Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,681
- 40,623
Mhe Rais,
Najua pressure ambayo unayo toka kwa GB na Brown hasa kuhusu suala la Zimbabwe. Wanatarajia support ya Tanzania likitolewa Azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani Zimbabwe na matukio yote yaliyotokea baada ya uchaguzi na hasa kitendo cha kutotangaza matokeo.
Ninafahamu ni jinsi gani wakuu hawa wanajaribu kukujenga na kukupa ujiko kama alivyofanya Blair kwa Mkapa na hiyo kuinua profile yako kimataifa kuliko wakati mwingine wowote ule.
Ninafahamu baada ya US kumwaga Dola Milioni karibu 700 wanauwezo wa kuitisha wimbo itakuwa vigumu kuwakatalia. Nafahamu pia Uingereza na wenyewe wameandaa kimfuko kizuri tu kuendeleza ushirikiano na urafiki..
Yota haya nafahamu na nina uhakika na wewe unafahamu. Kwamba wakuu hawa katika suala la Zimbabwe wanataka nchi ya Kiafrika ambayo inaweza kumsimamia Mugabe na kumwambia ukweli bila woga na wao (US na UK) watakuwa tayari kusupport na kuanza kusema "even the AU, Tanzania or President of Tanzania" anaunga mkono. Najua watapamba kwa kutumia nafasi yetu ya historia ya ukombozi n.k na hivyo sauti ya Tanzania kuhusu Zimbabwe itakuwa na nguvu sana.
Sasa Mhe. Rais, hata kama unaamini unayotaka kusema au ambayo wanatarajia useme, naamini hapo siyo mahali pake. Wewe hapo UN piga maneno ya kidiplomasia lakini msimamo wa serikali yetu kuhusu Zimbabwe usisemwe hapo nenda ukausemee nyumbani kwenye Ikulu yetu. Hatutaki Rais wetu uonekane Kibaraka wa wakubwa! Ukisharudi nyumbani na kukutana na baraza lako la mawaziri basi ndio mchukue msimamo kama Taifa na kuamua kulaani hali ya kisiasa ZImbabwe.
Ombi langu ni hilo tu, usitumiwe na wakubwa kuwafanyia kazi yao chafu. Kama una jambo zito la kusema kuhusu Zimbabwe nenda kasemee katika Ikulu yetu pale Magogoni. Vinginevyo, Africa yaweza kukuona umenunuliwa!