Mr. President... Please don't do it. tomorrow..

Mimi nadhani wote mnamshauri Rais wetu vibaya , Mimi namshauri ajuizulu kwenye hiko cheo cha AU mara moja . Kama mtu ameshindwa kutatua matatizo ya nchi yake ataweza matatizo ya afrika ?

Let us be serious ...nchi yetu inakufa , mafisadi kila kona nyie mnazungumzia Zimbabwe .
 
Mimi nadhani wote mnamshauri Rais wetu vibaya , Mimi namshauri ajuizulu kwenye hiko cheo cha AU mara moja . Kama mtu ameshindwa kutatua matatizo ya nchi yake ataweza matatizo ya afrika ?

Let us be serious ...nchi yetu inakufa , mafisadi kila kona nyie mnazungumzia Zimbabwe .
Watu wengi mnasahau kuwa kwa tangu tupate uhuru ni chama kile kile kiko tawala na kulikua mafisadi toka siku hizo.

Sasa huoni tangu Kikwete ameingia Ikulu hawa mafisadi wameanza kuonekana. Kwa nini tusijiulize? is it maybe JK is playing behind the scene?ili asiwakasirishe wazee wa CCM ambao ndio walikuwa wakiwalinda hawa mafisadi. Jamani hebu at least tumpe credit kidogo JK
 
I dont care wapi anasemea kwani kwa vitendo vyake Kikwete tayari ni Kibaraka.

Mwanakijiji namwelewa sana na ninaunga mkono hoja yake endapo tu angekuwa anamwongelea Rais Muungwana.
Tatizo ni kwamba MH Kikwete yeye Binafsi ni mtu asiye na hoja yake Binafsi, anachezeshwa kama Joyce Wowowo, ni mtu wa kuwekewa maneno mdomoni. NI mtu anayefikiri kwa vichwa vya wengine kama akina Chenge ,Rostam na Shogake Lowassa.

Akiweka msimamo wake huko UK aweke tu, kwani kama ni ukibaraka kesha kuwa kibaraka hata kabla ya kusema neno. Kuna mambo mengi tu yanamwingiza kwenye Ukibaraka hili haliwezi kubadili sifa yake.

Napenda Yule Nyati mzee aliyejeruhiwa( Mugabe) aondoke yeye na pembe zake haraka iwezekanavyo.

Asemee UN au asemee Tanzania MH Kikwete ataendelea kuwa Kibaraka tu.
 
Watu wengi mnasahau kuwa kwa tangu tupate uhuru ni chama kile kile kiko tawala na kulikua mafisadi toka siku hizo.

Sasa huoni tangu Kikwete ameingia Ikulu hawa mafisadi wameanza kuonekana. Kwa nini tusijiulize? is it maybe JK is playing behind the scene?ili asiwakasirishe wazee wa CCM ambao ndio walikuwa wakiwalinda hawa mafisadi. Jamani hebu at least tumpe credit kidogo JK

Hakuna Credit yeyote hapo.

Kikwete ni Gobarchev wa Tanzania.

Kikwete is a weak Leader.

Subiri uone kitimtim na kimbembe chupa zote zilizo hifadhi uovu zikifunguliwa.
 
Mimi siamini kwamba kila kitu ni politics. Kama hukubaliani na mugabe na unapenda Zimbabwe unatakiwa kusema, UN, TANZANIA, AU popote na mawazo yanayotoka moyoni hayajali ni nyumbani au ugenini haki za binadamu hazina mipaka. Kila msimamo hata wa haki za binadamu unachukuliwa kama kibaraka na watu wengine lakini haki za binadamu hazijali umasikini au utajiri hivyo raisi anatakiwa aseme msimamo wa nchi kuhusu haki za binadamu bila kutegemea bunge.Mimi nasapoti kikwete kusema hapo NY kwamba tumesikitishwa na mugabe
 
ur right men na si kusema akiwa nyuma ya pazia la UN...nami nitamwita bin mnafiki kwa hili...aweke wazi kama wenzake wanawaswa wa zambia....africa tuwe na msimamo kama alikuwa na msimamo wa comoro yyyyyyyyy not zimbabwe ,,,atangaze basi kupitia kivuli cha AU.....
 
indumene huyu tabho ni kibaraka wa mugabe si lazima nchi za magaribi ziwe na vibaraka wake hata africa kwa africa....ukweli utajulikana tu
 
Tunataka matokeo...zishapita wiki tatu sasa mbona wanakuwa wasiri sana..kuna nini?
cover_650x435.jpg
 
Kumekuwa na vikao na mawazo kwamba Zimbabwe ivamiwe kijeshi, wazo ambalo Mbeki na Kikwete wanaona ni kucheza na moto.

Lakini hasa kinachojadiliwa kati ya Marekani na Uingereza ni kuivamia Zimbabwe ila kwa namna ipi ndio watu wanakuna vichwa.

Mugabe anataka kufanza mtindo wa kama kuna machafuko nchini humo na kutoa amri za serikali ambayo bado haijaapishwa huku akisaidiwa na ma-veterans wake wa ZANU-PF.

Tunasubiri tuone kinachotokea.
 
Yaani viongozi wa Afrika tabu sana. Angekuwa Mugabe kashinda wangeshatangaza matokeo na siku hiyo hiyo angeapishwa, hata kama ingekuwa ni jumapili saa mbili usiku.
 
I see this from different point of view. There is no point of politics of fear, Jakaya was supposed to condemned Mugabe's actions. There is nothing wrong for African leaders to point a finger on stupidity leaders like Mugabe.

Jakaya failed to do so yesterday, he had opportunity to point a finger on Mugabe face and tell him to quit his naive politics. US and UK are right concern Mugabe dictatorship empire, this guy is digging grave for Zimbabwean. Pointing a finger doesn't mean your Kibaraka, but it shows the stability and maturity of your leadership. Jakaya fails to do so under international arena.
 
Whether we like it or not, Mugabe is just a liability na ni watu kama yeye wanazidi kutufanya Africans tuonekane PUNGUANI! Why hold elections if you are not ready to release results or accept defeat? Only in Africa! Swala la JK nadhani inabidi tuliangalie kwa mapana. JK ni mwenyekiti wa AU! sasa kutolea tamko Dar haitasaidia, inabidi aonekane to be walking the walk. AU needs to be serious, waachane na siasa za kulindana. Kama kweli Africa wants to be relevant! WE ARE BEGGARS! YES WE ARE!

It is the same JK na Mbeki jana walikuwa wanaomba pesa za kumaliza migogoro Africa kutoka kwa mataifa makubwa, sasa najiuliza, hiyo migogoro watu kama wanaogopa hata kuiongelea, ndo itamalizwa na pesa? Africans we should WAKE UP! you cant say Bush and Brown are bad people, wakati uko busy unawaomba pesa za kusolve matatizo yako (hapo hujaongelea njaa na wakimbizi wanaoishi makambini wakitegemea hisani za USAID na wenzake)! Kweli sisi ni punguani! Angalia Darfur, Somalia, Congo, Kenya....viongozi wa Africa wanaogopa kunyosheana vidole. Harafu tunalalamika kwama US na EU are not helping us! Are we real?

Listen: we either (few of African elites) continue living in the west enjoying their developments as slaves while the masses on the continent perish as fools and hopeless creatures or we ALL join forces to battles these corrupt and stupid leaders we have in our countries!. We cant continue with these kinds of politics za kinafiki na kulaumu watu kwa matatizo na ujinga wetu wenyewe! Jukumu ni gumu, but it is high time we start and we have to start from somewhere. Siasa za matumbo yetu haziwezi kutufikisha popote. Iam sure jana Bush na Brown wakati wanaongea na viongozi wa Africa (kama walipata hiyo nafasi) walikuwa wanajiuliza kama kweli wanaongea na watu au majangili!!
 
Sasa nimeweka hoja ya kushirikisha vyama vya upinzani katika Umoja wa Nchi huru za Afrika kama zinavyofanya wawakilishi wa Nchi za Ulaya katika Umoja wao ,kwani katika umoja hii wanaowakilishwa ni wananchi hivyo katika hilo hata wapinzani wanaisabika kuwa na wao wanawakilisha au wana uwakilishi hivyo kufanya umoja kushirikisha watu wote.
Wazungu sio kama hawajaliona au hawajaiona kasoro iliyopo katika Umoja wa Nchi za Afrika lakini wamelinyamzia na kuwawacha wakijua kuwa wataweza kuwatumia ,ila kwao wapinzani wanapewa nafasi kwa kila nchi mwanachama ni lazima pia wawemo wawakilishi wa kutoka mrengo wa upinzani.
Kinachoonekana kwa Afrika hivi sasa ni viongozi hawa kutoweza kunyoosheana vidole kwa sababu njia zote wanazotumia za kushinda Uchaguzi ni kutumia wizi wa kura na kuyabadilisha matokeo hivyo wapo katika ile ile sera ya kulindana.
Kama Kikwete angethubutu kumnyooshea kidole Mugabe basi huwezi kujua kwamba Mugabe ndio mwalimu wao na anazijua siri zote za watu wa dizaini ya akina Kikwete na Mugabe anaeleweka kwa kutoa mbovu.
Bado umoja huu unamatatizo kwa kuwepo umoja wa kulindana.Katika jumuia hii kila mpinzani anaonekana na kufananishwa na adui tumeona kuhusu Odinga alipotaka kupeleke ujumbe kwenye mkutano alizuiwa kwa nguvu zote ,huu kama umoja wa Nchi za Afrika vyama vyote vya siasa vilihitajiwa kuwa na muwakilishi.
 
Nakubaliana na maoni ya wenzangu ila angalizo kidogo juu ya hili balaa la zimbabwe .... wote tunajua kuwa Mugabe amechemsha na kuna sehemu pia amepatia mfano kwenye mashamba kurudisha kwa wanachi ... ndipo akawekewa vikwazo vilivyopelekea uchumi kuporomoka kwa kiasi kisichoelezeka. Tsevengerai anapata support financially toka mataifa ya Ulaya kwanini??? wana interest gani na Zimbabwe??? Wantaka demokrasia kweli au wantaka kurudi kutawala zimbabwe???? Kwa vile Mugabe amechemsha wazwazi hakuna mtu mwenye uwezo tena wa kuatazama mambo kwa undani na ku-analyse crotically nchi ya Zimbabwe itakuwa wapi miaka 10 ijayo iwapo Tsangirai atachukua urais na hizi interest za Wazungu wanaompa support!!!!
 
Mkuu mwanakijiji kwa nnavyomfahamu Mugabe hata hii JK akiisemea nyumbani Mugabe atasema amehongwa na hatasita kumtukana hadharani kwamba ni kibaraka. Mugabe is such a desperate kiasi kwamba sasa serikali inaforge ocuments kutaka waafrica waamini kwamba upinzani na magharibi wanataka regime change ili kurudisha ukoloni.

Mimi nadhani kama walivyoshauri wengine inafaa SADC leaders woote watoe tamko moja kwamba wanalaani vitendo vya ukiukaji haki za binadamu Zimbabwe na pia Wizi wa wazi wazi wa haki ya mwananchi kuchagua viongozi wanaowapenda.
 
Msimamo wa Tanzania kuhusu Zimbabwe utangazwe Tanzania... Na tukisha chukua huo msimamo kuhusu Zimbabwe, hatuna budi kuchukua kuhusu Darfur na Iraq... na yote tutangazie toka ardhi yetu.

Hivi tuna msimamo sisi kama nchi katika masuala haya? Foreign Polisi tunayo ya kueleweka?
 
Koba yeye mtu wa jazba jazba tu...fuatilia kwa ukaribu mabandiko yake utaliona hilo...sijui ana machungu gani tu?


...wewe kibaraka wa republican kuanzia leo nabadilisha tone ya ninachoandika hapa,lakini i'm not bitter in any thing
 
Waafrika hatuchoki kuabishwa na hawa mafisadi? Tuanzie kuwakandamiza hapa hapa kwetu... JK kazi kwako baba! Kama uliweza kwenda Comoro, Harare haitakushinda!

./Mwana wa Haki!
 
...kwa viongozi wa serikali zetu za kiafrika kumnyoshea mwenzake kidole ina maana kweli huyo mikono yake safi haswa!, la sivyo ndio yanakuwa yale ya kumnyoshea kidole wakati vidole vitatu vinakunyoshea mwenyewe!

British and US attempts to place Zimbabwe's elections on the agenda of the United Nations Security Council meeting flopped yesterday with African Union chairperson Mr Jakaya Kikwete saying Sadc was managing the situation.
 
Back
Top Bottom