Hapa ndio hata mimi kunanishangaza sana, kwanini maradhi haya yanaanywa deal ? kwanini, kampeni ya maralia ifanywe na kiingilio, wakati walengwa ni watu duni kabisa wa kule mwananyamala,vingunguti,Buguruni, Mtoni Aziz Alii, Mbagala, Temeke, Tandika, Mazense, ambao hawawezi kumudu hicho kii........Kuna mtindo umezoeleka sana hapa kwetu kugeuza magonjwa kama deal. Mara ya kwanza hii naona uzinduzi wa kampeni kupinga ugonjwa watu wanatoa kiingilio.UKIMWI na MALARIA ni magonjwa yaliyosumbua taifa letu kwa muda mrefu sasa. Inatakiwa nia ya kweli iwepo katika kupambana nayo. Clouds FM, Ruge na wote mlioandaa hii kitu in atakiwa muwaombe radhi watanzania kwa kuwaibia pesa zao. Mnatakiwa kumuomba radhi Mh Rais kwa kumuaibisha kiasi hiki.
Nimeangalia Press Conference zote mbili (ya Sugu na Ruge)...nimegundua mambo mawili.
1. Waandishi wetu wa habari Tanzania ni mbumbumbu kupindukia.
2. Waandishi wetu wa habari Tanzania wako corrupt and cheap.
3. Kila mjanja Tanzania anajua FACTS namba 1 na 2.
Safari ni ndefu sana.
Nimeangalia Press Conference zote mbili (ya Sugu na Ruge)...nimegundua mambo mawili.
1. Waandishi wetu wa habari Tanzania ni mbumbumbu kupindukia.
2. Waandishi wetu wa habari Tanzania wako corrupt and cheap.
3. Kila mjanja Tanzania anajua FACTS namba 1 na 2.
Safari ni ndefu sana.
Ok labda isomeke hivi:Naomba usigeneralise wote. Rekebisha hoja yako isomeke hivi
1. Baadhi ya Waandishi wetu wa habari Tanzania ni mbumbumbu kupindukia.
2. Baadhi ya Waandishi wetu wa habari Tanzania wako corrupt and cheap.
Hii ya kuweka neno baadhi ni kuwatendea haki wale waandishi wachache makini ambao sio mbumbumbu, wale ambao sio cheap na sio corrupt kwa kutoendekeza njaa, japo wanamaisha duni, kwao uandishi ni wito.
Hata kama Mista Tu ana matatizo, nadhani kwenye sakata hili ameonewa kweli. Jibu la januari hapo juu linaonyesha kuwa naye ana bifu na Mr 2 kwa namna moja au nyingine, na ameiandika kama kumkandya Mr 2 na kumtetea Mutahaba. Kwa kufanya hivyo ametoa statement namba 4 inayopingana kabisa na matamshi ya Mutahaba mwenyewe kama tulivyoona kwenye video hapo juu.
Nimesoma kwa masikitiko juu ya tuhuma za msanii Joseph Mbilinyi ambazo kaziweka kwenye forum nyingine ambako amelalamika kuwa mfanyakazi wa Ikulu January Makamba kwakutumia nafasi yake amemnyima ugali kwenye dili la Malaria No More (MNM)
Facts ni kama zifuatazo:
1. Si kweli kuwa hii idea ya Malaria No More ilikuwa ni idea ya Mr 2 bali ukweli ni kuwa hiki kitu kilianzishwa December 2006 na Peter Chernin and Raymond G. Chambers.
evidence gonga hapa:
http://www.malarianomore.org/about/who/board
na kabla hawajafanya hiki kitu Tanzania walifanya nchini SENEGAL je bado bwana Joseph Mbilinyi anataka kutuambia idea bado ilikuwa yake?
2. Si kweli kuwa aliwaleta MNM Tanzania na ukweli ni kuwa yeye Mr 2 alikutana na Country director wa Senegal kwenye ndege wakati huyu bwana alikuwa anakuja Tanzania kwenye huu mradi hivyo huu nao pia ni uwongo wa hali ya juu sana toka kwa msanii TOO PROUD aka MR 2 aka SUGU aka JOSEPH MBILINYI! so haiwezekana ikawa yeye ndio kawaleta Tanzania
3.Ni vizuri tukawekana sawa kwa kuamabina ukweli kuwa MNM walikuwa wanatafuta local partners who could deliver concert series na wakafanya their own DUE DILIGENCE mwishowe walikata shauri kuwa 2 PROUD hawafai kwa kutumia vigezo vingi tuuu na moja wapo ni kuwa last concert ya Too Proud ilikuwa na watu chini ya 50! if anything wangekuwa hawana akili ya kufuata tuu maneno yake ndani ya ndege!
4.Contrary na maneno yaliyopelekwa Jamii Forums RUGE MUTAHABA did not produce the show bali kazi ilifanywa na jamaa wa ROUNDTRIP!
5.Pia ningependa kusahihisha kwa kusema kuwa if anything DEIWAKA PRODUCTION ambayo inamilikuwa na bwana Sugu ililipwa (FINDERS FEE) na ROUNDTRIP.
6.Role ya Ikulu na kwenye hili ilikuwa ni kusecure the date for the President (Mheshimiwa Kikwete) ili ashirikishwe kwani ni suala la Kitaifa tena lina husu ugonjwa ambao unaongoza kwa kuua waTanzania wengi. Na hili liliwezeshwa kwa kiasi kikubwa na aliyekuwa balozi wa Marekani Tanzania bwana Mark Green
7.Mwisho naona makosa ya MNM ni kumwagia sifa Kem Kem January Makamba na timu nzima ya Ikulu kwa kuweza kufanikisha hii kampeni ambayo ilipata baraka za mkuu wa nchi...Kutokana na logs za ikulu January Makamba hajawahi kukutana na huyu '2 proud'
Nashkuru kwa kunipa nafasi ya kuweka records zangu straight
Ndugu yangu nguvumali, naomba tuwe waangalifu tusije kuwa tunaleta masuasa ya chuki binafsi kwenye kazi za watu. Ruge ni promota, sio msanii, yeye anawapromoti wasanii na wengine wakishasimama, wanajipromoti wenyewe na wengine kugeuka nao ni mapromota, kama alikomtoa JD na sasa JD alipo.
Mr. II ni msanii ambaye ameshasimama na sasa ni promota.
Naomba nimtete Ruge, na Joseph kwa kazi nzuri walizofanya kupitia kampuni ya Prime Time Promotion na Clouds Radio, msanii ambaye was nothing kugeuzwa kuwa something overnight huwezi kusema anadhulumiwa.
Msanii anaelalamika ni yule anaengalia amelipwa nini na kujilinganisha na promota analipwa nini bila kuangalia investment cost. Natolea mfano mdogo tuu, hiyo mic huyo msanii anayoimbia nyingine inacost mpaka milioni 10!, msanii akiimba zikalipwa milioni 3, yeye akapewa milioni moja, promota kabaki na milioni 2, hapo ndio basi kelele za kudhulumiwa!.
Tufike mahali tuwashukuru baadhi ya mapromota wetu, na kukubali baadhi ya wasanii wetu wana matatizo, haswa hawa wa kizazi kipya, wamezidi!.
Out of Topic kidogo...
Kwa upande mwingine; nafurahi sana kuona VIJANA wanafanya mambo ya kwenye jamii yetu; I mean hebu angalia hii trend hapa siku za karibuni....Jerry Muro, Sugu, Ruge, January Makamba, Nehemia, Santus n.k hawa wote ni vijana wakiwa mstari wa mbele kwenye fani zao pale walipo katika kulijenga Taifa...inatia moyo.
Hii mitafaruku ya hapa na pale ni Healthy kwenye ukomavu wa jamii yetu.
Now I know, siku zile mlipokuwa mkizungumzia ku patent ideas, kusema kweli mimi nilikuwa gizani kabisa, uliposema mahali umepatent ideas zako US, nikajisemea kimoyomoyo, what for?.
Sasa nimeelewa ulikuwa na maana gani!.
All in all,. mimi ni muumini mzuri wa sheria ambayo haijaandikwa popote, haina mahakama ya kuienforce, wala hailazimishwi bali ni aplicable, inaitwa ' Karma'.
Maada ulipanga kuyafanya yote kwa nia njema, hata kama ile good ideas zimeibiwa na kutumiwa na wengine kwa nia tofauti, wewe mwenye original ideas utaendelea kubeneft na matunda ya ile idea yako in a good way, wewe na uzao wako, na yule aliiba, hata kama atafaidika imediately. lakini atafidia three folds mbele ya safari.
Naomba usivunjike moyo, Tanzania ni yetu sote na itakombolewa na wachache waliobahatika kuona mwanga, kumulikia wengine ili hatimaye Tanzania nzima tutoke gizani.
Bahati mbaya huwezi kupatent wala kufanya copyright ya a mere idea, namwonea huruma Sugu kama hilo lingewezekana basi angekuwa na kesi nzuri sana lakini kwa sasa inategemea tu kama kulikuwa na mkataba tayari na vipengele vya mkataba huo vilikuwa vinasemaje lakini frankly speaking natamani ashinde ili awatoe nishai hawa wanaojiona mabingwa wa kuneemeka kwa jasho la wengine.
Bahati mbaya huwezi kupatent wala kufanya copyright ya a mere idea, namwonea huruma Sugu kama hilo lingewezekana basi angekuwa na kesi nzuri sana lakini kwa sasa inategemea tu kama kulikuwa na mkataba tayari na vipengele vya mkataba huo vilikuwa vinasemaje lakini frankly speaking natamani ashinde ili awatoe nishai hawa wanaojiona mabingwa wa kuneemeka kwa jasho la wengine.
Nakumbuka walivyo mwita kule Arusha afungue Hoteli kwa mbwembwe na kesho yake Tanroad wanaibomoa. Naona sasa nchi inaendeshwa kama kikundi cha Mdumange, maana kama Mkulu anafanywa mtaji naye anatabasamu tuu, ANATUDHALILISHA WOTE
Mkuu Gembe, kuna issues mbili hapa, naomba tusichanganye issues.
1. Uhamasishaji wa Malaria kwamba haikubaliki, hiki ndicho Mhe. Rais alichokifanya, its the right thing, na anastahili kuungwa mkono na sote tuunge mkono kuwa Malaria haikubaliki, it had nothing to do na usalama wa taifa, kazi yao ni kuhakikisha rais anakuja salama, na kuondoka salama
Nchi hii bwana, yaani kila kitu usanii tu!
Mkuu wa nchi msanii, rahisi kudanganywa mwepesi kuamini tena huyu angehoji kwa nini kuwe na kiingilio kama kuna nia nzuri ya kupamaba na malaria.
Nyimbo zilizoimbwa pale si za kupamba na malaria..
..Na hapa ndo hasa shida ilipo. We are keeping a watchful eye on him et al!Na hao wakina January ndio sampuli ya vijana watawala wanataka kuwarithisha nchi!!!
Ina maana rais hana Usalama wa Taifa wanaopaswa kugundua mambo feki kama haya ili yasimtie aibu?Walishindwa kweli kujua kama hili ni famba tu? Kama itakuwa ndo hivi si atakuja kudhurika siku moja?
Hivi ilikuwa busara pia kwenye ile Red Alert longolongo kuwalazimisha wasanii wachangie vinginevyo nyimbo zao hazitapigwa??? (am just curious)
.........4.Ni kweli kwamba Raisi wetu hashauriki kiivyo, kwamba alishuriwa au alipewa taarifa lakini akadharau?
5.Je ni sahihi kuamini kuwa kuna watu kwa makusudi wanawajibika kumtahadharisha raisi lakini kwa makusudi wanamwacha afanye kitu ili aaibike?
WEELEDI NAOMBA MAJIBU.
Jibu lililotolewa na January Makamba kuhusu sakata hili:
Hata kama Mista Tu ana matatizo, nadhani kwenye sakata hili ameonewa kweli. Jibu la januari hapo juu linaonyesha kuwa naye ana bifu na Mr 2 kwa namna moja au nyingine, na ameiandika kama kumkandya Mr 2 na kumtetea Mutahaba. Kwa kufanya hivyo ametoa statement namba 4 inayopingana kabisa na matamshi ya Mutahaba mwenyewe kama tulivyoona kwenye video hapo juu.
INTERESTING...
SUGU aka MR2 aka 2 PROUD aka
asuthubutu kkwenda Mahakamani kwani kabla ya kesi kuanza CREDIBILITY yake itavunjwa kani sio honest na bora aangalie namna ya kuhandle hii kesi kwa makini kwani FILE lake la HOME OFFICE idara ya IMMIGRATION la UK halihitaji kufunguliwa zaidi ya Pages 2 kujua kama ni mtu wa NAMNA gani.
KAZI KWELI KWELI