Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,313
- 24,171
Kama kuna Wizara ngumu kwa makandarasi nchi hii, basi ni Wizara Ya Maji.
Wizara hii haijielewi katika fani ya ujenzi.
Matatizo waliyonayo wizara hii ni tofauti kabisa na wizara nyingine.
Ni ukweli usiopingika kuwa Makandarasi wabobezi na wanaojielewa hawachukui kazi za Wizara ya Maji.
Ukitaka kupigwa Tanganyika Jacki na mwanasiasa basi unachukua kazi za Wizara hii.
Wizara ya Maji kuna uozo mwingi sana katika procurement za miradi yake ya Ujenzi.
Miradi mingi haina design(usanifu) za kina.
Miradi mingi ya Maji haina fedha za miradi na zikiwepo hazifiki kwa walengwa.
Sababu rahisi za kujieleza kwenye uso wa umma ni kuwalaumu makandarasi!
Hatuoni tarumbeta hizo na visingizio kwenye miradi inayotekelezwa kwenye wizara zinazojielewa kama Wizara ya Ujenzi na TANROADS.
Wizara ya Maji imelalamikiwa sana juu ya very poor Project Management katika idara ake zote, ile kumlaumi mkandarasi kwa kiasi fulani kinaeleza kushindwa kwa mwenye mradi(Wizara ya Maji) kwa ujumla.
Mtu usipojua kuendesha baiskeli, na inakuangusha kila mara, njia rahisi kujieleza ni kusema baiskeli ni mbovu.
Lakini kiuhalisia wengine wanaendesha baiskeli hiyo kwa weledi tu, haiwaangushi, tatizo ni kukubali kuwa hujui kuendesha baiskeli!
Ndiyo wizara yetu ya Maji
Sasa tukiona magazetini, hasa gazeti la serikali Daily News, ati Msemaji wa Serikali naye anaingia mkumbo wa kutoelewa kiini cha tatizo, ndo lile lile linaitwa passing the buck!
Dkt. Abbas changa la macho hilo!!