Mponjoli
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 668
- 159
Ndugu yangu nguvumali, naomba tuwe waangalifu tusije kuwa tunaleta masuasa ya chuki binafsi kwenye kazi za watu. Ruge ni promota, sio msanii, yeye anawapromoti wasanii na wengine wakishasimama, wanajipromoti wenyewe na wengine kugeuka nao ni mapromota, kama alikomtoa JD na sasa JD alipo.
Mr. II ni msanii ambaye ameshasimama na sasa ni promota.
Naomba nimtete Ruge, na Joseph kwa kazi nzuri walizofanya kupitia kampuni ya Prime Time Promotion na Clouds Radio, msanii ambaye was nothing kugeuzwa kuwa something overnight huwezi kusema anadhulumiwa.
Msanii anaelalamika ni yule anaengalia amelipwa nini na kujilinganisha na promota analipwa nini bila kuangalia investment cost. Natolea mfano mdogo tuu, hiyo mic huyo msanii anayoimbia nyingine inacost mpaka milioni 10!, msanii akiimba zikalipwa milioni 3, yeye akapewa milioni moja, promota kabaki na milioni 2, hapo ndio basi kelele za kudhulumiwa!.
Tufike mahali tuwashukuru baadhi ya mapromota wetu, na kukubali baadhi ya wasanii wetu wana matatizo, haswa hawa wa kizazi kipya, wamezidi!.
Tatizo lako unaangalia investment upande mmoja tu. Unadhani ili msanii aimbe inahitajika mic tu? Msanii amepewa kipaji na Mungu ili kimneemeshe,msanii anafanya mazoezi miaka kadhaa kabla ya kutoka,msanii anajilipia pesa ya kwenda studio,msanii anahonga baadhi ya radio djs ili nyimbo yake iweze kupigwa japo kwa mara ya kwanza, promota akijua nyimbo nzuri anaingia hapo....
Najua cluods walishindwa kuwaibia wasanii kama MR 2 wanaojua wanafanya nini katika maisha ndiyo maana bifu lipo kubwa sana naye mpaka wakaamua kuacha kupiga nyimbo zake. Pia kuna wasanii kama Inspector walikataa kuingia mikataba ya kitapeli na akina RUGE wakaishia kupotezwa kwenye ramani...
Clouds (wamiliki, watangazaji na management) wote ni vijana wa mjini wanaokula kupitia wasanii bila kugharamia chochote, hakuna ya investment wala nini. Kazi za wasanii zinakataliwa kwa wasambazaji kama hazijapitia kwa RUGE.
Kuna sheria ya anti-trust/competition najua inawabana clouds na akina Mamu kwa kufanya collusion ili kuwanyonya wasanii. Wasanii kama wangekuwa na umoja mzuri wangeweza kufanya mchakato kuwapeleka hawa jamaa mahakamani na wangelipa pesa nyingi mpaka wangefilisika kabisa...na hicho kiredio uchwara kingefungwa....
KUSAGA, RUGE NA CLOUDS
KILA JAMBO LINA MWISHO WAKE MAZEE, ACHENI HIZO, NETWORK MLIZO NAZO IKO SIKU TUTAZING'OA . ACHENI KUJISIFU KUWA MNAKUZA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA WAKATI MNAUFANYA UFE.
SHERIA ZIPO,FUATENI. NAJUA NYIE NI VILAZA HATA HAMJUI KUWA KUNA SHERIA ZINAWABANA KATIKA COLLUSION MNAYOFANYA NA PRODUCERS NA WASAMBAZAJI.