Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.

Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana

Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha

Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu

Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane

Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee

Cc Wizara ya Afya Tanzania


Asante TANESCO kwa majibu mazuri ya mipango ya kupambana na shida ya umeme ya muda mfupi na muda mrefu.
Sisi wananchi tunafarijika sana mnaposikia sauti zetu na kutujibu kama hivi
Ila sasa mjitahidi kwenda na hiyo mipango kwa wakati ili mwakani muda kama huu kukawa na tatizo hilihili na majibu yakawa hayahaya

Plan nzuri bila utekelezaji makini na kwa wakati inakua mbaya zaidi kwa wananchi waliokua na subra, Rais amewaamini abajua nyie ni wataalamu mnaoweza kumsaidia kuwahudumia watu wake. Basi msiipoteze imani ya watanzania kwa serikali yao

Tanesco Kazi iendelee 👍

07 Septemba 2022

Ni kweli kumekuwepo uhaba wa mvua uliojitokeza kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwenye miezi ya hivi karibuni, uhaba huu umesababisha kuwepo kwa upungufu wa kina cha maji kwenye mabwawa ya kufua umeme kwa kutumia maji hivyo kuathiri hali ya uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vyanzo vinavyotumia maji.

Aidha, ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma ya umeme inaimarishwa nchini, Shirika limeshachukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kama ifuatavyo;

Mipango ya muda mfupi

Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Ubungo III ambacho kimeshakamilika na kuingiza jumla ya Megawati 112 za umeme kwenye Gridi ya Taifa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi asilia cha Kinyerezi I Extension kitakachozalisha jumla ya megawati 185.

Tayari megawati 45 zimeshaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na megawati zilizobakia zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.

Mradi wa kufua umeme wa Rusumo kwa kutumia maji.
Mradi huu unaozihusisha nchi tatu (Tanzania, Rwanda na Burundi) utakapokamilika, unategemewa kufua jumla ya megawati 80 za umeme, ambapo kwa upande wa Tanzania, tutapata megawati 27 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua wa Kishapu, Shinyanga.
Mradi huu unategemewa kuanza ujenzi wake Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2023, utaingiza jumla ya megawati 150 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

Mradi wa kupeleka Gridi ya Taifa kwenye wilaya za mkoa wa Kigoma.
Tayari umeme wa Gridi ya Taifa umeshapelekwa kwenye wilaya ya Kibondo.
Serikali imeanza kuokoa jumla ya Tsh.9.44 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununulia mafuta ya dizeli na kutengeneza mitambo (jenereta).
Mpango uliopo ni kuufikisha umme wa Gridi ya Taifa kwenye Wilaya ya Kasulu hadi Kigoma mjini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2022 kufika.

Mipango ya muda mrefu

Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Mradi huu umefikia asilimia 71 ya utekelezaji wake.
Mradi utakapokamilika mnamo mwezi Juni 2024, unategemewa kuingiza megawati 2115 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

Kwa hatua hizi Shirika ilizozichuka zimesaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na iwapo jitihada hizi zisingechukuliwa, basi ya upatikanaji umeme nchini kwa sasa ingekuwa ipo vibaya zaidi.
 
Hujuma dhidi ya Samia zimekuwa nyingi tena ni haohao Wanaccm wenzake wameanza kampeni.
Acheni USANII nyie wababaishaji tu hamna lolote.

Taasisi zote ziko chini ya Rais na serikali yake! Kama kweli anahujumiwa kwanini asiwawajibishe hao wahujumu?

Urongo mtupu! Mwambieni ukweli huyo mama kwamba hajiwezi, acheni kulaghai watu eti anahujumiwa!

Anajihujumu mwenyewe na udhaifu wake!
 
Huyo mama yenu kila siku yeye anahujumiwa tu!!

Hawezi kubeba majukumu ya Urais na kutenda kazi inavyompasa...
Hii comment sio ya kupuuza, hii ndio picha wanayopewa watanzania kuhusu serikali yao, na ujumbe uwafikie
#WaziriMwenyeDhamanaYaUmeme
#WaziriMwenyeDhamanaYaMaji
#IdaraZoteZinazohusika

Sisi wananchi tunasema mama yetu Samia anza kuwashughulika wote wanaoshindwa kuhudumia wananchi. Tumbua mama uteue walio tayari kufanya kazi usiku na mchana kuondoa hizi kero ndogondogo kwa wananchi
 
Back
Top Bottom