Mradi wa Viwanja vipya - Kinyerezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa Viwanja vipya - Kinyerezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutwale, May 17, 2011.

 1. Mutwale

  Mutwale Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana na leo magazeti yamekuwa ya kitangaza kuanza mpango wa kuuza viwanja vya Tabata Kinyerezi!
  Lakini cha kushgangaza ni hizo bei! Hakika mtanzania wa kawaida kiwanja kilicho pimwa atakisikia kwenye bomba maana bei ya kiwanja cha makazi ni shs 10,000 kwa sqm moja, makazi na biashara shs 15,000, Biashara shs 20,000, Ibada shs 8,000 na waliokuwa na nyumba kabla ya mradi ni shs 5,000!

  Yako wapi maisha bora kwa kila Mtanzania? Niwazi viwanja hivi vitachukuliwa na Mafisadi wenye pesa ndefu.

  Kibaya zaidi watu waliochukuliwa maeneo yao hawajalipwa! Lakini viwanja sasa vinauzwa!

  Habari za uhakika kutoka Manispaa ya Ilala, nikwamba Selikari haina pesa za kulipa fidia hivyo Basi wanauza viwanja ili waweze kulipa fidia, kama si unyonyaji ni nini sasa!

  Wapi wanasiasa akina Nape na wenzake walioko madarakani? Je haya mnayaona? Au mnakalia ufisadi wa Slaa? Hima hima wana Kinyerezi haki yenu inapotea, na hakuna wa kuwasaidia, serikali imefilisika!

  Huwezi kusema gharama za viwanja zinafidia gharama za upima na miundo mbinu wakati miundo mbinu yenyewe hatuioni.

  Nguvu ya Umma Iko wapi!

  Mungu Ibariki Tanzani
   
 2. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni kinyerezi ipi? kinyerezi kubwa!
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ni typing erro walitaka kumaanisha bei ya kiwanja cha makazi ni shs 1000 kwa sqm moja, makazi na biashara shs 1500, Biashara shs 2000, Ibada shs 800 na waliokuwa na nyumba kabla ya mradi ni shs 500!
   
 4. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Gazeti gani limetangaza?
   
 5. Mutwale

  Mutwale Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sio amini bei tajwa watafute gazeti la Mtanzania au Mwananchi la jana au wafike office za manispaa ya Ilala, mabango kila mahali! Hakuna typing errors! That are the price! Na hii ni Kinyerezi Kifulu! Mpo hapo wana janvi?
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kaka mimi nimesoma gazeti la Mtanzania jana sikuamini. Nikapiga simu mahala nikaambiwa habari ndiyo hiyo. Yaani ukitaka kiwanja cha 25mx22m = 550m2 (high density) unatakiwa utoe Tshs. 5,500,000.00 tena within 2 weeks. Jamani nani anaweza kupata hizo pesa na kulipa. Mfanyakazi gani atapata kiwanja cha bei hizi? Serikali naona sasa inachezea maisha ya watu. Kama hali ni hiyo kwa nini watu wasijenge mabondeni na kwenye hifadhi za barabara?

  Wanasema unatakiwa urudishe gharama za miundombinu wakati hakuna miundombinu ni vichaka vitupu kule kinyerezi - Kifuru. Jamani jamani serikali hii naona imetuchoka sasa.
   
 7. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Nimeliona tangazo la uuzwaji wa viwanja kinyerezi kwenye mtanzania la tarehe 16/05/2011. Lakini kwa taarifa nilizokuwa nazo hivi viwanja vilikuwa na mgogoro mkubwa sana, ambao ninafikiri umeshakwisha. Swali langu ...serikali kuwauzia wananchi viwanja kwa bei kubwa (1 sqm = tshs 10,000/=) inawajali au inawakebehi? kwasababu kiwanja cha kawaida 40 * 30 au tuseme sqm 1200 utakipata kwa tshs 10,000 * 1200 ambayo ni 12,000,000/= huu sio ufisadi uliokubuhu jamani? Tena hela zenyewe zilipwe ndani ya siku 14. Kweli hii ni haki? Huu ni utawala bora? Najua kuna watu wenye uwezo zaidi ya huo lakini lengo si kumuwezesha mwananchi wa kawaida awe na makazi bora? Sera zetu za ardhi na makazi ndio zinataka hivi kweli? Halafu ukishabikia chadema unaonekana mtomvu......kwa style hii tutafika kweli?
   
 8. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Wizi Mtupu !
  Labda wenye hela za kifisadi; sasa kama ni afisa tu wa kawaida ukitaka kakiwanja ka low density si ndio utakoma kabisa na hiyo bei !
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nania alikuambia kuna maisha bora??? na nani alisema serikali itapanga bei hata kwa ardhi binafsi??? wameshindwa sukari wataweza ardhi?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ukisusa wenzako twala ati'
   
 11. zagalo

  zagalo Senior Member

  #11
  May 17, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huu ni wizi
   
 12. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutake tusitake bado mwenye nacho ataendelea kuwa nacho na hata kujilimbikizia maradufu.Kwa serikari hii tuliyo nayo sasa, chini ya chama hiki cha magamba sijui kama sisi Wtz wa hali ya chini tutamudu huu ugumu wa maisha,maana ninapata wasiwasi ipo siku mtu hatashindwa kulipia hata chumba cha kupanga kwa kila senti anayoipata kuikimbizia kwenye kuliudumia tumbo lake na familia yake.Sasa cha kufanya hapa ni kuwa active kuhakikisha ccm hairudi madarakani maana sera zake si za kumjari mtu wa hali ya chini.
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  serikali yenyewe ndio inayofanya mfumuko wa bei kuwa juu!maana mwaka jana ilikua 8500 per sqm,leo 10 000.sidhani kama kuna mwenyeji wa kifuru ataweza kununua kiwanja!
   
 14. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  nakubaliana nawe, huo ni wizi. Serikali inatakiwa kutoa huduma sio kufanya biashara. Anyway, hii ndio serikali ya mafisdi...cha moto tutakiona.
   
 15. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Makazi bora kwa jamii za Watanzania ni ndoto,tutegemee muendelezo wa ujenzi holela na makazi holela hadi mwisho wa dunia.kutegemea Mtanzania kumudu kulipa 10m kwa plot is a day dream unless Watanzania wote ni watoto wa Vigogo tena mafisadi!!! Kwa mfumo huu,Prof Tibaijuka utapwaya sana kwenye wizara ya ardhi.
   
 16. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jumatatu nimesoma gazeti la mtanzania kwamba kuna viwanja 20,000 vimepimwa kinyerezi na form zitaanza kutolewa kuanzia kesho tarehe 19 may,square meter 1 ni tsh 10,000/= kwa hiyo ina maana mtu akitaka kiwanja cha 30m kwa30m anatakiwa kuwa kutoa milion 9 na ni ndani ya siku saba sasa jamani hivi hii manispaa ya ilala inataka mafisadi tuu ndio wawe na viwanja au wamemwangalia na mtanzania wa hali ya chini? Garama ya square meter moja kuuzwa 10,000/= hii si sahihi kabisa .haya maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana
  naomba kuwasilisha
   
 17. k

  kinyongarangi Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bei hiyo ni kubwa mno na lengo lao nadhani ni kuwauzia mafisadi wenzao. Ni raia gani wa kawaida au mfanyakazi mwaminifu anayeweza kununua kiwanja kwa 9000000 ndani ya siku saba???.
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na unajiuliza kama kweli walengwa wa mpango huu ni watanzania, maana kipato cha watanzania kinafahamika. Huu ni mpango wa kuwafungia milango wenye shida ya viwanja kweli na kuwaachia wale wenye tabia ya kuhodhi. Kama mtu anatakiwa kulipa milioni 9 katika wiki 1 kabla hata hajajua bei ya tofali au trip ya mchanga basi huyo si mtanzania wa kawaida. Je watanzania elfu 20 wa kipato hicho wanatoka sekta gani? Hivi ni lini watu watafaidika na rasilimali zao ndani ya nchi yao? Wanataka ku-achieve nini na wanalenga watu gani?
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi kabisa maana naambiwa hata kule kigamboni, fisadi mmoja kwa kupitia mtoto wake anamiliki viwanja 40 vy mradi. Ni hao tu ndiyo wanaoweza kumudu na ni wazi wangewaambia knaga ubaga watanzania kwamba hii ni toleo maalum kwa watu wasio waadilifu.
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Dawa ni kuvivamia kabla havijauzwa na kujenga......
   
Loading...