Bwawa la Kariba Mbioni Kushindwa Kuzalisha Umeme kisa Ukame. Zimbabwe & Zambia kwenye Hatihati ya Mgao wa Umeme

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,049
49,731
Mamlaka inayosimamia Bwawa la Kariba linalotegemewa Kwa Umeme na Nchi za Zimbabwe na Zambia imesema inatarajia kuwa na maji kiwango Cha chini kabisa Cha Lita za ujazo bil.16 ambazo ndio zitazalisha umeme.

Kiwango hicho ni Cha chini kabisa kiwahi kufikiwa kutokana na Hali ya ukame ambayo imepelekea maji kupungua.

Hali hiyo huenda ikasababisha matatizo makubwa ya umeme Nchini Zimbabwe na Zambia kwani sehemu kubwa ya Umeme hutoka Kariba Dam.

RAIS SAMIA KUONGEZA BAJETI YA KILIMO MWAKA UJAO WA FEDHA

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) akiongea na wawekezaji wa ndani amesema tayari wamesha wasilisha maombi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza bajeti ya Sekta ya Kilimo ili kutekeleza ajenda yake ya 10/30 kilimo ni biashara.

Aidha, Waziri wa Fedha amesema maombi hayo tayari yanafanyiwa kazi na kuwa Mhe. Rais Samia amesisitiza kuwa lazima tuendelee kuimarisha bajeti za sekta za uzalishaji, huku sekta ya kilimo ikiwa inagusa maisha ya wa Tanzania wengi.

Viongozi hao wamesema hayo wakati wa Mkutano wa Wawekezaji wa Ndani uliona nyoka tarehe 18 Desemba 2023 katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

My Take
Tanesco wanaposema mvua ni Kiduchu muwe mnaelewa.

Sijui Hilo bwawa lenu la Nyerere litazalishaje umeme miaka michache ijayo ikiwa mvua zitapungua miaka 3 mfululizo licha ya serikali kusema linaweza kumudu uzalishaji wa umeme hata kama mvua haijanyesha endapo likijaa inavyotakiwa.
 
Back
Top Bottom