Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike?

Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike?

Sidhani kama ni kweli huenda mlikuwa kijiweni mnakunywa kahawa tu, Kitilya ninayemfahamu hawezi kujadili kama ulivyonukuu humu, hata hivyo yeyote ndani ya CDM anaweza kugombea ni kadri watakavyokubaliana, hii habari ya kuwatia watu maneno sidhani kama ina uhai. Kuhusu tofauti ningeshangaa kama huko CDM wangekaa bila kutofautiana umesahau ule usemi kama mnakubaliana kila kitu basi mmoja wenu hana uwezo wa kufikiri!
 
Mkuu Matola,

Unataka Dr. Kitila akurupuke kujibu kabla hajasoma posts za wengine humu? Unataka awe mkurupukaji kama wale wengine? Unajua hapa JF ni kama tunaongea ni kama kikao,haitakuwa ustaarabu kuanza kuchangia mada inayokuhusu kabla ya kusikiliza wenzako wanasemaje.
........Basi inawezakana alitumia miaka 10 kufanya PHD yake, hili liko wazi kabisa, wala haliitaji kujiumauma hapa swala ni kweli Kitila Mkumbo aliyasema haya au hapana?
 
........Basi inawezakana alitumia miaka 10 kufanya PHD yake, hili liko wazi kabisa, wala haliitaji kujiumauma hapa swala ni kweli Kitila Mkumbo aliyasema haya au hapana?

Kitila ni msomi na mshauri wa chadema kama kuna jambo linafuka moshi mlitaka afiche?
 
Sihamini kama viongozi wa Chadema wanaweza kufanya madudu kama wafanyavyo magamba,
viongozi wa chadema wanafaamu taratibu zote za kumpata kiongozi wa kusimama 2015 kwahiyo
tusubiri vikao halali ndivyo vitakavyo amua nani atangulie mbele kupeperusha bendera ya chama
 
katika mambo ambayo sitegemei kusikia kutoka kwa Kitila ni kukiri hadharani kwamba alizungumza mambo hayo kwani inategemea kama wakati wake wa kuweka wazi umefika au la lakini pia itategemea alizungumza kwa dhamira gani? Pengine alikuwa anakusanya maoni kama mtafiti kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa mvutano huo ndani ya chadema.
 
Akitoake Kitila atasema ni uongo ndilo jibu jepesi kuliko yote.
 
Sidhani kama ni kweli huenda mlikuwa kijiweni mnakunywa kahawa tu, Kitilya ninayemfahamu hawezi kujadili kama ulivyonukuu humu, hata hivyo yeyote ndani ya CDM anaweza kugombea ni kadri watakavyokubaliana, hii habari ya kuwatia watu maneno sidhani kama ina uhai. Kuhusu tofauti ningeshangaa kama huko CDM wangekaa bila kutofautiana umesahau ule usemi kama mnakubaliana kila kitu basi mmoja wenu hana uwezo wa kufikiri!

Wengi tunamfahamu Kitila na ametufundisha chuo kikuu cha Dar es salaam lakini hiyo haitoshi mimi kumsemea
 
Gamba mkubwa wewe,nani kakuambia kuna vita Chadema,Chadema tunautaratibu wake wa kumpata mgombea.

Na wewe ulikuwepo Uingereza tupe data kama unazo badala ya kupayuka hovyo hapa.
 
Kwanza kitila mkumbe tarehe tisa march nimemuona hill park sasa cjui anavyosema alikuwa nae ngambo labda ni kitila mwingine, jambo lingine ni kwamba hata angekuwa nae navyomfamu mkumbo asingeweza ongea hayo mambo, lakini hata kama angesema hakuna mtu asiyejua kama dr slaa anaushawishi mkubwa ndani ya umma wa watanzania japo mbowe nae yupo makini katika siasa na kuimarisha chama, na mwisho chadema kina mbinu zake za kusimamisha wagombea nani alijua kama slaa angegombea 2010! Inawezekana 2015 wakasimama wengine kadri ya upepo utakavyokuwa kama kina mnyika,lissu,zitto kama katiba mpya itamruhusu.
 
Useless thread, plenty of members speaks on behalf of Kitila Mkumbo instead of himself while he's online!!....clown's show.
 
CHADEMA msikubali kuwa mnachokozeka kirahisi!! Kwani mkikaa kimya kitawapata nini?
 
SLAA anajisumbua. Kazi yake kuu ilikuwa ni kukijengea chama umaarufu na kwa sababu hiyo atalazimika kukaa pembeni wenye chama washike hatamu. Mkuu au umesahau kazi ya ule mpira wa kiume? ukishamaliza kazi sharti utupwe.

Mmejipanga vizuri kweli. tatizo hamna akili mnashindwa kuconceal intentions zenu kitu ambacho ni cha muhimu sana kwenye Propaganda. Sijui mnawasilianaje na hii itakuja kuwacost sana huko mbeleni sababu hamtakuwa huru hata kidogo, Uza kila kitu hata wewe mwenyewe jiuze ila sio kuuza uhuru wako.

Kwa kifupi, na haya majibu sijapewa na mtu kama nyie mlivyoelekezwa kuichangia hii mada haraka haraka. Mbowe ana Uhuru wa kuwa na nia ya Kugombea Urais 2015 kama ambavyo DR Slaa ana uhuru huo kama ambavyo Baba zenu na Mana zenu wana uhuru huo pia wa kuwa na nia ya kugombea na ama kutaka kukamilisha nia hizo kupitia CCM, CHADEMA, CUF n.k

Hivyo huu hauwezi kuwa ni mpasuko. msifikiri watu wote ni wajinga wa kuyachukulia matatizo yaliyo CCM ni lazima yawepo na kwenye vyama vingine vya siasa.

CCM ni kama mtu mzee sana alafu asiyemjua Mungu, ambaye zaidi ya kupungukiwa na nguvu za mwili kutokana na Umri na Maradhi ya kiutu uzima labda lakini ni muoga sana wa kifo hivyo hata kivuli chake anaweza kudhani ni Malaika mtoa roho amekuja kummaliza.
 
Kwani kukiwa na Mpasuko ndiyo nini bana? Ni jambo la kawaida tu ila baada ya uchaguzi, wanarudi kuwa kitu kimoja.

Mpasuko siyo jambo baya kabisa duniani. Hata Baba na Mama yako wameungwa kwa Mpasuko, sembuse Chadema?

Kitila usijibu hata neno moja hapa maana utakuwa unamfukuza Kichaa aliyekuchukulia nguo ukioga.
 
Kwanza kitila mkumbe tarehe tisa march nimemuona hill park sasa cjui anavyosema alikuwa nae ngambo labda ni kitila mwingine, jambo lingine ni kwamba hata angekuwa nae navyomfamu mkumbo asingeweza ongea hayo mambo, lakini hata kama angesema hakuna mtu asiyejua kama dr slaa anaushawishi mkubwa ndani ya umma wa watanzania japo mbowe nae yupo makini katika siasa na kuimarisha chama, na mwisho chadema kina mbinu zake za kusimamisha wagombea nani alijua kama slaa angegombea 2010! Inawezekana 2015 wakasimama wengine kadri ya upepo utakavyokuwa kama kina mnyika,lissu,zitto kama katiba mpya itamruhusu.

Kitila alirudi kutoka safari tarehe 10 machi 2012 lakini sijui alikokuwa acha uongo wewe
 
mbona nasikia ni Shibuda ndio mgombea 2015
 
Kwani kukiwa na Mpasuko ndiyo nini bana? Ni jambo la kawaida tu ila baada ya uchaguzi, wanarudi kuwa kitu kimoja.

Mpasuko siyo jambo baya kabisa duniani. Hata Baba na Mama yako wameungwa kwa Mpasuko, sembuse Chadema?

Kitila usijibu hata neno moja hapa maana utakuwa unamfukuza Kichaa aliyekuchukulia nguo ukioga.

Kama ni jambo la kawaida unatafuta nini kwenye thread hii? ungesoma na kuondoka zako tuachie sisi tunaoona kwamba kuna mantiki ya kujadili
 
si Mbowe wala Slaa anayefaa kuwa Rais wa Nchi hii labda kwa upinzani mngemsimamisha Lipumba huyu ana sifa za kuwa Rais.
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom