Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by day 24, Feb 27, 2012.

 1. d

  day 24 Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanajamii,
  kama kuna mtu anafaham juu ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa naomba tushee utaalam ili nijue faida ya biashara hiyona hasara ya na vitu vinavyotakiwa kuanzia wanapopatikana hao ng'ombe na bei wanazouzia,soko la maziwa na tahadhari zake...naomba msaada wenu tafadhari   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili suala, limeshajadiliwa sana hapa, hivyo ingekuwa ni busara kama ungepitia post za nyuma zinazoelezea suala hili hili kwani zitakuwa na msaada kwako na tutaokoa ujazo kwenye server za JF. Unaweza ukazipata hapa chini

  1. [FONT=&amp]ngombe wa maziwa[/FONT]
  2. [FONT=&amp]natafuta ngombe ankole type[/FONT]
  3. [FONT=&amp]kwa wanaopenda ufugaji mkubwa[/FONT]
  4. [FONT=&amp]naomba ushauri kufuga ng'ombe[/FONT][FONT=&amp] wa maziwa na kupack maziwa[/FONT]

  Pia kuna hili andiko la FARM AFRIKA linalihusiana na ufugaji bora wa ngombe wa asili. Tafadhali lipitie
   

  Attached Files:

 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nilipita mitaa ya Nadanya huko umasaini, nikaona kundi kubwa la ndama mchanganyiko, wakubwa na wadogo. Nikashawishika kuuliza bei. Bei inacheza kati ya laki tatu mpaka laki nne.

  Nikasema moyoni, nikiwanunua kumi hawa ndama madume, kisha niwahasi. Baada ya mwaka mmoja ninaweza pata ada ya watoto bila taabu. Kwa sasa dume mmoja mzuri pale Dar anaweza fika milioni moja bila udalali. Kwa wenye maeneo ya kufugia madume yaliyohasiwa hii ni biashara nzuri.
   
 4. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  nakukubali sana mkuu!
  Hivi nikitaka kumiliki hayo madume 200 natakiwa kua na eneo la ukubwa gani?na bei ya kuasi dume 1 ni bei gani?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  DSM ufugaji mkubwa hauruhusiwi, labda mhamie MTWARA ndo mkafugie kule
   
 6. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Vp chalinze hapafai?
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Malila!

  Juzi mnadani pale Wilayani Monduli,Dume mmoja kt ya madume walioletwa pale mnadani hakika aliuzwa Tsh. 1,100,000/= na wale wengine walilamba 1M na hata wale wa size ya kati ni laki 8 mwisho.

  Ndio kweli nikakubalia na msemo huu

  "KIZURI KINAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA"

  Yule Dume alikuwa hakosi kg 420 na hadi 50.
  Ufugaji dili Kamanda!
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Chalinze panafaa sana mkuu. Kwa sababu hiyo Nadanya iko Chalinze huko huko. Kibaha kuna njia inakwenda B/moyo, kuna jamaa ana shamba zuri la ng`ombe la kufa mtu.
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nimesahau kidogo, ukubwa wa eneo kwa ng`ombe mmoja. LAT akiiona hii maada atatoa jibu na pia anaweza kutoa gharama za kuhasia ng`ombe.
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wakuu naomba kuuliza swali. Ng'ombe dume anahasiwa ili iweje? Mimi nilidhani ananunuliwa ili azalishe?
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Si kila dume linafaa kwa mbegu, kumbuka dume moja laweza kuhudumia majike mpaka 250 kwa mwaka kama litatumika kitalaamu ( kama sijakosea). Pili dume likihasiwa ( ng`ombe, mbuzi nk) linakuwa haraka na kunenepa sana ktk muda mfupi. Kwa njia hii mkulima anaweza kupata faida haraka. Tunahitaji majike zaidi kuliko madume ktk ufugaji, hata kuku, jogoo ni mmoja kwa matetea matano.
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Shukrani sana mkuu,ngoja nimsubili LAT.
  Pia kuna thread yangu nimeiweka hapa kwenye ujasiriamali inahusu"kufungua duka la mboga na matunda"naomba mawazo yako pale mkuu.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ngoja niipitie, kama ninalo la kuchangia nitatoa.
   
 14. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Imeandikwa hivi"msaada kuhusu kuanzisha biashara ya matunda na mboga mboga"
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Malila huu mpango wa kufuga ng'ombe wa nyama na mimi ninao kilichobaki sasa hivi nikuanza utekelezaji tu by 2013 nadhani mradi utakuwa hewani.. lakini mimi nafikiria kufuga ng'ombe wa nyama wa kisasa.. niliona kwa bwama ASAS aisee ng'ombe anakwenda mpaka kg 1000 within a year baada ya castration. ASAS anaimport mbegu kutoka Denmark na kuzihifadhi kwenye vacuum tanks na alisema pia anaziuza kwa wafugaji wengine.
  Hawa wakienyeji tatizo ukuaji wake kidogo unachukua muda mrefu lakini kama utapenda unaweza kupata mbegu nzuri ya ng'ombe wakubwa kutoka kanda ya ziwa i.e shinyanga
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Heko Kamanda!
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa wa kienyeji wanachelewa, lakini kuna hawa chotara. Mwezi jana nilifanikiwa kumpata mkulima mmoja na aliniuzia dume chotara kwa laki 3 na nusu. Nakubaliana na ww kabisa,lazima kuwa na mbegu kubwa.Kilichobaki kwangu ni kujenga zizi la kisasa ili niwaongeze wengine. Tafadhali,ukifanikiwa kupata mbegu kubwa nishitue.
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu hii hapa chini ni appraisal ya mradi wa ng,ombe wa maziwa nadhani unaweza kupata point chache hapa .... nilifanyiwa na jamaa wataalam wapo india ingawa sijaanza hii project

   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  sawa hamna shida nikiwapata ambao hawajachezewa nitakutaarifu. Inatakiwa ucheze vizuri sana na msimu wa njaa, kwenye minada kule mpwapwa kipindi cha njaa unapata ng'o,mbe mkubwa kati ya 60-200,000/=, mbuzi anacheza kati ya 10-20,000/= january na feb njaa inazidi kupamba moto na bei inazidi kuporomoka.. march katikati karanga na mahindi ya kwanza yanaanza kukomaa na kidogo hapa bei inapanda, april mazao yote yanakuwa yamekomaa na bei inazidi kuongezeka... june..july..august-november mahindi, mtama vinasagwa and so ugali mwingi, hapa bei haikamatiki.. wauzaji wanaringa vibaya sana.
  Wanyama wazuri utawapata kati ya janu-april, miezi ya june-november wanyama waliopo sokoni ni wale wenye matatizo.

  Ukicheza vizuri kisomi na huu msimu wa njaa utatoka mapema sana na hautakuwa na haja ya kusubiri ng'ombe azae mtoto mmoja, kumkuza kwa miaka 4 na kuja kumuuza kwa 1-1.5m. Simply utanunua ndama wa miaka 2 unamkuza kwa mwaka 1.5 unamuingiza sokoni au unanunua wakubwa unawalisha vizuri kisasa wakifikia uzito wa maana wanaingia sokoni

  NB: Miaka ya nyuma tulikuwa tunabadili ng'ombe huko vijijini, tulikuwa tunapeleka dume moja la kisasa, wanatupa ng'ombe mpaka 10 wa kienyeji wale wakubwa
   
 20. a

  anonimuz Senior Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mambo vipi wakuu. Ninaomba anayefahamu minada ya mbuzi katika mikoa ya jirani especially Tanga, Morogoro (?), na Dodoma hasa siku za Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili anifahamishe please. Kama una information nyingine yeyote kuhusu hili ambayo unadhani inaweza kusaidia unaweza kuchangia. Suggested Format: Mkoa-> Kijiji-> Siku-> Extra info (e.g. range ya bei, quality ya mbuzi, gharama za kusafirisha etc). Asanteni sana.

  *On a second thought, nimeona kwamba watu wengine wanaweza kuwa interested na minada hiyo katika mikoa mingine na siku zingine. So, feel free to share the info regardless of the day and the region.
   
Loading...