Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike?

Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike?

Hapana hii ni ya uhakika kabisa kutoka kwa mshuri wa chadema bwana kitila mkumbo ndio alievunja ukimya huu,si habari ya kufikirika kama zile za kina membe,lowassa na sitta kwamba wanautaka urais.

Mkuu wewe ndiye uliyekuwa London na Dr. Mkumbo wakati anasema hayo maneno?
 
Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012.

Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa. Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.

Wanaomuunga mkono Dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko Mbowe lakini pia kwamba Dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo Dk. Slaa anaweza kuwa Rais ajaye.

Kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa Mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao. My take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015. Source: Nilikuwa Uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu Kitila.

Hii kitu mbona iko hapa muda mrefu mpaka slaa mwenyewe tulikua nae akiichungulia nyie mko wapi,sio siri tena hii,amkeni usingizini,yamewakuta safari hii,tunajaribu kuwasaidia.
 
Ndugu yangu hivi huyo namba 5 kweli ana sifa za kugombea urais kweli au umeamua kuwaliwaza wana Chadema.
 
Tatizo wana CHADEMA walio wengi bado wanabeza kuwepo kwa mpasuko huo, afadhali wewe KIM KARDASH umekubali ukweli na kutoa mapendekezo yako. Kama ulivyosema, tumezoea kuona vyama vya upinzani vikiibuka na kuzama kila kunapokucha na mifano mizuri ni hiyo uliyoitoa. Tofauti hizo zinazoleta mpasuko zisipo rekebishwa mapema hii CDM nayo itabaki historia kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi ya Mrema.

Mkuu tofauti ndio uhai wa chama. Chama kimeishakomaa hivyo kila mtu ndani ya Chama anaamini akipewa kupeperusha bendera ya Chama basi chama kitambeba. Ikulu ni tamu mzee kila mtu anataka awepo pale.
 
Mkuu wewe ndiye uliyekuwa London na Dr. Mkumbo wakati anasema hayo maneno?

kwani kakanusha mkuu,maana nayeye alionekana akichungulia pia iliokuja first time,ni kama zile za lowasa kutuma sms akiwa kitandani ujerumani tu.
 
Huyo Kitila au Mbowe au Slaa, hawajui kama kuna vikao halali vya CHADEMA ambavyo huwa vinapitisha majina ya wagombea katika nafasi za urais na ubunge? Au hivi sasa ndani ya chadema wanateuana tu, kwa hiyo wanahofia kwamba mtu fulani anaweza teuliwa na mwingine asiteuliwe?

Yaani nyie magamba hamuishi kuibua visa vya mitaani na kuvihuisha vionekane vya kweli. No wonder mtaendelea kuaibika pale ukweli unapowekwa hadharani. Ni bahati ilioje kwamba JF hatutumii majina halisi, maana waweza kuwa Wasira au Kikwete weye, na ikawa ni aibu kubwa pale ukweli ukiwa wazi; ndo mnaishia kusema nilikuwa natania, unatania kwenye umati?
 
Hakuna ubishi kwamba chadema ndio chama kikuu cha upinzani angalau kwa sasa nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na cuf ambao nao waliirithi kutoka kwa NCCR-MAGEUZI ile ya Mrema na Marando ambae kwa sasa yuko chadema huku Mrema yeye akiwa na chama "chake" siku hizi.

Lakini katika hali ya kusikitisha taarifa kutoka chanzo cha kuaminika(mshauri mkuu wa chadema)zinaeleza kwamba ndani ya chedema kuna mpasuka mkubwa kuhusu nani anapswa kuandaliwa kugombea urai kati ya mwenyekiti mbowe na katibu dr slaa.Ama hakika hii si habari njema sana kwa wapenda demokrasia na mabadiliko kiujumla.

Ushauri wangu ili kunusuru hali hii ya mpasuko isizidi kusambaa,Mbowe na slaa wake pembeni,hii itawavunja nguvu wapambe wao,watakuwa hawana tena kinachowatofautisha na pia itwapa muda mzuri mwenyekiti na katibu wake kushiriki mchakato huru wa kuitafutia chadema mgombea akaekidhi matarajio ya chama hicho ambayo siamini kama ni just kuwwa chama kikuu cha upinzani tu.

Mi naanza kuonyesha njia,majina haya sita kati yao anaweza kuipeperusha vyema bendera ya chadema kwenye urais.

1:Kitila Mkumbo(dr)
2:Zitto Kabwe
3:Halima Mdee
4:Abdallah Safari(prof)
5:Godbless Lema
6:Tundu Lisu

Nawasilisha.

hapo kwenye red umetafakari kwa umakini au umekurupuka!
 
Kwenye nyekundu hapo, ni mzigo kwa chama hivi sasa. Wakazi wa Arusha wanajuuuta kumchagua. matukio ya uharibifu yamezidi jijini hapa, Watalii wengi hivi sasa hawaendi tena kuhofia usalama wao na sasa wengi wanakwenga mikoa ya morogoro, kigoma na kwingine. Watu wenye busara zao jijini Arusha tunaona kama tumevuliwa nguo kutokana na watu wote wa jiji hili kuonekana kama ni wahuni tu. Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, lakini muda wote huo Mbunge huyo amekuwa akilumbana tu na Meya wa JIJI bila sababu yoyote ya msingi. Hakuna ambalo vijana wamekwishalipata pamoja na kwamba ndiyo waliompa umaarufu huo.
 
Ndugu yangu hivi huyo namba 5 kweli ana sifa za kugombea urais kweli au umeamua kuwaliwaza wana Chadema.

Mkuu huyo namba tano hata ubunge wa jiji la Arusha hatapata tena. Watu wa Arusha wamechoka naye japo bado wanaipenda CDM. Wanasema amekuwa ngumi mkononi mno haangalii maendeleo ya jiji la Arusha. Kuna mtu alinipeleka stend kuu ya mabasi hapa Arusha imebana kweli akaniambia Mbunge na Halmashauri hawana mpango wowote na stend mpya. Pia wanasema hawasikii mipango ya kuindeleza Arusha zaidi ya shari tu.
 
kitila mkumbo-msahuri mkuu wa chadema,sio mwanahalisi.
Weka habari hiyo hapa kama alivyosema..Weka link!
Hiyo uliyoweka hapo juu hamna kitu maana toka jana tumeidiscuss na kuona ni utunzi na usanii wa mtu!
 
Hapana hii ni ya uhakika kabisa kutoka kwa mshuri wa chadema bwana kitila mkumbo ndio alievunja ukimya huu,si habari ya kufikirika kama zile za kina membe,lowassa na sitta kwamba wanautaka urais.

Una uhakika gani kwamba mshauri wa CHADEMA ameyasema hayo?
 
Kwenye nyekundu hapo, ni mzigo kwa chama hivi sasa. Wakazi wa Arusha wanajuuuta kumchagua. matukio ya uharibifu yamezidi jijini hapa, Watalii wengi hivi sasa hawaendi tena kuhofia usalama wao na sasa wengi wanakwenga mikoa ya morogoro, kigoma na kwingine. Watu wenye busara zao jijini Arusha tunaona kama tumevuliwa nguo kutokana na watu wote wa jiji hili kuonekana kama ni wahuni tu. Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, lakini muda wote huo Mbunge huyo amekuwa akilumbana tu na Meya wa JIJI bila sababu yoyote ya msingi. Hakuna ambalo vijana wamekwishalipata pamoja na kwamba ndiyo waliompa umaarufu huo.

Mkuu huo ni ukweli hata kama watabisha. Mimi binafsi nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Lema japokuwa si mpiga kura wa Arusha ila nilimsikia akiongea kwenye kipindi cha Mchakato Majimboni. Niliurahia jinsi alivyokuwa akijieleza na nikasema jamaa akishinda nitakunywa chupa moja ya mvinyo; jamaa akashinda nikanywa mvinyo chupa moja lakini baada ya kuona anayoyafanya ilibidi niutapike mvinyo. Angeacha shari aka concentrate kwenye kuhudumia wapiga kura angeweza kuwa Mbunge wa kudumu lakini kwa hali hii asiombe uchaguzi mdogo hiyo tarehe 5/04/2012.
 
mshauri mkuu wa chadema ndugu, kitila mkumbo alitembelea uingereza katika miji ya london na readings kuanzia tarehe 5 machi na 6 machi 2012 na kuondoka tarehe 10 machi, 2012.

miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kati ya freeman mbowe na dk. Slaa. mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.

wanaomuunga mkono dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko mbowe lakini pia kwamba dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo dk. Slaa anaweza kuwa rais ajaye.

kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. my take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa ccm katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015. source: Nilikuwa uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu kitila.

unapima joto eeh, mtasema sana
 
Kabla hujaandika chochote, hebu chukua muda utafakari uelewa wa hadhira yako. Unaoneka mpaka kwenye medula oblangata yako nini lengo la uzi wako. Propaganda huwa hazifanywi hivyo. Jipange upya
 
Mkuu tofauti ndio uhai wa chama. Chama kimeishakomaa hivyo kila mtu ndani ya Chama anaamini akipewa kupeperusha bendera ya Chama basi chama kitambeba. Ikulu ni tamu mzee kila mtu anataka awepo pale.

Aiseee! hapo kwenye red mkuu, tofauti huleta migogoro na mipasuko katika chama vitu ambavyo mwisho wa siku na yaliyoikumba NCCR Mageuzi na wengine.
 
1. Hakuna mpasuko

2. Wewe unatamani kupandikiza mpasuko.

3. Chadema wana utaratibu thabiti hawana haja ya kuweweseka.

4. Dhana hii umeitoa kwenye kinachoendelea CCM, ambayo inawahusu CCM tu hakuna anayeishadidia kwa sababu mwamuzi wa mwisho ni mpiga kura pamoja na rubuni zinazotumiwa.

5. Hujatueleza tufanye sasa ili tunusurike na hili; kwa maana hiyo unachufua hali ya hewa tu.

NAKUSHAURI ZUNGUMZIA MAMBO MUHIMU YA TAIFA, WAACHIE UMBEYA WAMBEYA
 
Back
Top Bottom