Mr. II aibuka dhidi ya Zinduka!

Si unajua tena shem nikikutiaga machoni mwenzio ninakuwa "distracted"....

Naona twisheni ya Kisukuma inafanya kazi. Hongera sana kwa jibu lako murua

same here shemeji ila tukitoka vekesheni nadhani mambo yatakuwa poa.
najitahidi kujifunza hivo hivo....
 
Mimi ninafanya biashara na wasanii huwezi ukaniambia niache kutafuta wasanii wakati nahitaji hela, matatizo yake amalizane nao huko huko" Ruge alisema
yeye issue kwake bwana Ruge nikusaka mahale, hata kwa kunyonya jasho la wasanii hawa duni....
 
mzee.. wakati mwingine hawa wenzetu huwa wanaweza kufanya lolote lile. Ungeona mawasiliano yetu na dada yule wa Vodacom ungejua jinsi gani tumemdharau. Sasa nikiyaona haya naombea isiwe kweli..

We dare to talk Openly "Mwamvita Makamba" .Hata kama GT atakuja juu basi bwana Ah!
 
Hivi wakati wa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kupima Virusi na JK alikuwepo kulikuwa na kiingilio chochote kile?
 
Usicheze na Ruge , kiboko ya wasanii, peleka dili then una achwa kwenye mataa , hii nikawaida kwa Tanzania lakini , pole sana SUGU nend amahakamani!

Tutanzisha kampeni ya RUGe asipewe usimamizi wa hiyo Mastering Studio ndio tumeshaanza maandalizi tuna anza na maandamano, no voting mbaka RUge awe pembeni..JK hatutaki RUge

Asipewe wakati wao ndio walio omba hiyo studio, na waliomba kama wasanii wa THT.Ila mkuu ajuhi hilo.Na siku ile Kikwete alisema kuwa ameshawapa hela na anasubiri siku ya uzinduzi.
 
............Na hii tunayoiona hapa Tanzania ni cha mchezo tu na wenzentu walishapitia huko zamani sana na walishauwana sana tu na hadi leo hii kuna wengine wanaogopa kabisa kushika Mic kwani mabwana zao watakuja hapohapo na kudai kipato chao chote. Kama hii isipotulizwa mapema, basi tusishangae tukafika huko very soon kwenye kutishiana maisha au kuuwana.

Na hilo jambo Ruge analifahamu vizuri sana..................

Si unaona sugu nae, kwenda hivyo je kama ndiyo angelikuwa na pass kama akina Ruge si ingekuwa balaa, jamaa kalimwa swali, wewe hauna tatizo lolote na Sugu na Sugu na wewe, nini kilichofanya aandikiwe barua ya kuitwa mahakamani na kuombwa sijui mpaka Jumatatu?

Nchi hii bana, yani mtu anakuja ofisini, eti jamani naomba mumuandikie barua Sugu ya kumtaka asitishe madai yake mpaka Jumatatu, na mahakama nayo inafanya kama ilivyoombwa damn, eti nimeitikia wito wa taifa ndiyo maana nikawalipa wasanii wiki moja kabla, kwani hao wasanii wakiombwa watumbuize bure watakataa?

Lakini nchi ilipofikia panatisha, yani baadhi ya watu wanaamua fanya lolote lile. Kichefu chefu yani, eti jana nimeongea na Sugu usiku nikamwambia sijui yeye hizo hela adai yeye ni mwanaume, lakini asiende kwenye press, sasa kwanini umemkataza asiende kwenye press kama hakuna kinachofichwa, watu wengine bana!

Halafu hizi ngono ninazosikia mnadai ili dada zetu ndiyo watoke, hivi mnataka mlale na wanawake wangapi ndiyo mjisikie nyie ndiyo wanaume? Watu wengine bana achaa tu...

Hayo ni maswali ya msingi amabyo Ruge anatakiwa ajibu

Hivi wakati wa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kupima Virusi na JK alikuwepo kulikuwa na kiingilio chochote kile?

Mkuu Mwanakijiji.....
........yaani nami nilishangaa sana kumsikiliza Ruge anasema eti........."pale kutakuwepo na Rais.........gharama za ulinzi........" and then blah blah blah.......gimmee a break..........Ulinzi wa Rais?..............

Kwanini uwa-charge watu kiingilio ?.........hii bado haijakaa sawa.............tukio ambalo udhamini wake uko nje nje........tena hao wakubwa ndio walitakiwa walipe zaidi ili Raia wa kawaida apate kushiriki kisawasawa............
 
Oooh kumbe ndo maana wasanii wote (kasoro prof J) walioperform siku ile wako chini ya management ya Ruge!!

Haya bwana....naona na mkuu anamnunulia Ruge Mastering Studio kwa pesa zetu za kodi!!

Bora wewe umegundua hilo, Hila mkuu wetu ameingia mkenge ajuhi kuwa hiyo ni kwa ajili ya THT, na sio kizazi cha Bongo Flavor.
 
Inamaana kule kumvesha T shirt Mkulu ya Zinduka na kumwita usiku ule pale Leaders yote ilikuwa kumwingiza mjini watu wale mishiko? ama kweli sasa Mkulu umeruhusu watu wakufanye mtaji kama alivyosema Makamba kuwa wewe ni Mtaji.

Nakumbuka walivyo mwita kule Arusha afungue Hoteli kwa mbwembwe na kesho yake Tanroad wanaibomoa. Naona sasa nchi inaendeshwa kama kikundi cha Mdumange, maana kama Mkulu anafanywa mtaji naye anatabasamu tuu, ANATUDHALILISHA WOTE
mie naona kama mchezo mzima ulipata baraka za mkulu.ni maoni tu kutokana na matendo yote yalivyokwenda.

by the way kuna njia ya kuwasiliana na hawa jamaa wa marekani tujue kama ni msaada au biashara na misaada yao wanajua inaenda wapi?
 
Hivi wakati wa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kupima Virusi na JK alikuwepo kulikuwa na kiingilio chochote kile?
hili dili la zinduka jamaa wameingia kichwa kichwa na misaada yao wajanja wenye njaa zao,sijui tamaa zao,sijui tabia zao wakaona hapa hapa mgeni njoo mwenyeji hapone.
 
Maswali mawili hayajajibiwa.

Kuna contracts?

Kama zipo zinasemaje?
 
Na hilo jambo Ruge analifahamu vizuri sana..................

Hayo ni maswali ya msingi amabyo Ruge anatakiwa ajibu

Mkuu Mwanakijiji.....
........yaani nami nilishangaa sana kumsikiliza Ruge anasema eti........."pale kutakuwepo na Rais.........gharama za ulinzi........" and then blah blah blah.......gimmee a break..........Ulinzi wa Rais?..............

Kwanini uwa-charge watu kiingilio ?.........hii bado haijakaa sawa.............tukio ambalo udhamini wake uko nje nje........tena hao wakubwa ndio walitakiwa walipe zaidi ili Raia wa kawaida apate kushiriki kisawasawa............
ha ha ha gharama za ulinzi wa raisi wakati watu wanamwaga hela zao kutaka kusaidia kupambana na malaria inamana serikali wao hawana ulinzi wa kumpa raisi kuhudhuria jambo ambalo linasaidia wananchi wake? kweli jamaa huwa wanakuja na majibu ya kitoto kwenye mambo muhimu.

zile harusi za marafiki na ndugu anazokwenda raisi huwa gharama za ulinzi analipia nani?
 
ukiambiwa ikulu nako kuna fungu la maana lilitengwa kwa ajili ya rais kwenda zinduka utakataa?jaribu kuulizia pale utaambiwa mamilioni mangapi yalitumika,hiyo ndio bongo dalisalama,watu wanapiga dili kushoto,kulia,nyuma,mbele,hadi wadanganyika tunapata kizunguzungu.
 
Sugu alihojiwa jana live na station moja ya radio ya hapa Bongo,amezungumza maneno yaliyonisikitisha sana kama mtanzania mpambanaji. Jamaa anapigana sana na maisha kama kijana lakini wayu wenye connections wanakuja kumnyang'anya tonge mdomoni. Anasema alisikitika sana katika waliotajwa kufanikisha tamasha hilo,jina lake halikutajwa kabisa wakati amefanya kazi kubwa sana na katumia pesa nyingi sana. Jamaa alistahili hata appreciation tu.

Anasema proposal yote kaindaa yeye kasoro mambo machache tu ambayo yameongezewa na akina RUGEMALILA MUTAHABA kama viingilio,kufanyika usiku nk. Jamaa ameongelea jinsi urafiki uliopo kati ya January Makamba na Rugemalila pamoja na clouds jinsi ulivyosababisha Sugu na Deiwaka Productions wapokonywe kazi ya kuandaa tamasha hilo.

BALOZI MARK GREEN

Sugu akiwa anafanya michakato ya tamasha hili alikuwa akiwasiliana na aliyekuwa balozi wa Marekani hapa kwetu Mark Green ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa shirika la Malaria No More mpaka inafikia mahali Green anamwambia itabidi washirikiane na akina Ruge kwani yeye Sugu ndiye mwanzilishi wa idea.

MLAWA WA IKULU

Sugu pia alielezea jinsi alivyokutana na msaidizi wa Rais anayeitwa Mlawa kwa maelezo yake alimpa ukweli wote na kumuomba amkutanishe na Rais kabla ya tamasha. Lakini huyo bwana Mlawa akamkatisha tamaa kwa kumshauri kuwa kwa issue ilipofikia imekuwa complicated na aachane nayo.

RUSHWA KWA WANAHABARI

Baada ya kuongea na vyombo vya habari, Sugu anasema kuna ushahidi kuwa counterparts wake walitembeza mlungula wa waandishi wa habari ili habari isitoke,lakini waandishi wngine ambao wanaheshimu kazi yao na weledi walitoa habari kama kawaida.

Maoni yangu

MAGONJWA KUGEUZWA DEALS

Kuna mtindo umezoeleka sana hapa kwetu kugeuza magonjwa kama deal. Mara ya kwanza hii naona uzinduzi wa kampeni kupinga ugonjwa watu wanatoa kiingilio.UKIMWI na MALARIA ni magonjwa yaliyosumbua taifa letu kwa muda mrefu sasa. Inatakiwa nia ya kweli iwepo katika kupambana nayo. Clouds FM, Ruge na wote mlioandaa hii kitu in atakiwa muwaombe radhi watanzania kwa kuwaibia pesa zao. Mnatakiwa kumuomba radhi Mh Rais kwa kumuaibisha kiasi hiki.
 
Namalizia kusoma post ya 113.

Baada ya kusoma, kama mtu muungwana kinachosubiriwa ni hekima na busara yangu kuishirikisha katika mjadala huu.

Wenye weledi wa uendeshaji wa serukali kama taasisi mhimili wa dola katika taifa watusidie kuelew yafuatayo:
1. Nini nafasi ya Raisi katika mwaliko kama huu katika kufanya maamuzi ya kukubali kushiriki au kukataa.
2. Watu gani wanahusika zaidi, Usalama wa Taifa, Wasaidizi wake ama Washauri wa Raisi (Kumpatia Raisi habari sahihi pamoja na kumshauri juu ya ushiriki wake) Kwa mfano NI YUPI KATI HAO ALIYETAKIWA KUMWAMBIA RAISI KUWA HILI NI TAMASHA LA KULIPIA NA HALIWEZI KUWA UZINDUZI WA KAMPENI YA KITAIFA.
3.Katika hali ya aibu kama hii ni yupi kati hao anayetakiwa kuwaomba radhi watanzaia wanaokufa kwa malaria kwa Kuwakejeli? au hata kujiuzulu?

4.Ni kweli kwamba Raisi wetu hashauriki kiivyo, kwamba alishuriwa au alipewa taarifa lakini akadharau?

5.Je ni sahihi kuamini kuwa kuna watu kwa makusudi wanawajibika kumtahadharisha raisi lakini kwa makusudi wanamwacha afanye kitu ili aaibike?

WEELEDI NAOMBA MAJIBU.

Mr II
Kwanza nikupe pole sana, Ukifungua kesi hapa itakumaliza kiuchumi na haki hutapata, ukifanikiwa kuipata haitatekelezwa mpaka ukamilifu wa dahari.

Umeshitaki kwa jamii, endelea kushitaki kwa jamii mpaka kila mmoja alijue hili, haki yako iko kwa kizazi kijacho.

Kesi ya Marekani imekaa vizuri kimbizana na hiyo, kule unaweza kupata haki. kwa sababu wenzetu wanaheshimu sana mawazo ya watu katika ubunifu.

Mwisho ni mwisho tu, inabidi kitu au mtu afikie mwisho siku moja.
 
Naweza kusema tu kwamba mara nyingi sana kwa hapa kwetu imekuwa ni mazoea ya watu wenye nguvu waliokosa ubunifu kuwanyonya watu makini na wabunifu. naungana kabisa na Mr II katika kuujulisha umma ni namna gani inaumiza moyo na kukatisha tamaa. Najifikiria kama huyu bilinyi angeamua kuendelea na uamuzi wake wa kwenda mahakamani na tamasha kusimamishwa ni nini kingejieleza mbele ya mwaliko wa rais!
 
Kwa kweli naomba niwapongeze wanajamii kwa kulijadili hili mmetimiza wajibu wenu na nimshukuru Sugu kwa kuwa muumini wa kweli wa haki na ujasiri aliouonyesha kutujuvya hili!

Katika majukwaa tofauti tumeshawahi kuelezea uozo uliopo katika baadhi ya media camps zetu hapa nchini kama si zote; Na bahati mbaya hawa jamaa wa Clouds wametajwa sana! Ni bahati mbaya hili nalo ni mwendelezo wa hayo mabaya tuliyowahi kujadili.

Binafsi najaribu kuona sisi kama jamii ya watanzania tunawezaje kuhakikisha waliotukosea namna hii na kutuaibisha (maana kumwaibisha kiongozi tuliyemchagua ni kutuaibisha sisi sote!) wanachukuliwa hatua walau kwa KULAZIMISHWA kutuomba radhi Watanzania?

Naendelea kuwaza.
 
Sugu alihojiwa jana live na station moja ya radio ya hapa Bongo,amezungumza maneno yaliyonisikitisha sana kama mtanzania mpambanaji. Jamaa anapigana sana na maisha kama kijana lakini wayu wenye connections wanakuja kumnyang'anya tonge mdomoni. Anasema alisikitika sana katika waliotajwa kufanikisha tamasha hilo,jina lake halikutajwa kabisa wakati amefanya kazi kubwa sana na katumia pesa nyingi sana. Jamaa alistahili hata appreciation tu.

Anasema proposal yote kaindaa yeye kasoro mambo machache tu ambayo yameongezewa na akina RUGEMALILA MUTAHABA kama viingilio,kufanyika usiku nk. Jamaa ameongelea jinsi urafiki uliopo kati ya January Makamba na Rugemalila pamoja na clouds jinsi ulivyosababisha Sugu na Deiwaka Productions wapokonywe kazi ya kuandaa tamasha hilo.

BALOZI MARK GREEN

Sugu akiwa anafanya michakato ya tamasha hili alikuwa akiwasiliana na aliyekuwa balozi wa Marekani hapa kwetu Mark Green ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa shirika la Malaria No More mpaka inafikia mahali Green anamwambia itabidi washirikiane na akina Ruge kwani yeye Sugu ndiye mwanzilishi wa idea.

MLAWA WA IKULU

Sugu pia alielezea jinsi alivyokutana na msaidizi wa Rais anayeitwa Mlawa kwa maelezo yake alimpa ukweli wote na kumuomba amkutanishe na Rais kabla ya tamasha. Lakini huyo bwana Mlawa akamkatisha tamaa kwa kumshauri kuwa kwa issue ilipofikia imekuwa complicated na aachane nayo.

RUSHWA KWA WANAHABARI

Baada ya kuongea na vyombo vya habari, Sugu anasema kuna ushahidi kuwa counterparts wake walitembeza mlungula wa waandishi wa habari ili habari isitoke,lakini waandishi wngine ambao wanaheshimu kazi yao na weledi walitoa habari kama kawaida.

Maoni yangu

MAGONJWA KUGEUZWA DEALS

Kuna mtindo umezoeleka sana hapa kwetu kugeuza magonjwa kama deal. Mara ya kwanza hii naona uzinduzi wa kampeni kupinga ugonjwa watu wanatoa kiingilio.UKIMWI na MALARIA ni magonjwa yaliyosumbua taifa letu kwa muda mrefu sasa. Inatakiwa nia ya kweli iwepo katika kupambana nayo. Clouds FM, Ruge na wote mlioandaa hii kitu in atakiwa muwaombe radhi watanzania kwa kuwaibia pesa zao. Mnatakiwa kumuomba radhi Mh Rais kwa kumuaibisha kiasi hiki.

Kama ni kweli then the all project 'sucks'.
 
Salut Mr. II kwa kusimama na kusema ukweli ijapokuwa inawezekena ushahidi wa moja kwa moja wa kutia watu hatiani usiwepo lakini Ofisi ya Raisi kufanya faulo ni kawaida sana kwa kisingizio cha usiri unaotumika kuendesha kazi zao.

Makampuni madogo ya consulting na auditing wameumia sana kwa mtindo huu wakati mwingine hata proposal ukituma anatumiwa mtu wanayemtaka na anashinda kiulaini sana. Pole sana mzazi lakini in the future mkiwa na deal kubwa msikae kimya mpaka mambo yaharibike. Hata BOT wanamtindo huo pia, silaha yao kubwa ni kutafuta mtu ambaye wanamtaka wao kwa maslahi yao na kazi inafanyika.

Sugu, haki huwa haipotei kirahisi lakini tumia vizuri karata zako badala ya kwenda kwenye media ni bora ukalalamika kupitia taratibu za manunuzi zinazokubalika, kwa mfano bongo kunasheria ya manunuzi ambayo inatosha kwa kuanzia kama ni contract ya serikali.
 
Nimeangalia Press Conference zote mbili (ya Sugu na Ruge)...nimegundua mambo mawili.

1. Waandishi wetu wa habari Tanzania ni mbumbumbu kupindukia.

2. Waandishi wetu wa habari Tanzania wako corrupt and cheap.

3. Kila mjanja Tanzania anajua FACTS namba 1 na 2.

Safari ni ndefu sana.
 
Back
Top Bottom