Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
4,330
Points
2,000

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
4,330 2,000
Malila huu mpango wa kufuga ng'ombe wa nyama na mimi ninao kilichobaki sasa hivi nikuanza utekelezaji tu by 2013 nadhani mradi utakuwa hewani.. lakini mimi nafikiria kufuga ng'ombe wa nyama wa kisasa.. niliona kwa bwama ASAS aisee ng'ombe anakwenda mpaka kg 1000 within a year baada ya castration. ASAS anaimport mbegu kutoka Denmark na kuzihifadhi kwenye vacuum tanks na alisema pia anaziuza kwa wafugaji wengine.
Hawa wakienyeji tatizo ukuaji wake kidogo unachukua muda mrefu lakini kama utapenda unaweza kupata mbegu nzuri ya ng'ombe wakubwa kutoka kanda ya ziwa i.e shinyanga
Hizo ni mbegu za ng'ombe wa nyama au wa maziwa?
Utaalamu wa kupandisha ng'ombe kwa chupa (AI) ni mdogo sana
Mi nafuga na lastly niliamua kununua dume
 

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
4,330
Points
2,000

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
4,330 2,000
Kuna Aiana Fulani ya Ngo'ombe wako Kenya,wanatoa lita 40 kwa siku, ila kuwatoa kule si kazi ya kitoto,
Hiki kitu tatizo ni wizara ya mifugo na kilimo wana tatizo hapa kwetu.
Yaan ninafuatilia nataka kununua dume moja la ng'ombe kwenye ranch fulani IPO Kenya nataka niboreshe shamba langu.
Vibali ni mgogoro usiopimika. Ila sekta ya mifugo bila kuwa na breed za kibiashara utachemka.

Maana kwenye ufugaji wa ng'ombe kuna fursa kubwa tatu; maziwa, nyama na kama ukiwa na breed nzuri ni Ujazaji wa Mitamba (hii ndio inalipa ingawa ni uwekezaji mrefu). Hii sekta inakuwa sana ingawa serikali haijaweza kutenga hata maeneo ya wafugaji wadogo au wa kati hasa wale wa zero grazing.

Nenda kwa watu wa Mipango miji angalia master plan zao hawaoneshi kabisa kuwa labda hapa wafugaji madogo au eneo la wafugaji wa kati hivi wanaweza kufugia hanna wao ni makazi biashara na fremu tu.

Mi nilinunua shamba kwa madhumuni hayo, wamekuja kupima vimetoka viwanja vya makazi 39 na mibarabara kibao kwahiyo hata sielewi nafanyaje.

Hii sekta ukiitolea macho vizuri inakutoa kwakuwa kila uchao matumizi ya mazao yapatikanayo kwa mifugo ni yanahitajika hasa nyama na maziwa

Asante
 

Attachments:

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
4,330
Points
2,000

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
4,330 2,000
Nilisikia South Africa wanauza ng'ombe dume wa fleckvieh anauza $ 15,000 ambayo ni sawa na kama Tshs 35,000,000 za kitanzania. Wale ng'ombe ni dual purpose na wanaimili sana maisha ya baridi kali na Joto kali pia na ulaji wao sio mkubwa
Hii bei inazidi vitoyota rush au vanguard zinazosumbua hapa mjini
 

khashdz

Member
Joined
Jul 14, 2011
Messages
28
Points
45

khashdz

Member
Joined Jul 14, 2011
28 45
Nina tatizo Kama lako la Aina hiyo ya ngombe kutoa maziwa kidogo na katika kudadisi kwangu nikaambiwa kadri atakavyokuwa ana zaa maziwa yatakuwa yakiongezeka ,Sasa ana mimba miezi sita nangoja nione

Pili nimembiwa ngombe akiwa na kiwele kikubwa anatoa maziwa mengi sijui Ni Kweli...
Kwa uzoefu wangu naamini ng'ombe mwenye kiwele kikubwa na chuchu kubwa nakuwa na asilia nyingi za kutoa maziwa mengi.
 

khashdz

Member
Joined
Jul 14, 2011
Messages
28
Points
45

khashdz

Member
Joined Jul 14, 2011
28 45
AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA

Kuna aina nyingi za ng’ombe wa maziwa ambao hutofautishwa kwa sifa zifuatazo;

-Umbo, mahali alipotokea.
-Rangi ya ngozi
-Uzalishaji wa maziwa nk.

Zaidi kabisa kuna aina kuu mbili ambazo ni; “Bos taurus” na “Bos indicus”.

Bos taurus inahusisha: Friesian, Ayrshire, Brown Swiss, Guernsey and Jersey na wengine wengi kama vile (Red Dane, Swedish Red and White, Holstein Friesian nk.)

Bos indicus inahusisha: Sahiwal, Red Sindhi, Kenana, Criolo, Tharpakar nk.

1. FRIESIAN/FRESHIANI

-Asilia yao ni holand.

-Hutambuliwa kwa kuwa na rangi nyeupe na nyeusi.

-Uzalishaji bora wa maziwa (7800l/mwaka).

-Walikuwa maalum kwa ajili ya kutengenezea “cheese”.

2. AYRSHIRES

-Wanatambuliwa kwa kuwa ana rangi nyekundu na nyeupe.

-Wanatoa maziwa yenye wastani wa fati 4%.

-Huzalisha maziwa yenye fati nyingi (5400l/mwaka).

3. JERSEYS

-Asili yao ni visiwa vya jersey katikati ya Uingereza na Ufaransa.

-Wanatambuliwa kwa kuwa na rangi mtambuka wa nyeusi na kahawia.

-Maziwa 5700l/mwaka.

-Maalum kwa ajili ya utengenezaji wa “butter”.

KUHUSU UNUNUZI WA HEIFER/MTAMBA.

Siku zote hatushauri mfugaji atafute mtamba mbadala kwa sababu zifuatazo;

-Hawapatikani kwa urahisi na kama wakipatikana ni ghali sana.

-Hatari ya kuingiza magonjwa shambani kwako.

-Ugumu wa kufuatilia historia ya wazazi.

-Hakuna mfugaji anaeweza kuuza mtamba wake bora.

JE WAJUA Kila mwaka ng’ombe wengi wa maziwa wanaondolewa katika shamba kwa sababu mbalimbali ???

Zifuatazo ni sababu kuu;

-Uzalishaji mdogo wa maziwa

-Magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza (TB).

-Matatizo ya uzazi

-Kuuzwa au kuchinjwa tu bila sababu maalum.

HIVYO USHAURI NI KWAMBA, SI KILA MTAMBA UNAOUZWA NI BORA HIVYO ZINGATIA SANA KUOMBA TAARIFA NA KUMBUKUMBU ZA MTAMBA PINDI PALE UTAKAPO ENDA KUNUNUA MTAMBA.

Kuhusu upatikanaji wake kwa huko songea sijafahamu ila Njombe kuna shamba moja kubwa la serikali lipo maeneo ya kitulo pale utapata mtamba mzuri kwa bei nzuri..
Thanx mkuu, nimepata madini adimu, kama hautojali weka namba ya simu utusaidie zaidi.
 

Forum statistics

Threads 1,343,290
Members 515,003
Posts 32,779,210
Top