Chikuvi2021
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 459
- 516
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2020/2021 ilikuja na wazo zuri la urasimishaji wa Makazi Holela kwenye Majiji na miji mbalimbali. Wananchi wengi walijenga nyumba kwenye mashamba yao au viwanja ambavyo havijapimwa Al maarufu (squarter) Mradi wa MKURABITA.
Kwenye jiji la Dar es Salaam maeneo Kama Vituka, Buza, Vingunguti, Mbagala nk Ni miongoni mwa maeneo hayo.
Madhumuni ya MKURABITA ilikuwa kuwawezesha wananchi kupata hati za umiliki wa makazi yao na hizo hati zinaweza kutumika kama Colleteral (dhamana) ya kuomba mkopo kwenye taasisi za fedha.
Wananchi walitakiwa kulipa shs150,000 kwa ajili ya zoezi la upimaji, uchoraji wa ramani na uwekaji wa Beacon.
Fedha hizo zilitakiwa kulipwa kwa awamu moja au awamu tatu. Baada ya kulipa shs150,000 ilitakiwa makumpuni yalifanya zoezi la urasimishaji, wawasilishe ramani na michoro wizara ya Ardhi nyumba na Makazi kwa ajili ya kuandaa hati za nyumba ( baada ya masharti na vigezo vya kutoa hati kutimizwa, na Wamiliki kulipa gharama za kuandaa hati,kodi ardhi,ushuru nk).
Serikali za mitaa ziliunda kamati za urasimishaji Makazi Holela kwenye mitaa yao. Kamati zilifungua akaunti maalum kwa ajili ya zoezi hilo na wananchi walitakiwa ku-deposit fedha kwenye akaunti hizo na kupeleka stakabadhi kwenye ofisi za Serikali za mitaa kwa ajili ya kupewa stakabadhi na kumbukumbu.
Aidha kamati ziliajiri Makampuni ya watu binafsi kufanya survey na uwekaji wa mawe/beacon.
Mwezi uliopita nilitembelea ndugu zangu Mtaa wa Sigara na Vituka, nikaona wamewekewa mawe(beacon).
Katika kuongea nao, wakasema wao walilipa Shs 150,000 kwenye akaunti ya urasimishaji Makazi Holela Mtaa wa Sigara na Vituka 24/03/2021 na wameshawekewa beacon. Lakini kila wanapofuatilia hati zao, wanaambiwa Wanakamati na Kampuni iliyopewa zabuni ya upimaji na kuweka beaconwameingia mitini.
Hii ni ishara kuwa wananchi hawa wameshatapeliwa na viongozi wao wa Serikali za mitaa kwa kushirikiana na hayo makampuni binafsi.
Wananchi walikuwa wana Imani na Serikali zao za mitaa walipoambiwa kuwa fedha zenu weka kwenye bank account waliona wako salama, kumbe wajanja wamekwenda benki kuchukua fedha zote na kupeleka kwenye matumizi mengine.
Wito kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dr Angelina Mabula kufuatilia na kiungulia kati suala hili usisubiri mpaka Rais Dr Samia H.Suluhu atembelee wananchi, ndiyo waibue malalamiko hayo.
Wananchi ambao wamekamilisha malipo yote waandaliwe hati miliki zao, linatia doa wizara yako.
Kwa kufanya hivyo kwanza, Serikali itaongeza mapato ya Kodi ya ardhi ambayo baadhi ya Wamiliki hawalipi kwa hivi sasa.
Pili, kwa wale ambao hawajamaliza kulipa instalments zao,na wao watahamasika kukamilisha malipo ,ili wapatiwe hati.
Tatu, wananchi wengi,watatumia hati hizo kuchukua mikopo kwa ajili ya maendeleo.
Ninawasilisha.