Mpya: Askari polisi wa kituo cha Mbalizi Mbeya wafanya Ibada kituoni kuomba Mungu atuepushie janga la Corona

kuna watu humu kazi yao ni kupinga tu maombi hayafanyi kazi mara ooh fwateni maelekezo tu. niwakumbushe tu hakuna jambo lolote katika dunia hii ambalo halijaanzia katika ulimwengu wa roho maana huu ulimwengu ni kopi tu ya ulimwengu wa roho. Halafu hao walio matajiri na teknolojia za hali ya juu wapo wapi kama siyo tu wanalia hadi makamasi yanawatoka wakati Tanzania vifo ni vya kudunduliza. Na watatkuja na hoja muda bado lakini na wahakikishia kama ni Mungu huyu tunayemuabudu mjiandae kuaibika kwa maneno yeno na kebehi zenu juu ya huyu Mungu na nchi yetu ya Tanzania.
Police kufanya maombi we unaona si jambo la kupinga kweli wajinga hawaishi humu duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunako elekea huku Sasa mpaka inakera yaan, dunia inatushangaa kwa haya maigizo tunayo yafanya
 
Kuna watu wanamfanyia Mungu dhihaka
Hasira yake itajibu very soon
Askari polisi wa kituo cha Mbalizi mkoani Mbeya leo wamefanya Ibada kituoni hapo kutimiza maelekezo ya Rais Magufuli ya kufanya maombi dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

Ibada hiyo iliongozwa na mkuu wa kituo afande Lusekelo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya.

Source ITV habari.

My take; Tukio hili la ibada na namna makamanda walivyokuwa wakikemea katika jina la Yesu limenibariki sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi la polisi halina dini lakini nashangaa wanageuza kituo cha polisi kuwa kanisa nina uhakika ingekuwa waislamu ndio wamefanya hayo kelele zingekuwa nyingi sana, waache upuuzi siku nyingine wakitaka kumuomba huyo wanayemuita Yesu waende kanisani
Kwani mkuu limesali jeshi au wamesali watu, jeshi linaweza kuwa halina dini ila linatambua na linajua kuna dini.

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
 
My take; Tukio hili la ibada na namna makamanda walivyokuwa wakikemea katika jina la Yesu limenibariki sana
Wameishiwa na mabomu ya machozi?

Korona itasumbua vipi mbele ya mabomu na risasi!

Waeleze hao askari waliofanya ibada hiyo wapo njiani kutumbuliwa, kwa sababu akili zao haziendani na askari wengine.
 
Askari polisi wa kituo cha Mbalizi mkoani Mbeya leo wamefanya Ibada kituoni hapo kutimiza maelekezo ya Rais Magufuli ya kufanya maombi dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

Ibada hiyo iliongozwa na mkuu wa kituo afande Lusekelo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya.

Source ITV habari.

My take; Tukio hili la ibada na namna makamanda walivyokuwa wakikemea katika jina la Yesu limenibariki sana!
Limekubarikije?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri: Tuepuke ibada za kinafiki. Mungu hadhihakiwi. Tunaweza kuwa tunaomba hukumu tusipokuwa makini katika maombi yetu. Tuache ibada za maigizo. Tuombe kwa ibada iliyo kuu mioyoni mwetu.

Tusiombe kwa nia ya kutengeneza habari, na kujionesha kwa aliyeagiza.
Uzuri wa JF huwezi kukosa wanaotumia vichwa vyao kufikiri na kupata jibu.

"Tusiombe kwa nia ya kutengeneza habari na kujionesha kwa aliyeagiza."

Na kwa hakika, hata aliyeagiza hakuaagiza kwa nia ya 'kuombea taifa' kalenga kupata faida kisiasa kutokana na agizo hilo.
Sarakasi hizi zimekuwa rahisi siku hizi kuzing'amua.
 
Ushauri: Tuepuke ibada za kinafiki. Mungu hadhihakiwi. Tunaweza kuwa tunaomba hukumu tusipokuwa makini katika maombi yetu. Tuache ibada za maigizo. Tuombe kwa ibada iliyo kuu mioyoni mwetu.

Tusiombe kwa nia ya kutengeneza habari, na kujionesha kwa aliyeagiza.
Watu wakiomba mnaongea,wakienda kunywa gongo napo mnaongea,
Mtaacha lini kuongea?

Acha jina la mungu loitwe kila kona maana zinaa na dhambi mlifanya kila mahala pia
..
 
Weka video/picha tuone makamanda wetu wanavyofanya juhudi ya kupambana na COVID-19
 
Back
Top Bottom