Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,
Tumsifu Yesu Kristo.
Declaration of Interest
Mimi ni Mkristo Mkatoliki die hard, yaani wale Wakatoliki ambao wamezaliwa Wakatoliki, na kupokea zile sakramenti 4 za Katoliki, yaani wamebatizwa Katoliki, wamepokea Komunio Katoliki, Kipaimara Katoliki, ndoa Katoliki, na ile sherehe ya mwisho pia ni Katoliki, ila ni waumini wa type ya Tomaso!.

Imani ni kitu very delicate, unaambiwa Mungu yuko mbinguni, unaamini bila kujiuliza lolote!. Unaambiwa kuna peponi, unaamini!, unaambiwa kuna motoni, unaamini!. Unaambiwa kuna malaika wanaruka kwa mabawa, unaamini!. Unaambiwa kuna shetani na kuna mapepo unaamini!. Sisi waumini wa Tomaso type tukiambiwa chochote, huwa tunauliza na kujiuliza!.

Kufuatia imani ni kuamini kile unachoaminishwa na the people you can trust, ndio maana mtu unapozaliwa, ukizaliwa kwenye Uislam unaamini Islam ndio dini ya kweli!, ukizaliwa kwenye Ukiristo, unaamini Ukristo ndio dini ya kweli!, mimi nimeishi kidogo India na kupata fursa ya kusoma kidogo Hinduism na Buddhism, ndipo nikagundua kumbe Christianity na Islamic ni kama dini za juzi juzi compared to Hinduism na Buddhism!

Watu tuna tendency ya kuwaamini sana viongozi wetu wa dini kuwa mafundisho yao yote ni mafundisho ya Mungu, neno lao ni neno la Mungu!.

Kanisa langu Katoliki Tanzania from time to time, huwa linatoa Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, kuzungumzia jambo lolote kiwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Hivi karibuni TEC imetoa waraka kupinga mkataba wa DPW na Bandari zetu. Waraka huo umesomwa wote kwenye misa zote, na ibada zote za makanisa yote ya Katoliki Tanzania nzima, kwa wiki mbili mfululizo.

Kwa vile waraka huo unasomewa altareni, madhabahuni na mimbarini, Hivyo kuna baadhi ya Wakristo Wakatoliki wanadhani waraka huo wa Maaskofu Katoliki Tanzania, ni sehemu ya ibada na ni neno la Mungu!.

Hivyo Wakatoliki waaminifu na watiifu wakauamini waraka huo kwa kudhani ni neno la Mungu, hivyo kuuheshimu hadi kudhani usipokubaliana nao, ni kwenda kinyume cha kanisa Katoliki hadi wengine kudhani ukitofautiana na msimamo wa Maaskofu Katoliki Tanzania ni kutenda dhambi!.

Natoa wito kwa kanisa langu, ambalo ni kanisa moja Takatifu Katoliki la Mitume, Ili kuepuka kuchanganya dini na siasa, waumini Wakatoliki pia tuambiwe ukweli kuwa Waraka ule wa TEC, Sio Neno la Mungu!, ni maoni ya Maaskofu Katoliki Tanzania na sio maagizo ya Mungu na mtu Mkatoliki usipokubaliana na waraka huo, sio dhambi na wala sio kosa lolote kutotii waraka wa TEC, ili Wakatoliki wote wanaiunga mkono serikali yetu katika issue ya DPW na Bandari zetu, wasikose amani ndani ya nafsi zao!.

Na ili kuepuka mkanganyiko ya kutukanganya waumini kuhusu uwezekano wa kuchanganya dini na siasa, kunapotokea nyaraka au maagizo ya kidunia ambayo sio ya Mungu, kama hili tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, lisiwe linasomewa madhabahuni, liwe linasomewa kwenye podium ya chini, ili lisije kuhesabika nalo ni neno la Mungu!, au ni sehemu ya ibada kumbe ni mambo tuu ya kidunia na sio mambo ya Mungu!.

Hivyo sisi Watanzania Wakatoliki tunao unga mkono uwekezaji wa DPW kwa Bandari zetu, tusikose amani ndani ya nafsi zetu kwa kutokubaliana na Maaskofu wetu, ambao ni viongozi wetu wa dini, tunao waamini sana, tunawaheshimu sana na kuwategemea sana kutuongoza kufika mbinguni kwa Baba yetu kwenye makao yetu ya milele!.

Tumsifu Yesu Kristo

Paskali.
Rejea
 
Bwana Pascal Mayalla naona unahaha sana. Huenda wewe ni mkristo usiyelijua neno la Mungu.

Tangu enzi na enzi watumishi wa Mungu wametumika mara zote kwenye siasa.

Nakusihi uende kwenye Biblia ukasome habari za Yohana Mbatizaji na mfalme Herode.

Yohana alimkemea sana Herode kutokana na kufanya mambo ya hovyo.

Nenda kasome habari za Daniel pia.

Mimi nitaendelea kukufundisha tu mpaka kichwa chako kikae sawa.
 
Natoa wito kwa kanisa langu, ambalo ni kanisa moja Takatifu Katoliki la Mitume, Ili kuepuka kuchanganya dini na siasa, waumini Wakatoliki pia tuambiwe ukweli kuwa Waraka ule wa TEC, Sio Neno la Mungu....
Hii yote ni kuhusu upingaji wa DP world tu hakuna kingine, naona ujumbe umewafikia vzr waamini kila kona ya Tanzania!

Mnaosema viongoz wa dini wanachanganya dini na siasa ujumbe wenu huo hapo 👇👇👇👇

IMG_20230824_154435~2.jpg
 
Hata hujui Mungu hufanya kazi yake kwa njia zipi, na huwatumia watu gani, kwa makusudi yako, nakuona unaligeuza lile tamko la TEC kuwa la kisiasa, ili upate sababu za kulipinga kisiasa, ili toka hapo, ndio uanze kupindisha ukweli wa lile tamko, mayalla sasa unaifanya kazi ya shetani bila woga wala hofu.

Unapokataa waraka wa TEC sio neno la Mungu, unamzungumzia "mungu" wako anayenyima haki za wengine, asiyejali wanaoonewa, wanaolalamika kudhulumiwa haki zao, yule aliyeamua kuwazibia masikio wale wamliliao.

Usijidanganye kutumia kivuli cha "dini na siasa" ili kuukataa/kuufisha ukweli uliopo kwenye ule waraka, endelea kuukataa kwa interest zako, ili umfurahishe huyo unayemtumikia ukiamini atakukumbuka kwenye ufalme wake wa ulimwengu huu ...

Lakini pia utambue, yupo Mungu mkuu unayemkasirisha kwa haya maandiko yako, yaliyojaa utapeli, yasiyojali haki za wanyonge wanaoonewa, siku yaja pale atapokuchapa kwa fimbo yake, usilalamike.

Mungu hadhihakiwi.
 
Back
Top Bottom