Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012.
Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa. Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo
Wanjamvi, tuna bahati ya kuwa na ukumbi na kukutana na baadhi ya viongozi, watu wenye uzoefu mbali mbali, taaluma n.k. Ni dhima yetu kuhakikishia tunaitumia fursa hii kujadiliana mambo yanayolisaidia taifa ikiwa ni pamoja na ukuaji wa demokrasia kwa ujumla.
Ukisoma mada utaona ina mapungufu. Kitila kuwepo Uingereza tarehe hizo inaweza au kutoweza kuwa kweli.
Mtoa mada ameandika ili kujenga hoja yake kwa mashiko lakini tarehe peke yake hazijengi hoja.
Nilitaraji angetueleza aliyoyasema Kitila ''miongoni mwa mambo aliyotueleza..' yangekuwa ima ya mkutano, kikao au mkusanyiko fulani rasimi au usio rasimi na hata mahali na muda. Mtoa mada hajasema hayo! Ameweka tarehe kama hoja.
Nikikutana na Kitila Mwenge halafu nikaweka uzi kuwa 'amesema' sidhani kuwa tutakuwa tunawatendea watu haki.
Ikifika hapo kila atakayepeana mkono na Dr au Nape au Kitila anaweza kuzushiwa uzi tu kwahiyana au hata kwa heri.
Mtoa mada angeileta kama 'analysis' kwa kutumia maneno hayo bila kumnukuu mtu kusingekuwa na tatizo.
Tatizo ni pale alipomnukuu bila kutuwekea vithibitisho vingine halafu anataka umma uamini kile anachosema.
Tujifunze kuwa na Source, simple research, presentation skills, independent analysis n.k. Tusifanye ukumbi kama kituo cha majungu. Hata ukweli usioweza kuwakilishwa vizuri ni majungu tu.
Kwa maoni yangu, ninawaomba wote waliotajwa wasijibu chochote. Hii itasaidia sana katika kulinda heshima ya jamvi na jamii kwa ujumla. Ninasema hivi nikiamini uhuru wa kujieleza, lakini kila uhuru una mipaka yake.
Kujibiwa tuhuma kama hizi kuta encourage watu kuzusha mambo yasiyo na maana kwasababu tu watu fulani wapo hapa Jamvini.
Si ajabu siku nitakaposalimiana na Halima Mdee basi ikawekwa tarehe, saa na mahali halafu ikawekwa habari ya uchafu.
Tutumie fursa hizi kubadilishana mawazo, kupingana, kukubaliana kwa mustakabali wa taifa. We must have health debate based on constructive criticism. Majungu ni silaha muhimu sana kwa wasiowerevu.