Mpango wa kumng'oa Dr. Ndalichako

Mpango wa kumng'oa Dr. Ndalichako

Status
Not open for further replies.
wakifanikisha hilo waombe na kiarabu iwe ni lugha ya kufundishia ktk skuli zote nchini.
Na ikiwezekana Quran waifanye kuwa dictionary.

Msihofu wote watafaulu tuu bila hata ya kusoma.
Kazi yetu itakuwa ni madrasa tuu, paper likija ni kufumua kwa kwenda mbele au sio maulamaaa.
 
Napata wasiwasi kama hizi barua si kazi ya kutengeneza (fake). Hazionekani kuwa na hata mtiririko unaoleweka au kuweka majina dhahiri ilhali ni mpango wa siri; sidhani viongozi wa waislamu ni vilaza kiasi hicho. Tuwe makini tunapojadili taarifa kama hizi wakati uthibitisho wake haupo wazi (vinginevyo mleta mada atuthibitishie).

Ushauri:
Ndani ya waislamu kuna wasomi wengi tu wenye uwezo, basi watumie elimu yao kufanya tafiti zinazoweza kuwanasua walipo sasa hivi. Kwa mpango huu basi wanapigana vita ambayo hata adui hawamfahamu. Huko ni kupoteza muda na milele hakitabadilika kitu.
 
Machadema yanahangaika kupandikiza chuki kati ya serikali na waislam. Shame at u
 
Mbunge wa Mchinga, Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda (CCM) anatajwa kwenye nyaraka hizo kuwa shujaa wa harakati hizo.

Huyu mbunge ana udugu wa damu na Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa.

bahati nzuri kumbe kiongozi wa wizara ni wa kwao
 
Kosa lake kubwa ni ukristo laiti waziri wa elimu angekuwa mkristo asingekuwa salama.
Mkuu Ngongo,

Angalia usiingie kwenye trap kwa hiyo barua ya kijinga.
 
Last edited by a moderator:
hatuhitaji malumbano yote haya. tunchohitaji ni kimoja tu nacho ni kufuta masomo yote ya dini kwa shule za serikali kuanzia primary mpaka kidato cha sita, kupiga marufuku uvaaji au ubebaji wa aina yoyote ya nguo au kitu chochote chenye kiashiria cha dini. kuzuia baraza la mitihani na wizara ya elimu kujihusisha na mitaala ya dini au kutunga mitihani ya dini au kusahihisha mitihani yoyote ya kidini.
Masomo yoyote ya kidini katika mashule yanayoendeshwa na taasisi za kidini kutokutambuliwa au kujumlishwa katika matokeo ya mitihani yakitaifa.

NI MUHIMU KUTENGANISHA MASUALA YA KIDINI NA ELIMU YETU.
Naunga mkono hoja yako mkuu kwa 100% kwani tusije tukaletewa mabalaa ambayo hana tija.
 
Nyie wafuasi wa Chadema mtahangaika sana mnazuwa upuuzi ili muwatukane Waislam.

Pamoja na kuwa jukwaa hili ni lasiasa lakini kuna mambo tunatakiwa kupinga kulingana na tukio sasa hapa ndugu Ritz HADEMA imetoka wapi? unatakiwa kutuambia kuwa hizo barua sio halali kuliko kukimbilia kukishambbulia chama. Unatakiwa kujua kuwa CHADEMA na CCM sio muhimu sana kuliko Tanzania yetu chamsingi ni kujenga hoja za kuondokana na mabalaa haya ya udini ndugu kwani haikuwa huluka yetu watanzania kuchukiana kwa misingi ya dini zetu sasa tunapaswa kuhoji chanzo na njia za kuondokana nalo.
 
Hii serikali imejaa uswahili wa kupitiliza.Huyu mama ana shida gani? mnashindwa kusimamia elimu mnamuandama Ndalichako!
 
Pamoja na kuwa jukwaa hili ni lasiasa lakini kuna mambo tunatakiwa kupinga kulingana na tukio sasa hapa ndugu Ritz HADEMA imetoka wapi? unatakiwa kutuambia kuwa hizo barua sio halali kuliko kukimbilia kukishambbulia chama. Unatakiwa kujua kuwa CHADEMA na CCM sio muhimu sana kuliko Tanzania yetu chamsingi ni kujenga hoja za kuondokana na mabalaa haya ya udini ndugu kwani haikuwa huluka yetu watanzania kuchukiana kwa misingi ya dini zetu sasa tunapaswa kuhoji chanzo na njia za kuondokana nalo.
Sikiliza wewe hauwezi kunipangia cha kuongea humu ni muda mrefu JF tunajuana kwa ID's zetu.

Imeishajiuliza mbona sijakujibu wewe nimemjibu Mzito Kabwela,

Kama una uchungu mbona haujawakataza wenzako kuwashambulia Waislam wote kwa kejeli na dhihaka.

Huyo niliomjibu ni msemaji wa Chadema humu fuatilia posts zake ni kuisifia Chadema na kuwashambulia Waislam.

Kama roho inakuuma Chadema kutajwa sina cha kukusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Duh! hii ni zaidi ya habari wazee. Kama nchi hii inaendeshwa hivi, tumekwisha.
 
Hawa wenzetu wamezidi sasa, kila kitu watakachokiota na kuja nacho kwa public wanataka wakubaliwe tu! safari hii hakuna kitu kama hicho,

kwanza si kweli kuwa ana genge la watu wanaotaka kuhujumu elimu yetu, huu ni ujinga sana, Dr, Ndalichako hawezi kuhujumu elimu yetu, kwanza ili iweje na yeye ili apate nini, huu ni ujinga sana na upumbavu wa hali ya juu, wamemtafuta kila kona sasa wanataka kumbambikizia hili, kwani hiyo tume iliyoundwa na Waziri mkuu inaongozwa na mtu wa dini gani? kama na mwislamu mwenzao basi Dr. amekwisha, kama ni mkristu haki itatendeka,

pili, Dr. Ndarichako yeye ni mtendaji tu! kumbukeni kuwa kuna mwenyekiti wa baraza la mitihani ambaye kila Dr. anachokifanya lazima am-consult yeye au baraza la Necta, pia, Dr. hatungi mitihani, hasahihishi mitihani ila anasimamia tu ndo maana yule mtu wa IT aliondolewa baada ya kuzembea!!

Tatu, Waislamu wanataka aondolewe lakini hawasemi wanamtaka nani? je akija mkristu mwingine na hali ikawa ndo hyo hyo watafanyaje?
je akija mwislamu mwenzao na bado hali ikawa hyo hyo watafanyaje? wata-msalia Albadri?
je akija mwislamu mwenzao wakafaulu sana pasipo halali na tukawa na kizazi cha kijinga watafurahi?
Serikali hasa waziri mkuu chonde chonde acha acha kumwondoa Dr. Ndarichako Necta
Rais kikwete aliwahi kuwaambia kuwa " Mnaona wenzenu wanavyowekeza katika elimu dunia! na ninyi mfanye hivo hvo"
 
Tina
Kuna mambo mengi nyuma ya pazia kuhusiana na hatima ya Ndalichako ikiwamo mahusiano yake na genge maalumu lenye mahusiano ya siri na nchi moja jirani yenye nia ya kuhujumu mustakabali wa Tanzania ikiwamo elimu na Nyanja nyingine. Kumekuwa na tahadhari kadhaa zilizotolewa kuhusu vikao vya genge hilo lenye nguvu za ajabu na kwa NDalichako kuhusishwa kwake, imekuwa tishio kubwa kwa hatima ya elimu yetu. Kwa sasa bado ni tuhuma na ndio maana ameombwa kupumzika hadi ukweli utakapodhihiri na yeye kuwahi kujihami kwamba anaomba likizo bila malipo ya mwaka mmoja na si kwamba ametakiwa kukaa pembeni.
===>Nafikiri hii ni sababu ya dhaifu sana na ambayo katika hali ya kawaida ni vigumu sana kuiamini,kuna tatizo la wanasiasa kuingilia kazi za kitaalamu mathalani;
1--Nani asiejua kuwa magari makubwa yanaharibu barabara zetu kwa kuzidisha mizigo kwenye magari haya makubwa?hembu iangalie barabara ya CHALINZE-DSM ina hali gani?mnataka kutuambia kuwa ile barabara ilijengwa chini ya kiwango?
2--Nani asiejua kuwa karibu maeneo yote ya wazi yameuzwa katika jiji la DSM?Mama Tibaijuka alipochaguliwa alijaribu kuyarudisha haya maeneo umeshamsikia tena?
Nchi hii ukiwa na msimamo na unachokifanya na ukikataa kufuata wanayotaka wanasiasa basi wewe umeshakuwa mbaya na wanakuchukia,sijui viongozi wetu huwa wanawaza kitu gani?
 
Huyu mama bogus kabisa hivi nyie mnaomtetea ni HAKI KWELI SOMO LIGAWIWE MARKS KWA AVERAGE YA 3 BADALA YA 2?hata kama formula ilikosewa jee waliwahi fanya manual kuhakiki majibu?jee ni kwa muda gani formula hiyo imewanyima A na B wanafunzi wa islamic studies?nina uhakika huyu mama angekua muislam angeshatolewa siku nyingi pale necta kwa nguvu ya kanisa iliyonayo nchi hii.kwa kuwa ni mkristo mpaka leo anakula mshahara,inanikumbusha madudu ya ngeleja lakini wakristo hawayakuyaona mpaka rais alipobadilisha baraza
 
Kwa hiyo ndiyo akina Mtanda wameona waunde Kamati ya kumshughulikia hadi atoke pale. Kwani Waziri wa Elimu si Muislamu mwenzenu, kwa nini asimuondoe kwa mamlaka aliyonayo kama kweli ana makosa ambayo ameyafanya. Rais mwenyewe muislamu mwenzenu sasa sijui mnataka nini. Na kama ni hilo suala la kugawa kwa 3 badala ya mbili, mbona hata ajira za walimu zilikuwa vurugu tupu waliokwisha ajiriwa wakapangiwa tena sasa hapo mbona hamjamwambia mwislamu mwenzenu Shukuru Kawambwa ajiuzulu. Hebu toeni maudini yenu hapa mtatuharibia nchi.
 
Kawambwa ataweweseka sana lakini ukweli nimkuwa uwezo wake ni mdogo sana. Hayo yote ya kumsakama Ndalichako yanawekwa tu na ndugu zake ili kuficha udhaifu wake. Lakini ukweli unabaki pale pale Wizara ya Elimu ina matatizo makubwa ambayo kamwe Kawambwa hawezi kuyatatua badala yake anatumia wenzake kuondoa hoja ya msingi ili tatizo lionekane ni NECTA.

Sasa havi amesaini mkataba kuwa matokeo ya mwaka huu ufaulu utafika 60% na matokeo yake wameweka Dodoso kwenye tovuti ya Wizara eti kupata maoni ya watu lakini kabla hata ya maoni tayari mwelekeo ni kushusha alama ya ufaulu iwe 11% ili ionekane watu wengi wamefaulu. Njia ya dodoso imetumika ili ionekane hayo ni maamuzi ya wadau lakini Wizara ndiyo inataka 11% ufaulu kidato cha Nne. Kama kweli lengo ni maoni kwa nini Wizara imetoa waraka kwa wanavyuo mafunzo ya ualimu kufanya mtihani wa kuingia mwaka wa pili na atakeshindwa kupata 41% anafukuzwa. Kwa nini hapa hawakupeleka dodoso vyuo vya ualimu.

Ona dodoso la ufaulu Kidato cha Nne na Sita tembelea tovuti ya elimu

DODOSO LA UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA NA MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI KATIKA MITIHANI
 
Kuna mambo mengi nyuma ya pazia kuhusiana na hatima ya Ndalichako ikiwamo mahusiano yake na genge maalumu lenye mahusiano ya siri na nchi moja jirani yenye nia ya kuhujumu mustakabali wa Tanzania ikiwamo elimu na Nyanja nyingine. Kumekuwa na tahadhari kadhaa zilizotolewa kuhusu vikao vya genge hilo lenye nguvu za ajabu na kwa NDalichako kuhusishwa kwake, imekuwa tishio kubwa kwa hatima ya elimu yetu. Kwa sasa bado ni tuhuma na ndio maana ameombwa kupumzika hadi ukweli utakapodhihiri na yeye kuwahi kujihami kwamba anaomba likizo bila malipo ya mwaka mmoja na si kwamba ametakiwa kukaa pembeni.
Tina
===>Sina uhakika na ukweli wa tuhuma hizi,nchi hii ukifanya kazi yako kitaalamu na vizuri na ukiwa mbali na wanasiasa basi wewe hudumu hata siku moja,huyu mama tangu ameingia madarakani kiwango cha uwizi wa mitihani kimepungua kwa kiwango kikubwa sana,na heshima ya bara za la mitihani imeongezeka kwa kiwango cha juu sana.
===>Siasa zimesababisha tunasahau mambo ambayo yanasababisha wanafunzi kufeli nitataja yafuatayo:
a--Udahaili wa walimu kuanzia miaka ya 2000 hapa kulifanyika madudu ya hali ya juu,walimu wengi walifoji vyeti vya shule hasa walimu wa grade A ambao wao ndio wafundishaji au wazalishaji wa mwanzo kabisa wa watoto wetu,kuna walimu wengi sana waliotumia vyeti feki na pia kutumia majina ya watu kupata nafasi za ualimu hawa ndio wauaji wa kwanza kabisa wa watoto wetu.
b--Kufutwa kwa mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili,hapa napo pameongza balaa kubwa sana maana wanafunzi wanafundishwa na walimu wabovu halafu wanapitishwa bila mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili unategemea hapa patapatikana wanafunzi wa aina gani?
c--Kubadilishwa kwa mitaala bila mpangilio na kufuta au kuunganisha baadhi ya masomo mfano kuna wanafunzi wa hapa hapa nchini hawakuwahi kusoma Physics,Chemistry na Biology haya masomo yalichanganywa sijui yakaitwa nini sijui,kufutwa kwa masomo ya ufundi kwenye shule za ufundi kama Tanga Tech,Moshi Tech,Mtwara Tech,Ifunda Tech,kufutwa kwa masomo ya Commerce na Bookkeeping hii ilitoka kipindi cha Mh Mungai
d--Kupuuzwa kwa Madai ya walimu,hapa ndio panatisha kabisa,hasa kwenye shule za kata na za serikali,hembu jiulize mwalimu ambae amefoji cheti/ametumia jina la mtu,hajui vizuri kufundisha,kugoma anaogopa maana akigoma hapati kazi sehemu nyingine yoyote anaamua kupiga magumashi darasani halafu anakata mitaa kwenda kutafuta pesa ya ziada unategemea nini hapo zaidi ya sifuri tu?
===>Wana JF naamini wahusika wanayaona haya,huyu mama Ndalichako anaonewa tu,amekataa kudhalilisha Phd yake,nafikiri kwa watendaji wengine kuna cha kujifunza hapa,Tumia elimu yako kuisadia nchi hii,sio kuwasaidia wanasiasa kuendelea kututilia vilema vya akili watoto wetu,wasomi wetu msitusaliti na wala msiwasaliti watanzania wenzenu kuweni majasiri wa kukataa kufanya mambo ambayo hayana tija kwa taifa hili.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom