Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,342
- 24,233
Mradi wa Maji huko Arusha unaelezea madudu yote yanayofanywa na serikali na wachina wanaowapendelea sana kuwapa tenda.
Isingekuwa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni, ingekuwa kama waswahili wanavyosema, "imeenda hiyo"
Siyo siri, wachina kwa rushwa ili kupata kazi, hawajambo.
Watendaji serikalini wanajua wakimpa kazi mchina, bahasha nzito zinafuata.
Sasa wengi wamekuwa mateja kwa rushwa.
TAKUKURU wanalijua hilo.
Na mtendaji akisha kuwa teja la rushwa mchina anafanya madudu yote tu kule site, na hachukuliwi hatua yoyote.
Sasa ile mvua ya Arusha imewaumbua.
Mchina kachimba barabara na kuweka mbomba, hakushindiloa kijandisi na kurudishia layer za udongo na kifusi sahihi. Yeye kafunika funika, na akalipwa raha mustarehe.
Consultant yupo, Engineer yupo, na Client mwenyekazi yupo na suti zake ofisini.
Hali hii imelalamikiwa na makandarasi wazalendo kwa miaka mingi, lakini utamu wa rushwa unaziba masikio.
Katika mradi huu wa Maji Arusha, wengi wanaingia kwenye kapu la rushwa na kutosimamia kazi.
Idara ya Maji yenyewe, TARURA na hata idara za Mkoa kusimamia kazi, ni wahusika.
Halafu mbaya zaidi serikali yenyewe ati inashangaa madudu hayo inayoyalea.
Serikali ilitegemea nini haswa na hao wachina.