Mr. II aibuka dhidi ya Zinduka!

Mr. II aibuka dhidi ya Zinduka!

Oooh kumbe ndo maana wasanii wote (kasoro prof J) walioperform siku ile wako chini ya management ya Ruge!!

Haya bwana....naona na mkuu anamnunulia Ruge Mastering Studio kwa pesa zetu za kodi!!
 
Sugu peke yake hantoweza......hii ni vita kubwa siyo nyepesi kiasi hicho!!!
Ni kweli Zamazamani, hii ni vita kamili ambayo Sugu anataka kuwafumbua macho hata wasanii wenzie, anawatolea uvivu Prime time ambao kwa kutokujua kuwa wanaibiwa baadhi ya wasanii huwaona kama wakombozi kumbe ni wezi watupu.

Wasanii wanapaswa waungane nae, wawe upande wao, wanaweza kupoteza kwa muda mfupi ila for longrun wao watakuwa mashujaa.

Mashujaa kamili.....nashukuru kuona hata hapa JF watu wengi wamemuunga mkono, ni mwanzo mzuri.
 
Pasco najua kuwa unataka kuwa rafiki wa kila mtu, lakini kuna wakati inabidi either ukae kimya au uje ingalau na kitu ambacho kitaonesha kuwa unataka kutoa mchango wako kwa jamii. Achana na Mic za 10m. Hebu tusaidie kujua haya mambo ambayo ni shocking namna hiyo kama:-

i) Je ni kweli nyimbo za Mr II huwa hazipigwi Cloud FM? Mimi sio mpenzi sana wa ubongo wa fuleva ila nilikuwa najiuliza kwa nini Mr II akiwa ni msanii wa mwanzo mwanzo lakini amepoa hivyo.
ii) Kwa kuwa unaelekea kumjua sana mtuhumiwa tunaomba utambie, je ni kweli kuwa anataka kutembea na wasanii kabla ya kuwapromote?

Najua hawa jamaa ni maarufu sana na watu wengi watapenda kuwa karibu nao lakini siyo vyema tukaacha haya maovu yatokee just kwa sababu tu ya kujuana. Sorry najua hawa watu ni muhimu kwa kampuni yako lakini kila mtu atavuna alichopanda
.
Shalom, kwanza asante kwa kudhania kuhusu mimi, sio kweli nataka kuwa rafiki wa kila mtu, I'm just speaking out my mind, na ukiwa mkweli siku zote, lazima uwe tayari kukubali utatengeneza maadui. Mtu anataka kumplease kila mtu, huyo lazima atakuwa ni mnafiki. Mimi sijamtetea Ruge kuwa ndio mtu mwema sana, bali nilichosema tutenganishe facts na chuki binafsi.

Sina uhakika kama nyimbo za Mr. II hazipigwi Clouds kwa vile kwa bahati mbaya, mimi sio msikilizaji wa Clouds ukiondoa kipindi cha Jahazi. Clouds ni redio ya watoto wangu, sisi wa above 40, its not of our age, ila baada ya taarifa hii, nitafuatilia. Ila hizi bifu za kituo fulani kususia nyimbo za mwanamuzi fulani hapa bongo, halikuanza leo, tangu enzi za RTD, kuliwahi ibuka bifu nyimbo za bendi fulani fulani maarufu zikasusiwa.

Pia sio kweli kuwa namjua sana Ruge, bali namfahamu tuu kutokana na majukumu yake, ila Ruge kama promota, anaweza asiwe tofauti na mapromota wenginre wote duniani kote, yule mwanadada Datas, alishasema wazi kuhusu mapromota wanapromoti muziki wako, na ikibidi na mwili wako wanaupromoti japo kidogo.

The line between natural attraction/ true love na promotion kati promota na mteja wake ni very thin.

Mwisho Shalom, hawa watu sio muhumu kwa kampuni yangu, watu muhimu kwa kampuni yangu ni wateja waolipa pesa zao kwangu ili na mimi ndio niwalipe hao.Watu muhimu sana kwa vituo vya redio ni wasikilizaji kama ilivyo watazamaji kwa vituo vya TV na washabiki kwa timu za michezo.
 
Pasco nyimbo za Sugu hazipigwi clouds kabisaaaa!! Na si Sugu tu, kuna wasanii wengi tu nyimbo zao hazipigwi clouds.........Ruge& Kusaga huwa hawakubali kutokubaliana na msanii yoyote yule.

Ukikataa kukubali na kufanya wanachosema, basi nyimbo zako hazitosikika clouds na matamasha yote wanayosponsor either kama lead promoters ama la basi hawatokualika hata kama una nyinbo/albamu kali kuizidi Thriller ya Michael Jackson by then!!

Ni bahati mbaya sana watu wabaya wanaishi maisha marefu!!
 
Pasco nyimbo za Sugu hazipigwi clouds kabisaaaa!! Na si Sugu tu, kuna wasanii wengi tu nyimbo zao hazipigwi clouds.........Ruge& Kusaga huwa hawakubali kutokubaliana na msanii yoyote yule.

Ukikataa kukubali na kufanya wanachosema, basi nyimbo zako hazitosikika clouds na matamasha yote wanayosponsor either kama lead promoters ama la basi hawatokualika hata kama una nyinbo/albamu kali kuizidi Thriller ya Michael Jackson by then!!

Ni bahati mbaya sana watu wabaya wanaishi maisha marefu!!

Wanaishi maisha marefu lakini hawaishi milele,kuna mtego wao Brooklyn
 
Kutokana na maelezo ya sugu,kuna mawili hapa,moja ni a breach of contract,mbili inawezekana kuna watu walioitumia ofisi ya raisi kugain more credibility na hivyo kutake over shuguli nzima na kumgeuka sugu,hata hivyo ni sawa na wizi wa kifaa ambacho matumizi yake huyajui kwani mwishowe utaumbuka tu!

Kitendo cha wao kuto kufollow up na madhumuni halisi ya tamasha hilo inaonyesha walimgeuka sugu halafu hawakuwa na taarifa zote za namna shughuli nzima ilitakiwa kuwa handled,wao walijikita kwenye utapeli kwa kuangalia pesa tu na wakafanya wanachotaka kwakutumia ubavu wa ofisi ya Rais na media,noma kwasababu kama ni kweli walifanya tamasha kibishoo na kugawa neti kwa matajiri na huku wakichaji viingilio inaonyesha ni kinyume cha matakwa halisi ya matumizi ya pesa hizo.

Kuna umuhimu wa popcorn hapa unless wa-settle na sugu.
 
Mmh kweli kufa kufaana..

Hii njaa wabongo inatupeleka pabaya sana hebu fikiria kama tamasha lile lilikuwa ni la kuhamasisha wananchi kwanini watu walitozwa kiingilio? Halafu wale walioingia bure kwa ukaribisho maalum wakakaa VIP wakapewa na zawadi za chandarua wale wenzangu na mie waliojihimu kulipa kiingilio wakaambulia patupu.

Nchi hii jamani kila kitu kinakuwa biashara sasa.
 
Nakubaliana na wachangiaji wote kuwa nyimbo za Mr II hazipigwi Clouds FM...,licha ya tamasha hilo kugubikwa na mushkeli za hapa na pale lakiini limetusaidia kale ka-barabara kanaoingia Leaders kanaitwa Tunisia kamewekwa mkeka...

Kwa hilo nawapongeza Kinondoni Municipal kwa kuzinduka....!!!
 
Nakubaliana na wachangiaji wote kuwa nyimbo za Mr II hazipigwi Clouds FM...,licha ya tamasha hilo kugubikwa na mushkeli za hapa na pale lakiini limetusaidia kale ka-barabara kanaoingia Leaders kanaitwa Tunisia kamewekwa mkeka...

Kwa hilo nawapongeza Kinondoni Municipal kwa kuzinduka....!!!
Tusker baridiii, hapo umenena mjomba......ni kweli kanjia hako kamewekwa mkeka mororo....hahaaaa Tz bana.
 
Mbona hawa jamaa wanaongea kama vile Kiswahili ni lugha ya kigeni? Kweli Watanzania hatujui lugha.....
 
Baadhi ya wabongo waliowahi kwenda ama kuishi Marekani, warejeapo huzungumza kiswahili cha namna hiyo
 
Alimhola unamhala?

naogopa kuandika (ntakosea maandishi) ila nikikupigia utasikia vile ntajibu

lemme try though
mhola du!!!! hahaaaaaaa
uwiii shem patent rights, ownership of ideas and longolongo za kwenye zinduka ndo mada ujue!!!
 
naogopa kuandika (ntakosea maandishi) ila nikikupigia utasikia vile ntajibu

lemme try though
mhola du!!!! hahaaaaaaa
uwiii shem patent rights, ownership of ideas and longolongo za kwenye zinduka ndo mada ujue!!!

Si unajua tena shem nikikutiaga machoni mwenzio ninakuwa "distracted"....

Naona twisheni ya Kisukuma inafanya kazi. Hongera sana kwa jibu lako murua
 
Si unaona sugu nae, kwenda hivyo je kama ndiyo angelikuwa na pass kama akina Ruge si ingekuwa balaa, jamaa kalimwa swali, wewe hauna tatizo lolote na Sugu na Sugu na wewe, nini kilichofanya aandikiwe barua ya kuitwa mahakamani na kuombwa sijui mpaka Jumatatu?

Nchi hii bana, yani mtu anakuja ofisini, eti jamani naomba mumuandikie barua Sugu ya kumtaka asitishe madai yake mpaka Jumatatu, na mahakama nayo inafanya kama ilivyoombwa damn, eti nimeitikia wito wa taifa ndiyo maana nikawalipa wasanii wiki moja kabla, kwani hao wasanii wakiombwa watumbuize bure watakataa?

Lakini nchi ilipofikia panatisha, yani baadhi ya watu wanaamua fanya lolote lile. Kichefu chefu yani, eti jana nimeongea na Sugu usiku nikamwambia sijui yeye hizo hela adai yeye ni mwanaume, lakini asiende kwenye press, sasa kwanini umemkataza asiende kwenye press kama hakuna kinachofichwa, watu wengine bana!

Halafu hizi ngono ninazosikia mnadai ili dada zetu ndiyo watoke, hivi mnataka mlale na wanawake wangapi ndiyo mjisikie nyie ndiyo wanaume? Watu wengine bana achaa tu...
 
Back
Top Bottom