Mpango wa kumng'oa Dr. Ndalichako

Status
Not open for further replies.
Hawa wenzetu wamezidi sasa, kila kitu watakachokiota na kuja nacho kwa public wanataka wakubaliwe tu! safari hii hakuna kitu kama hicho,

kwanza si kweli kuwa ana genge la watu wanaotaka kuhujumu elimu yetu, huu ni ujinga sana, Dr, Ndalichako hawezi kuhujumu elimu yetu, kwanza ili iweje na yeye ili apate nini, huu ni ujinga sana na upumbavu wa hali ya juu, wamemtafuta kila kona sasa wanataka kumbambikizia hili, kwani hiyo tume iliyoundwa na Waziri mkuu inaongozwa na mtu wa dini gani? kama na mwislamu mwenzao basi Dr. amekwisha, kama ni mkristu haki itatendeka,

pili, Dr. Ndarichako yeye ni mtendaji tu! kumbukeni kuwa kuna mwenyekiti wa baraza la mitihani ambaye kila Dr. anachokifanya lazima am-consult yeye au baraza la Necta, pia, Dr. hatungi mitihani, hasahihishi mitihani ila anasimamia tu ndo maana yule mtu wa IT aliondolewa baada ya kuzembea!!

Tatu, Waislamu wanataka aondolewe lakini hawasemi wanamtaka nani? je akija mkristu mwingine na hali ikawa ndo hyo hyo watafanyaje?
je akija mwislamu mwenzao na bado hali ikawa hyo hyo watafanyaje? wata-msalia Albadri?
je akija mwislamu mwenzao wakafaulu sana pasipo halali na tukawa na kizazi cha kijinga watafurahi?
Serikali hasa waziri mkuu chonde chonde acha acha kumwondoa Dr. Ndarichako Necta
Rais kikwete aliwahi kuwaambia kuwa " Mnaona wenzenu wanavyowekeza katika elimu dunia! na ninyi mfanye hivo hvo"

Akija Mwislamu mwenzao watafaulu kwa kuwa alama za ufailu zitashushwa kama alivyofanya Kawambwa asijue kwa kufanya hivyo anazalisha mazezeta ambao watashindwa kufanya lo lote mbele ya safari. Yangu macho.
 
Ndalichako, hafai kabisa huyu, amewahujumu Waislaam waziwazi, aliposhtukiwa akajidai eti kompyuta!

Kwani yeye ndiye anawashikia kalamu? Hii issue ingekuwa na mantiki kidogo kama yale makosa yaliyofanyika kwenye Islamic Knowledge yangefanyika kwenye somk jingine. Jivi mtu akipata A kwenye IK na kisha akapata D na F kwenye masomo mengine itamsaidia nini mbele ya safari?
 
Kwani yeye ndiye anawashikia kalamu? Hii issue ingekuwa na mantiki kidogo kama yale makosa yaliyofanyika kwenye Islamic Knowledge yangefanyika kwenye somk jingine. Jivi mtu akipata A kwenye IK na kisha akapata D na F kwenye masomo mengine itamsaidia nini mbele ya safari?
kinauche
===>Mimi pia nashanga,labda linasaidia kwenda kusoma kozi kama Sharia Law kwenye vyuo vinavyotoa shahada hizo.
 
Last edited by a moderator:
huyu Dr alinifundisha masomo ya Measurement and Evaluation in education EP 202 & 402.
nilimkubali sana sana kwenye taaluma yake hii.

sijui ni kosa gani alilolifanya hadi watu wamwone kwamba hafai lkn kwa taaluma yake hii juu ya mambo ya mitihan watu wasimbeze manake anaijua vyema na yuko competent sana kwenye haya mambo ya testing and eveluation

Unafikiri Kuna kosa kiongozj, NI utaratibu wa kuendeleza Taifa la wajinga, wafaulu wasio Na sifa
 
Ifike sehemu tuwaheshimu watu wenye maono juu ya taifa letu,siasa watanzania hazitupeleki popote kizazi cha sasa tuwe macho,ninaamini hata Nyerere angetokea leo hasinge pata nafasi ya kuongoza nchi hii maana wale wote wenye dira bora ya nchi hii tuntwapiga mawe tukiwa juu ya mti ili wasituone watu lakini zambi ni zambi hata ukiifanya usiku.:shocked:
 
Ndiyo sababu katika harakati hizi kila siku kelele na malalamishi ya hovyo humlenga ndalichako yaani ubaguzi na chuki za kidini.......

Sijawasikia hawa ndugu zangu wakimlalamikia au kumkejeri kawambwa kumbe kunaajenda ya siri nyuma yake....
Hawawezi kumlaumu Kawambwa kwani ni wa -kwao.Hata ikitokea ndege au gari limepata ajali likasababisha madhara wanaanzia kuuliza rubani/dereva ni wa upande upi kama si wakwao huwa ni sababu toshA kusema ni dhuluma dhidi yao!
 
Tina
===>Sina uhakika na ukweli wa tuhuma hizi,nchi hii ukifanya kazi yako kitaalamu na vizuri na ukiwa mbali na wanasiasa basi wewe hudumu hata siku moja,huyu mama tangu ameingia madarakani kiwango cha uwizi wa mitihani kimepungua kwa kiwango kikubwa sana,na heshima ya bara za la mitihani imeongezeka kwa kiwango cha juu sana.
===>Siasa zimesababisha tunasahau mambo ambayo yanasababisha wanafunzi kufeli nitataja yafuatayo:
a--Udahaili wa walimu kuanzia miaka ya 2000 hapa kulifanyika madudu ya hali ya juu,walimu wengi walifoji vyeti vya shule hasa walimu wa grade A ambao wao ndio wafundishaji au wazalishaji wa mwanzo kabisa wa watoto wetu,kuna walimu wengi sana waliotumia vyeti feki na pia kutumia majina ya watu kupata nafasi za ualimu hawa ndio wauaji wa kwanza kabisa wa watoto wetu.
b--Kufutwa kwa mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili,hapa napo pameongza balaa kubwa sana maana wanafunzi wanafundishwa na walimu wabovu halafu wanapitishwa bila mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili unategemea hapa patapatikana wanafunzi wa aina gani?
c--Kubadilishwa kwa mitaala bila mpangilio na kufuta au kuunganisha baadhi ya masomo mfano kuna wanafunzi wa hapa hapa nchini hawakuwahi kusoma Physics,Chemistry na Biology haya masomo yalichanganywa sijui yakaitwa nini sijui,kufutwa kwa masomo ya ufundi kwenye shule za ufundi kama Tanga Tech,Moshi Tech,Mtwara Tech,Ifunda Tech,kufutwa kwa masomo ya Commerce na Bookkeeping hii ilitoka kipindi cha Mh Mungai
d--Kupuuzwa kwa Madai ya walimu,hapa ndio panatisha kabisa,hasa kwenye shule za kata na za serikali,hembu jiulize mwalimu ambae amefoji cheti/ametumia jina la mtu,hajui vizuri kufundisha,kugoma anaogopa maana akigoma hapati kazi sehemu nyingine yoyote anaamua kupiga magumashi darasani halafu anakata mitaa kwenda kutafuta pesa ya ziada unategemea nini hapo zaidi ya sifuri tu?
===>Wana JF naamini wahusika wanayaona haya,huyu mama Ndalichako anaonewa tu,amekataa kudhalilisha Phd yake,nafikiri kwa watendaji wengine kuna cha kujifunza hapa,Tumia elimu yako kuisadia nchi hii,sio kuwasaidia wanasiasa kuendelea kututilia vilema vya akili watoto wetu,wasomi wetu msitusaliti na wala msiwasaliti watanzania wenzenu kuweni majasiri wa kukataa kufanya mambo ambayo hayana tija kwa taifa hili.
Wakiyajua haya watanzania wote tutapona,
 
Ndalichako, hafai kabisa huyu, amewahujumu Waislaam waziwazi, aliposhtukiwa akajidai eti kompyuta!

Hoping u r ok Maadam.Usiwe extremest kiasi hiki.Akiondolewa Dk Ndalichako hakutabadili hali kwani ni sawa na kupaka rangi ukuta ukidhania umeziba nyufa. Kikubwa ni kuzingatia yote ILIM DUNIA na ILIM AKHERA hebu jaribuni ilo kama hamtafanikiwa niite mchochezi.Who is Joyce Vs[(Kikwete,Bilali,Shein,Seif ,Kawaambwa),Rashid Othman,Saidi Mwema et al]
 
Mi nawashangaa watu wanaomshambulia huyu mama. Kazi necta sio kufaulisha watoto ni kupima uwezo wao wa maarifa waliyoyapata toka shuleni yaliyosimaiwa na wizara ya elimu. Kama ufundishaji ni mbovu, anayehusika ni wizara si Ndalichako.

well said!
 
Huyu mama bogus kabisa hivi nyie mnaomtetea ni HAKI KWELI SOMO LIGAWIWE MARKS KWA AVERAGE YA 3 BADALA YA 2?hata kama formula ilikosewa jee waliwahi fanya manual kuhakiki majibu?jee ni kwa muda gani formula hiyo imewanyima A na B wanafunzi wa islamic studies?nina uhakika huyu mama angekua muislam angeshatolewa siku nyingi pale necta kwa nguvu ya kanisa iliyonayo nchi hii.kwa kuwa ni mkristo mpaka leo anakula mshahara,inanikumbusha madudu ya ngeleja lakini wakristo hawayakuyaona mpaka rais alipobadilisha baraza

Kama alivyo mtumishi yeyote wa umma kuna siku Ndalichako atahamishwa ama atastaafu! Jambo muhimu ni kuangalia utendaji wa NECTA ktk mustakabali mzima wa kuboresha elimu yetu ili tupate wahitimu wenye weledi na wanaokubalika hata vyuo vya nje ya nchi yetu!

Nakumbuka wizi wa kwanza kwanza wa mitihani ilikua ktkt ya miaka 80 wakati huo nikiwa nasoma shule ya sekondari ya Tambaza hapa Dar! Kwa wale mliokua shule nyakati hizo ntakua ni mashahidi wangu!

Wizi wa mitihani uliendelea ukichagizwa na wamiliki wa shule binafsi za sekondari kutaka wanafunzi wao wafaulu ili shule zao zipate soko zaidi na baadhi ya shule za sekondari za Seminari za Kiislamu,kwa wanaokumbuka shule ya Al haramain! pale Upanga,Dsm!

Walimu wa shule za umma walianza kugundua kwamba wanafunzi wengi toka baadhi ya shule walikua na ufaulu wa juu sana lakini wakiingia kidato cha Tano wanaonekana wako wachovu sana! Ukaanza uchuguzi na baadaye hii tabia kwa kiasi kikubwa ikakokomeshwa ktk kipindi cha uongozi wa Dr. Ndalichako. Kudhibitiwa kwa wizi wa mitihani kumemuacha Dr. Ndalichako na maadui wengi,kuanzia wanasiasa,wamiliki wa shule binafsi na jamaa zangu wanaosingizia mfumo Kristo!!
 
Napata wasiwasi kama hizi barua si kazi ya kutengeneza (fake). Hazionekani kuwa na hata mtiririko unaoleweka au kuweka majina dhahiri ilhali ni mpango wa siri; sidhani viongozi wa waislamu ni vilaza kiasi hicho. Tuwe makini tunapojadili taarifa kama hizi wakati uthibitisho wake haupo wazi (vinginevyo mleta mada atuthibitishie).

Ushauri:
Ndani ya waislamu kuna wasomi wengi tu wenye uwezo, basi watumie elimu yao kufanya tafiti zinazoweza kuwanasua walipo sasa hivi. Kwa mpango huu basi wanapigana vita ambayo hata adui hawamfahamu. Huko ni kupoteza muda na milele hakitabadilika kitu.

wangekua wamepata elimu nzuri wangeandika barua nzuri pia .... elimu dunia ni muhimu sana!
 
Huyu mama bogus kabisa hivi nyie mnaomtetea ni HAKI KWELI SOMO LIGAWIWE MARKS KWA AVERAGE YA 3 BADALA YA 2?hata kama formula ilikosewa jee waliwahi fanya manual kuhakiki majibu?jee ni kwa muda gani formula hiyo imewanyima A na B wanafunzi wa islamic studies?nina uhakika huyu mama angekua muislam angeshatolewa siku nyingi pale necta kwa nguvu ya kanisa iliyonayo nchi hii.kwa kuwa ni mkristo mpaka leo anakula mshahara,inanikumbusha madudu ya ngeleja lakini wakristo hawayakuyaona mpaka rais alipobadilisha baraza

mbona unazungumzia mtendaji huyu tu awajibike kwa kosa la mtu mwingine wa chini? .... sijakusikia ukisema kina IGP mwema, Kova, othman wa TISS wawjibike kwa makosa ya wanaowaongoza

CHUKI na WIVU mbaya sana ndugu yangu!
 
Kwani yeye ndiye anawashikia kalamu? Hii issue ingekuwa na mantiki kidogo kama yale makosa yaliyofanyika kwenye Islamic Knowledge yangefanyika kwenye somk jingine. Jivi mtu akipata A kwenye IK na kisha akapata D na F kwenye masomo mengine itamsaidia nini mbele ya safari?

hili ndio swali la muhimu .... mimi huwa nawashangaa sana wale wanaopata A au B za masomo ya dini halafu wamechemsha kwingine wanashindwa kupata credits za kuendelea na elimu ya juu ... credits for nothing

it is about time haya masomo ya dini yaondolewe shule za serikali na hata yakibaki yasitambuliwe kwenye assessment na upangaji wa madaraja/matokeo ya mtu .... yafahamike tu kama extra credits!
 
Unafikiri Kuna kosa kiongozj, NI utaratibu wa kuendeleza Taifa la wajinga, wafaulu wasio Na sifa

na hili ndio watanzania hawalioni

ukosefu wa elimu ni mtaji tosha wa mafisadi kuendelea kuongoza nchi na wizi wa rasilimali za taifa

watu hawajiulizi kwa nini hao mafisadi au viongozi watoto wao hawasomi hizi shule za wasiwasi hasa za serikali?
 
Huyu mama nahukumiwa kutokana na dini yake na si kitu kingine......Hizo barua ukiziangalia kwa makini utagundua walio ziandika hawana akili kabis a na niwatupu kichwani.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom