Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
We ndio akili NDOGO kweli..🤣🤣
 
Kaka paskali mchakato wa kuwapa dipiwelidi bandari unamkanganyiko na chembe chembe nyingi za sintofahamu.

Viongozi wasiwe na haraka kwenye hilo suala la bandari.

Halafu hao tec hawajakurupuka aiseee wamewahoji wahusika wengi.

Mwambieni Mama awe anasoma vitu na apatapo mashaka awe na vijana watiifu kwa jamhuri na sio chawa wawe wanamwambia ukweli mchungu.

Hatuna rekodi nzuri za kimikataba hasa tunayoenda kusaini tukiwa na njaa

Shida ni kubwa ni kuwa kama taifa hatuna dira rasmi.
Wao wametoa mashauri yao kama baraza naamini wanamaono yenye wema ndani.
Ingekuwa watu wote humu wanatoa comments zenye busara ndani yake kama comment hii sidhani kama kungekuwepo na mipasuko ambayo inaonekana miongoni mwa jamii inayojadili suala hili humu mitandaoni !!

Kebehi kejeli na dharau huwa siku zote hazijengi bali hubomoa tu. !!

Tusubiri tuone !!
 
Du we Mayalla mi nadhani unafikiri kwa kuendeshwa na tumbo/njaa wala si ubongo, kwa hulka hii haufai kuwa kiongozi mahali popote hata kwenye familia yako.

Hao maaskofu ktk waraka wao hakuna mahali wamekataa mkataba wa bandari kwa kuzingatia dini ya mtu isipokuwa wametumia hoja zinazotokana na mkataba wenyewe pamoja na mgawanyiko uliojitokeza kwa wananchi na wewe ungejikita huko ktk kuwapinga na si kutumia hisia zako za udini ambazo haziwezi kuthibitika.

Ingawa ndani ya mawazo(moyo) ya mtu hatuwezi jua kilichomo pasipo kutamkwa au kuashiriwa, basi kwa kuwa maaskofu hawajasema wala kuashiria kupinga mkataba kwa hoja za kidini basi na wewe jikite kuwakosoa kwa kutumia hoja walizotumia, kinyume na hapo wewe na wenzako wenye mawazo sawa na yako ndo mtakuwa wadini.
 
Kwaiyo na usomi wako wa Sheria ,hoja za kukiukwa kwa Sheria mbalimbali za nchi kwenye mkataba (IGA) ambazo wadau wengi wamekuwa wakizipinga we umeona sawa tuu?? Dah...ndio kuwinda teuzi sio? Maaskofu nao niwananchi.... unless utueleze sifa za mtu kuwa mwananchi ni zipi?? Na Je hao maaskofu wanazo?? Au hawana ?? Ebu tuweke utaifa mbele ,na tuendane na usomi wetu .
 
"Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Mungu mwenyewe, kumaanisha Vox Populi is Vox Dei, hii maana yake waraka huu ni sauti ya Mungu.

Ushauri wa bure kwa Rais Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu,..........

Nakushauri Mama kubaliana tuu na ushauri wa TEC, hili jambo achana nalo kwa sasa, kisha anzisha mchakato upya kwa kufuata a due process, hakuna mwekezaji wa Bandari kushindana na DPW, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, very honourably". Alisema Pascal Mayalla
 
Watu wanaotumia dini ya mtu au mlengo wa kisiasa kupinga au kukubaliana na mkataba wa bandari hawana tofauti na waraibu wa madawa ya kulevya kwa kuwa tayari wamekuwa addicted hivyo hawana uwezo wa self control hivyo wanahitaji msaada.
 
Pasco aliyekupatia haki wewe kutoa maoni yako ndiye aliyewapatia TEC kutoa maoni yao. Hakuna mwenye monopoly ya kutoa maoni. Sauti ya kinabii ni pamoja na kuwasemea watu. Hata hivyo ukumbuke kuwa maaskofu wa Tanzania ni watanzania kama wewe. Mali za watanzania ni mali zao, hivyo wana haki ya kikatiba kama watanzania kuzilinda na kuzisemea mali zao. Kuwa viongozi wa dini hakuwaondolei haki yao kama raia. Tena hauwezi kutenganisha dini na siasa safi. Manabii katika maandiko hawakunyamaza walipoona mambo hayaendi vizuri!
 
Ndo hao eti wanajiita machawa,wapo tayari kwa lolote,ili wapate hela,hata ikiwezekana kupiga magoti ili wapate teuzi,na hata ikiwezekana wanaweza hata kuingiliwa kinyume na mila na desturi endapo wakiona fursa.Nyerere alikosa nini hadi akajitosa kupigania uhuru au Mbowe anakosa nini hadi anaendelea kupambana kwaajili ya wananchi wenye kipato cha chini?
Akina Lissu,ana pesa ambazo anaweza akala hadi anakufa,pesa ambazo anaweza kuishi maisha ya kawaida na asipate shida yoyote,lakini bado wanapigania wananchi.Tuwe real,tuache uchawa.
 
Baraza la maaskovu haliruhisiwi kutoa kauli (matako) ya kukemea au kuipinga uonevu,unyonyaji na ukandamizaji? Kanisa pia lina kazi ya kutetea haki za wananchi kwa kupaaza sauti linapoona haki zao zinakanyagwa na serikali.
Mkuu ni matamko sio matako
 
Siju nyingine usamarize hayo maandiko yako, uandishi wa kizamani peleka huko magazetini hapa mtandaoni briefly and clea.

Sijui uelewi nini kwa ulichoandika..
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, CCM ndio chama cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?

Kufuatia kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.

Tuambiane ukweli, angekuwa ni Magufuli ameileta DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.

Bwana wetu Yesu Kristo alituasa tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Ki Mungu, jee waraka mzito kama huu, haujachanganya ya Ki Mungu na ya Kaizari?.

Pia Bwana wetu Yesu Kristo alituusia tuwe makini sana na manabii wa uongo, niliwahi kuandika hivi humu Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

Sipingi uhuru wa Maaskofu Katoliki kutoa kutoa maoni yao binafsi kuhusu jambo lolote, lakini maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW, kitu ambacho kitawakwaza Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha Kanisa Katoliki!.

Sina tatizo kiongozi yoyote wa dini akihubiri amani, mimi mwenyewe ile 2010, JK alikuwa na hali mbaya, nimezunguka nchi nzima na Askofu Moses Kulola kuokoa jahazi Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Niliwahi kuuliza maswali haya kuhusu viongozi hawa wa dini
Hitimisho
Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Mungu mwenyewe, kumaanisha Vox Populi is Vox Dei, hii maana yake waraka huu ni sauti ya Mungu.

Ushauri wa bure kwa Rais Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe, Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo tangu alipoupuuza ushauri huu,... naomba nisimalizie.

Hivyo mimi nikiwa ni mmoja wa wana jf wenye kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Nakushauri Mama kubaliana tuu na ushauri wa TEC, hili jambo achana nalo kwa sasa, kisha anzisha mchakato upya kwa kufuata a due process, hakuna mwekezaji wa Bandari kushindana na DPW, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, very honourably.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu DPW na Bandari zetu
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
  8. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  9. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  10. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  11. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  12. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!.
  13. Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
  14. IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
  15. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  16. IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
  17. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
  18. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?

Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?​

I don't think you have a good understanding of the Bible even if you are Catholic. I am Catholic and I was raised in the church and studied in seminary.

Iko hivi, "Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari" Jesus gave this answer publicly because he was trapped by the Pharisees and it was just a response to get out of the trap he was trapped in.

"Then the Pharisees went out and laid plans to trap him in his words. Tell us then, what is your opinion? Is it right to pay the imperial tax to Caesar or not?
But Jesus, knowing their evil intent, said, You hypocrites, why are you trying to trap me? 19 Show me the coin used for paying the tax. They brought him a denarius, and he asked them, Whose image is this? And whose inscription?

Caesar’s, they replied.

Then he said to them, So give back to Caesar what is Caesar’s, and to God what is God’s.
People believed it was wrong to pay tax and Jesus gave a very intelligent answer. A replica of statement was made again by Kwame Nkrumah when he asked "where Africa is facing?", Kwame Nkrumah replied "We face neither East nor West; We face forward"

Sasa hayo yalikuwa majibu ya kiakili kujitoa kwenye mtego na sio uhalisia wa mambo yalivyo ama msimamo wake kuhusu ulipaji wa kodi.

Yesu aliliongelea hili la kodi tena vyema kutoa msimamo wake: Matthew 17:24-27

"The Tax
After Jesus and his disciples arrived in Capernaum, the collectors of the two-drachma temple tax came to Peter and asked, “Doesn’t your teacher pay the temple tax?” Yes, he does, he replied.

When Peter came into the house, Jesus was the first to speak. What do you think, Simon? he asked. From whom do the kings of the earth collect duty and taxes—from their own children or from others? From others, Peter answered.

Then the children are exempt, Jesus said to him. But so that we may not offend them, go to the lake and throw out your line. Take the first fish you catch; open its mouth and you will find a four-drachma coin. Take it and give it to them for my tax and yours.

sio kuchanganya dini na siasa?​

Only a fool can confuse himself and put up baseless objections against the well-being of his life and his future generations.
 
Matamko ni kawaida maslahi yao yakiguswa

Msamaha wa Kodi na mizigo yao imepigwa biti
Watalia sana na ni kawaida ukigusa huko
Kuna money laundering sana bandarini
 
Ukibatizw unakuw kuhani, nabii na mfalme

Na ndivyo kanisa lilivyo

Kuhani kuongoza matakatifu


Nabii kusema ukweli hats ukikatwa kichwa kama yohana


Mfalme kutawala na kuongoza kama daudi, au Solomon


Bear it in mind bro uteuzi si muhimu kuliko maisha ya wanetu

Be humble
 
Back
Top Bottom