Mradi wa Viwanja vipya - Kinyerezi

Jana na leo magazeti yamekuwa ya kitangaza kuanza mpango wa kuuza viwanja vya Tabata Kinyerezi!

Lakini cha kushgangaza ni hizo bei! Hakika mtanzania wa kawaida kiwanja kilicho pimwa atakisikia kwenye bomba maana bei ya kiwanja cha makazi ni shs 10,000 kwa sqm moja, makazi na biashara shs 15,000, Biashara shs 20,000, Ibada shs 8,000 na waliokuwa na nyumba kabla ya mradi ni shs 5,000!

Yako wapi maisha bora kwa kila Mtanzania? Niwazi viwanja hivi vitachukuliwa na Mafisadi wenye pesa ndefu.

Kibaya zaidi watu waliochukuliwa maeneo yao hawajalipwa! Lakini viwanja sasa vinauzwa!

Habari za uhakika kutoka Manispaa ya Ilala, nikwamba Selikari haina pesa za kulipa fidia hivyo Basi wanauza viwanja ili waweze kulipa fidia, kama si unyonyaji ni nini sasa!

Wapi wanasiasa akina Nape na wenzake walioko madarakani? Je haya mnayaona? Au mnakalia ufisadi wa Slaa? Hima hima wana Kinyerezi haki yenu inapotea, na hakuna wa kuwasaidia, serikali imefilisika!

Huwezi kusema gharama za viwanja zinafidia gharama za upima na miundo mbinu wakati miundo mbinu yenyewe hatuioni.

Nguvu ya Umma Iko wapi!

Mungu Ibariki Tanzani

habari ndo hiyo jamani.si lazima wote tule nyama!!!!wengine mandondo, wengine kauzu na wengine twala kuku!ndo maisha ya bongo.wengine tutaishia nyumba za kupanga hadi mwisho wa maisha yetu, Mungu tusaidie!!

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom