradi wa madini ya mchanga.

Wananchi asilimia 90 wamekubali kulipwa fedha hizo kiduchu kisha wakitakiwa kwenda kujitafutia viwanja wenyewe na kujenga kwa gharama zao wenyewe, waliosalia mpaka sasa ni takribani Asilimia 10 ndio hawajalipwa kwa kuwa wamekataa malipo.

Ukweli ni kuwa sisi wakazi wa Kigamboni tunafahamu thamani ya ardhi yetu, kwani kuna wawekezaji wamekuwa wakilipa Shilingi 30,000 kwa sq metre moja, sasa hii ambayo tunalipwa na mwekezaji haikidhi hata kupata kiwanja na kujenga nyumba sehemu nyingine Dar es Salaam labda uamue kwenda nje ya mjini kabisa.

Tumekuwa tukifuatilia kwa muda mrefu kuwa wanachokifanya si sawa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Baadhi ya wanaosimamia Mradi huo ambao bado haujaanza wanadai Serikali ndio imepanga lakini mwekezaji alikuwa tayari kulipa malipo mazuri.

Viongozi wetu wa Serikali za Mtaa hawana nguvu ya kutengeneza hoja kwa kuwa inavyoonekana ni maagizo kutoka juu.

Miaka ya nyuma Naibu Waziri Mkuu wa sasa, Dotto Biteko akiwa Waziri wa Nishati aliwahi kufika hapa tukamweleza hoja zetu, akawa kimya na hakutupata majibu mpaka leo.

Hiyo inakuonesha kuwa jinsi gani kuna mazingira tata ndio maana hata Serikali za Mtaa hawana ubavu wa kufanya chochote.

Tunaomba Dunia ifahamu kuwa Wananchi waliochuku fedha wamefanya hivyo kwa kuwa wanahofia usalama wao na ambao hawajachukua hatujui nini kitawatokea kwa kuwa mradi haujaanza na kunaonekana kuna mazingira flani ya ‘udalali’.
Mkikubali huu upuuzi nitawashangaa sana.

Kima cha chini square meter wawalipe Kwa sh 10,000/= per square meter au watumie bei elekezi ya wizara ya Ardhi
 
KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika. Ila ingekua kutengeneza MOVIE hapo chapu angekuja location
Atakuwa na muda Vipi na Watanganyika kazi mnayoiweza ni uchawa Tu.

Juzi kidume mizima inasema CCM ichapishe fomu moja ya mgombea Urais, ukiwauliza katiba ya CCM inasema hivyo wanakwambia ni utamaduni.

Stupid (In Samia voice.)
 
Bei elekezi ya Wizara ya ardhi ni kiasi gani kwa square meter mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maeneo hayo haipungui sh 9000 per square meter tena bei ya zamani miaka 7 iliyopita, sijui Kwa sasa.

Msiwe makondoo, muoneni waziri wa Ardhi ingawa ni jingajinga fulani Tu nalo lakini anaweza kufanya Jambo.

Tena nadhani yupo jimboni kwake Jana amezomewa huko Ukonga mtafuteni.
 
Kulalamika mnajua vizuri linapo kuja susla la kupiga kura kutafuta viongozi wa takao wajibika, mkipewa kanga na sabuni mnaanza kuiba nyimbo za kupamba chama, wengine hata kuhoji biongozi hamwezi kwahiyo msilalamike sasa hivi plz.
Si ajabu ukakuta ni kada wa ccm kindaki ndaki

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwa maeneo hayo haipungui sh 9000 per square meter tena bei ya zamani miaka 7 iliyopita, sijui Kwa sasa.

Msiwe makondoo, muoneni waziri wa Ardhi ingawa ni jingajinga fulani Tu nalo lakini anaweza kufanya Jambo.

Tena nadhani yupo jimboni kwake Jana amezomewa huko Ukonga mtafuteni.
Walifanya vizuri sana kulizomea tena mbele ya waziri mwenzake
 
Mbona nchi yote ishadalaliwa tu? Watanganyika tusubiri kuuzwa tu kwa ukimya, ujinga na ukondoo wetu!

Kwa hali ya sasa hivi ilivyo kimaisha, usingetegemea mtu hata mmoja akisema CCM oyeee; lakini hebu nenda mikutano ya CCM, utadhani waTZ aliyeturoga siyo tu kafa, bali hata kaburi lake halipo, lilishachukuliwa na tsunami!
 
Back
Top Bottom