Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpasuko CHADEMA, Nini kifanyike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Mar 22, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012.


  Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa. Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.

  Wanaomuunga mkono Dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko Mbowe lakini pia kwamba Dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo Dk. Slaa anaweza kuwa Rais ajaye.  Kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa Mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao. My take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


  Wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015. Source: Nilikuwa Uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu Kitila.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tiba .......kama hawataelewana chadema inaweza kuwajenga vijana wapya kama John Mnyika na Zitto Kabwe kabla ya mwaka 2015.

  Tamaa ya nani atakiwa kukibeba chama kwenda ikulu imeua vyama vingi sana
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  SLAA anajisumbua. Kazi yake kuu ilikuwa ni kukijengea chama umaarufu na kwa sababu hiyo atalazimika kukaa pembeni wenye chama washike hatamu. Mkuu au umesahau kazi ya ul ***********? ukishamaliza kazi sharti utupwe.
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Haya ni majungu online
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ili Mradi Kitila yupo hapa Jamvini atatueleza kwa kina kama hayo maneno aliyasema na kama alisema ndio hali halisi au yalikuwa maoni yake ,Lakini Mbowe amesikika akisema hatasimama mwaka 2015
   
 6. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Tuko bize na arumeru na nasari wetu,2015 haipingiki slaa ndio tumaini letu sio lowasa,6,membe wala lipumba.**********
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wafuasi ndio wanaleta mvutano kila kambi ikitaka mtu wao ili chama kikishika dola matunda yanakuwa matamu. Wala sishangai nilitegemea sana mgongano huu kutokea.
   
 8. P

  Pelege Senior Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gamba mkubwa wewe,nani kakuambia kuna vita Chadema,Chadema tunautaratibu wake wa kumpata mgombea.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kitila Mkumbo hawezi kwenda Low kiasi hiki kueleza mambo ambayo hayapo, labda yule wa Hybrid ya Ilonga!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa yako mpasuko umeanzia mwanza , Wenje kamshikia mtu pisto Mbele ya Katibu wenu Mkuu huyo. Sasa sijui nani atasuluhisha wakati Wenje yuko upande wa Mbowe na ndiyo maana alimdharau SLAA na kuamua kutoa pisto.
   
 11. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siwaniweke jembe LISSU, nahakika ndiye rais ninaemuota na ninatamani sana.
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa jinsi ninavyofahamu uadilifu wa Kitila, nitashangaa sana kama aliweza kuwaeleza ninyi hizo siri za ndani za chama. Na kama amefanya hivyo basi inawezekana aliwaamini watu wasio waaminifu, wasio na kifua cha kutunza mambo, ambao mwisho wa siku wameamua kuweka habari hizo mtandaoni kama hivi. Ni aibu sana kujua kwamba habari za chama zimevuja kupitia kwa mtu fulani ambaye anaheshima kubwa ndani ya chama. Tutayaongea haya kwenye vikao vyetu.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Thread za kipumbavu ndio hizi.... Mshauri wa CHADEMA akaongee mambo ya CHADEMA kwa wabeba mabox!!?? this is more than a craaaaaap!!
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wanao watu wengi wazuri wanaoweza kuipeleka CHADEMA magogoni, si lazima awe DR na Mbowe.
   
 15. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Huo sio mpasuko. Ndio demokrasia. Ila they need to reach a common amicable agreement. Kwamba kusiwepo tofauti ya maoni, hiyo sio sahihi. CDM ni makini hawatafarakana kwa hilo dogo tu.
   
 16. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  si Mbowe wala Slaa anayefaa kuwa Rais wa Nchi hii labda kwa upinzani mngemsimamisha Lipumba huyu ana sifa za kuwa Rais.
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nimekubali Information is power!
  Usipojua kitu unaongea utumbo tu!
  Unatakiwa uulize ilikuwaje ndipo uje hapa kuandika "mangure" yako hapa!
   
 18. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  It is high time the chaggas (owners) took reigns of power in CDM!
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mpasuko katika vyama vya siasa hasa vya upinzani mwisho wake huwa ni kufukuzana na baada ya hapo ni vyama hivyo kupoteza umaarufu wa kisiasa na kubaki majina tu....ngoja tuona mwisho wa hili.
   
 20. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani heshima ya Kamanda Mbowe haijashuka kwa yeye kumpisha Slaa.Kwanza ameweza kupata heshima zaidi kwa kuonyesha nia yake ya dhati ya kukijenga chama.

  Hoja ulizozileta hapa jamvini ni majungu
   
Loading...